Kishindo IPTL: Yahofiwa Pinda atajiuzulu

Kishindo IPTL: Yahofiwa Pinda atajiuzulu

pinda si anataka urais sasa atawajibika vip?

Kinachoonekana hapo baadae ni kuwa PINDA ATAPINDA TU na kamwe hawezi kujiuzulu. Watakaokuwepo katika ripoti hata kama ni 200 bora wawajibishwe kuliko kuvunja baraza la mawaziri na kuanza kuipanga upya serikali. ILA MUDA NDIO UTAKAOSEMA UFASAHA NGOJA TUSUBIRI
 
kweli hali hii inasikitisha sana hivi watu wanamchezea Mungu CCM hakuna anayemuenzi Mwl Nyerere ni shida Tupu hizo pesa kweli zingeingizwa wizara ya elimu umasikini usingepungua tunaelekea pabaya Mungu atusaidie kwakweli kama mambo yatakuwa hivi machafuko yatatujia ila tuombe Mungu atuondolewa hawa maccm wale wote wanapenda pesa kuliko binadamu tubaki na Amani yetu Mwl aliyoicha.
 
Kimenuka. Kwa hiyo walichakwapua watarudisha au ndo kuwajibishwa tuu kwa kuachia madaraka. Ilitakiwa mtu ikipatikana kaiba afilisishwe na jela juu.
 
Haya maandishi bado siyo uthibitisho wa dhamira yako mtu yeyote anaweza kutunga mandiahi kama haya na kuyaweka hapa.

Kudandia hoja kubaya sana na kwa kufanya hivyo nyie maCCM inafikia hatua hadi mnaandika vitu visivyoeleweka na hii inatokana na kujitahidi kutumia akili za kushikiwa huku za kwako ukiwa umezisahahu chooni.
 
eti mtu anaweza kupewa 1.4b na mtu,eti alimpa tu kama ndugu.watanzania tumelala hadi kero
Hiyo ni ajabu na kweli!

That can happen, only on the land of Kilimanjaro.

Kwamba family friend anaweza kukutumbukizia kwenye accont yako bilioni moja na nusu, na wewe unakuja kuistukia baada ya kwenda kucheki balance, unakuta akaunti yako imetuna, na aliyekuwekea anakutumia sms kuwa amekupatia vijisenti kidogo vya kunywa maji upoze koo!
 
Eh Mwenyezi Mungu wasitiri waadilifu wa nchi hii, mafisadi wanatuangamiza kila kukicha.
 
Utasikia inaundwa Kamati kulichunguza hili suala na maisha yanaendelea..
 
Hivi Pinda ata kama akiondoka hana impact yoyote Tanzania haijawai kuongozwa na PM type kama huyu .
 
Huyu bwana nilimsapoti Kwa nguvu zangu zote lakini bila shaka ametuangusha sana. Sijui ila ameliabisha taifa Kwa kushindwa kutumia nguvu aliyopewa kikatiba. Ila mzimu Wa mbinu zao chafu dhidi ya Waziri mkuu wake mtangulizi zitamtafuna hadi mwisho Wa dahari.

Tatizo alilifikiria zaidi Familia yake kuliko TAIFA lake .Hapo ndipo alipoanza kuharibu.Na marais wetu wa baada ya mwalimu waliponzwa na wake zao.

Ukimwangalia Mkapa na hata Prof wa Kichina wote wameponzwa na wake zao,kutaka maisha ya baada ya urais,pesa na utajiri.Wake hawa wameabudu zaidi MALI kuliko kuliangalia TAIFA,na tunachotakiwa kwa sasa kuminterview hata Mke wa rais kujua anafahamu nini kuhusu TAASISI ya URAIS na anataka kulifanyia nini TAIFA lake.

Pili zile NGOs za wake wa marais zipigwe marufuku na ianzishwe taasisi ambayo itakuwa ya kudumu kama ofisi ya Mke wa Rais awapo madarakani na akiondoka anaondoka yeye na kuiacha NGO/taasisi hiyo ikiendelea kama moja ya taasisi inayomilikiwa na serikali ili kuzishughulikia masuala ya jamii kupitia taasisi hii na hawa donors wanatakiwa kuambiwa kuwa wanachotakiwa kufanya kama wanaifadhili taasisi hii lazima pesa hizo ziwe audited na zawadi zote zitolewazo kwayo ziwe reported na kuelezwa zimepelekwa wapi na kwa nini.Hii itasaidia pia kufuatilia pesa za wafadhili zisitumike kufanyia kampeni za urais.
 
Mkuu hii ni ndoano ya ulimi lazima mkulu au PM wang'oke japo kwa mkulu historia itazingatiwa.

Siku MKULU mmoja akifanyiwa kama BURKINAFASO ndiyo watakapoona umuhimu wa kuogopa kutenda maovu.
 
Na wewe tangu uolewe unaongea maneno ya mtaani kweli sijui kama ndoa imekuvuruga au nini.

Pole sana.Nadhani kwa sababu ulipofunga ndoa wewe na kuchanganyikiwa unadhani watu wote wakifunga NDOA basi wanachanganyikiwa kama wewe.Ila kila siku nitakwambia huna haja ya kutukana mtu,toa hoja yako kama ina mashiko tutaisupport.Vinginevyo utaonekana MPUMBAVU kutokana na UPUMBAVU unaouandika wewe mwenyewe.

Tabia ya MWANAMKE yeyote huonekana kwenye KINYWA chake (Maneno yatokayo kwenye modomo wake)Na ndiyo maana walisema MWANAMKE MPUMBAVU huvunja ndoa yake mwenyewe.

Humjui mtu usimtukane.
 
AZIMIO LA ARUSHA lirudi na LIPEWE MENO MAKALI....huku tunapokwenda nina mashaka sana,kuna watu tumewaamini kiuhalisia hatukapaswa kufanya hivyo...tuko ktk kipindi kigumu sana cha kondoo kuishi na mbwa mwitu zizi moja!
 
Kila mtu anamaono yake na fikra zake siyo mbaya kueleza hisia zako ila siyo lazima wote tukubaliane na wewe, kilichoandikwa ni hisai tu za mwandishi ila ukweli na kipimo cha hoja ya kujiuzuru tutakiona siku ya kusomwa ripoti na baada ya michango ya waheshimiwa wabunge. Kama richmond vile, mkubwa alipima akaona havuki akaamua kuachia ngazi na sivinginevyo. Kwa maslahi furani ya kisiasa kuna watu wangependa iwe hivyo na wewe mwandishi ni mmoja wa hao watu. Na hii imenogeshwa baada ya mtoto wa mkulima kutangaza nia.
 
kujiuzuru kwa Pinda ni ndoto za mchana mtasubiri sana na mtachelewa uchaguzi serikali za mtaa
 
Back
Top Bottom