Kishindo IPTL: Yahofiwa Pinda atajiuzulu

Kishindo IPTL: Yahofiwa Pinda atajiuzulu

Ni afadhali wewe bwana Issenye umeeleza historia nzima ya makampuni haya tangu kuanzishwa kwake, kuuziana kijanja janja, hukumu za mahakama za nchini hapa na makubaliano ya wamiliki kuhusu kesi za mbeleni kusikilizwa na mahakama za kimataifa.

Hapo kwa kweli unaweza kuuona wazi ukwepaji wa kodi za serikali na uvunwaji wa sheria wa mahakama zetu kuhalalisha ufisadi kufanyika.

Sasa nimebadili mwelekeo na nasubiri hiyo tar 28/11 bunge liwake moto na tumbili atafahamika.
 
Weremaaaaaaaaa,mzee wa kubatiza watu majina mweeeeeeee
MKAKATI WA KUPAMBANA NA UMASKINI BINAFSI (MKAKUBI) ndo sera ya watawala wetu
 
Kama jeshi lingekuwa kweli la Wananchi,lingechukua hatu dhidi ya Wezi hawa! Ila kwa kuwa lipo kwa ajili ya CCM hakuna jinsi...
Jeshi la Burkinafaso ndo jeshi hasa la wananchi!
 
Haya maandishi bado siyo uthibitisho wa dhamira yako mtu yeyote anaweza kutunga mandiahi kama haya na kuyaweka hapa.

Kwa akili zako unadhani mtu atakuwa na lengo gani kutunga maandishi ya namna hii na kutaja majina ya watu bila hofu kama hana ushahidi? Acha kutetea wizi. Nadhani kama hali isingekuwa mbaya kama ilivyo wagonjwa kukosa dawa, shule kukosa madawati, wastaafu kushindwa kulipwa etc hakuna ambaye angejali hata kama wangegawana matrilioni. Lakini haiwezekani matatizo yote haya halafu watu wanapeana zawadi za mabilioni ya shilingi. No way!
 
Kwakweli kama ndivyo ilivyo bado tuna safari ndefu sana. Wenzetu wanatupatia misaada lakin wenzetu wanatia mifukoni, sasa kama mkuu wa nchi safari zake zote za nje ni kututaftia hii misaada atawaachaje hawa watu? Nadhani hapa iwe mfano kwa hawa watu waadhibiwe ikiwezekana hata kunyongwa japo sheria yetu hairuhusu.
 
Sasa sisi hizo fedha zinatuhusu nini,wao waibe mpaka basi_Wananchi wahitimu vyuo vikuu wenye GPA Za 5.0
 
Weremaaaaaaaaa,mzee wa kubatiza watu majina mweeeeeeee
MKAKATI WA KUPAMBANA NA UMASKINI BINAFSI (MKAKUBI) ndo sera ya watawala wetu

Teteteeeee...MKAKUBI.... ili la Tanzania pekee hata madikteta hawathubutu lakini ccm wameweza.
 
hali ni tete. ee mungu washa taa yako tuwaone wadudu wakali nyoka,simba n.k tuwauwe mara moja mauti kama yale ya mwanao yesu kristo yaliyoyupatanisha na nafsi yako mungu.AMEN
 
Kwanini tusiandamane kuanzia sasa au kesho alfajr tukutane mnazi mmoja cc wa dar, dodoma viwanja vya bunge, arusha waende karume, mwanza nyamagana wasipojiuzulu tuchome bunge, ikulu na tbc! tuone kama jk wa pili mwz atarudi!
 
Mjepo, ni dhambi gani ya kikatiba ambayo serikali ya ccm haijawahi kufanya?.. Kitaeleweka tu. Wala hakuna kung'ang'ania kwa sababu ccm imeshajifunza kwa libya, tunisia, misri, na kwingineko kwingi ambako watawala waling'ang'ania utawala wakadhani nchi ni zao. Hatutaki sisi kufika kule. Ccm step down, kwa amani watanzania wanataka kujenga taifa lao lisilo la kifisadi kama ambavyo sasa ccm imeliweka. No More No Less!.

Nenda ukasome tena katiba ili ujue ni mambo gani ambayo yakifanyika ndiyo kura ya kutokuwa na imani na rais inapigwa lakini vinginevyo unajipotosha mwenyewe.
 
Sishangai gazeti la JAMHURI kuandika kuwa Pinda atajizuru au kushabikia sakata la IPTL sababu gazeti hili linamilikiwa na LOWASSA na BALILE NA MANYERERE wanalipwa mshahara na LOWASSA.
 
kura ya kutokuwa na imani na rais tulipaswa kuipiga 2008 aliposema amewasamehe wezi wa EPA, sasa hivi haya yanayoendelea ni mwendelezo wa kosa letu la kutokuchukua maamuzi, hebu jiulize yeye kaenda kutibiwa Busha marekani wakati hosipitali hazina dawa wala vifaa bado tunasubiri nini kupiga kura ya kutokuwa na imani naye?

Kutibiwa nje ni kawaida kabisa kwa watu wa kada Fulani ,HATA MWALIMU ALIKUA ANATIBIWA NJE NA NDIYO MAANA HATA KIFO KILIMKUTA AKIWA NJE... Wizi wa Mali ya uma ulikuepo siku zote hata wakati wa Mlm . Tumpongeze Kikwete kwa KUONGOZA kwa uwazi na kuruhusu uhuru wa Habari , kitendo kinachowezesha raia wa kawaida kujua mambo ya ndani ya serekali yao.
Mbunge yeyote angeweza kupeleka MSWADA wa sheria Kali kwa wahusika wa wizi lkn tunaogopa kupitisha sheria Kali maana wizi na rushwa ni utamaduni wetu. Hadi hapo kutakapokua na mwafaka wa kitaifa kwamba tuazimie kwa pamoja kuacha WIZI NDIPO TUTATUNGA SHERIA NA KUZITEKELEZA DHIDI YA WEZI!
 
Mjepo, ni dhambi gani ya kikatiba ambayo serikali ya ccm haijawahi kufanya?.. Kitaeleweka tu. Wala hakuna kung'ang'ania kwa sababu ccm imeshajifunza kwa libya, tunisia, misri, na kwingineko kwingi ambako watawala waling'ang'ania utawala wakadhani nchi ni zao. Hatutaki sisi kufika kule. Ccm step down, kwa amani watanzania wanataka kujenga taifa lao lisilo la kifisadi kama ambavyo sasa ccm imeliweka. No More No Less!.

SUALA HAPA SIO CCM ILA NI MTU MWENYE UWEZO. Wenye uwezo wapo kama kule UKAWA JEMSI MBATIA ANA UWEZO , MTAMPA NAFASI?
CCM TUMPE MWIGULU NCHEMBA ATAPATA NAFASI?
 
Back
Top Bottom