Tukubaliafne kwamba suala la msingi hapa. Kinachoongoza nchi ni mtu peke yake, mfumo ama ni mtu katika mfumo?
Uwezo wa mtu unapimwa katika mambo mengi. Ni jambo lisilopingika kwamba hakuna mtu yeyote atakayeongoza nchi pasipo hila wala unafiki kutoka ccm. Kumbuka ccm na mafisadi wake kina kikwete ndio waliotufikisha hapa tulipo. Kikwete mara nyingine amekuwa akijaribu kuwa mwungwana, akishauriwa na Watanzania masuala ya kitaifa. Lakini mara zote ameshindwa kutekeleza hata moja na kuishia kuwa mnafiki mwongo mwongo, ndumila kuwili na msaliti wa wananchi kwa kuelemewa na nguvu ya mfumo wa chama chake. Huwezi kumtofautisha mtu na chama anachotoka kwa kuwa ndicho kinatakiwa kimpe support ya kutekeleza uongozi. Ccm leo haina hata chembe ya mwelekeo wa kusimamia suala lolote la watanzania. Hakuna mtu asiyelifahamu hili hata ndani ya ccm.
UKAWA, ndipo mahala pekee kuna watanzania wasiokuwa na mawaa. Hawajawahi kufisidi nchi japo walikuwa na uwezo huo kama wangetaka. Wamedhihirisha wazi ni kwa namna gani wanasimamia masuala ya kitaifa na si masuala yenye maslahi binafsi kwao.
UKaWA, wameonyesha kwa vitendo ni namna gani wanamaanisha na kuishi kwa wanayoyasema.
UKAWA, wameshaonyesha uwezo wao mkubwa wa kuona ni mambo gani yanakwamisha maendeleo ya nchi, ni nini mahitaji muhimu ya watanzania, nini kifanyike ili kuhakikisha nchi inarudi kwenye dira.
UKAWA, inawasomi wengi na zaidi ya yote inathamini elimu, utaalaam na inauwezo waktumia kila raslimali iliyopo nchini kwa maslahi ya taifa Kuanzia raslimali watu.
Unamesema Mwigulu nchemba, ameweza kufanya kitu gani? Kulalamika ama kufukuza kazi watoto BOT, kwa kuwa eti hawalipi mikopo benk walikokopa?? Kama mnaona ndiye pekee mliyenaye msimamisheni lakini Watanzania sisi bila kuajli vyama vya siasa, tunachagua UKaWA.
Bila UKAWA, Tanzania inakwenda kuwa historia.
WATANZANIA wakiwemo wanachama wa vyama vya upinzani, wasio na vyama kama mimi, na wana ccm wenye nia safi wanaoumizwa na ufirauni wa wahuni wanaoharibu nchi, tunaungana na TUNACHAGUA UKAWA. Tujenge mfumo mpya utakasimamia maslahi ya taifa. Hakuna nyongeza, hakuna mbadala wa UKAWA.
SUALA HAPA SIO CCM ILA NI MTU MWENYE UWEZO. Wenye uwezo wapo kama kule UKAWA JEMSI MBATIA ANA UWEZO , MTAMPA NAFASI?
CCM TUMPE MWIGULU NCHEMBA ATAPATA NAFASI?