Kisasi nini umuhimu wake

Kisasi nini umuhimu wake

Akimbute

Member
Joined
Apr 15, 2019
Posts
16
Reaction score
4
Naomba kueleweshwa kuhusu kisasi ni nin?
Faida za kisasi?
Umuhimu wa kisasi?
Lengo la kisasi?
Njia za visasi?
Hasara za kisasi?
GBWA-20190220230459.jpeg
 
kiuhalisia kabisa kisasi hakina faida zaidi ya kukufanya ufanye dhambi ambayo hata hukuwahi kuifanya,zaidi visasi huendeleza tu chuki kizazi mpaka kizazi

huwa tunaamini kulipa kisasi kwa mtu aliyekukosea hutuliza nafsi yetu,ila kiukweli na kutokana na ushuda wa wengi walilipa visasi wanakiri kuwa mara baada ya kulipa hakuna jambo walilolipata kutokana na kulipa huko zaidi ya kujikuta wametenda dhambi nzito labda hata ya kuua

kiufupi tu kisasi hakitimizi chochote kizuri,isipokuwa tu kihali ya kibinadamu si rahisi kumwona adui yako labda aliyekunyanyasa au kukuulia ndugu yako akifurahia maisha ilhali wewe una uchungu moyoni

hivyo kama unaweza kuwa na kifua na kuyaishi maandiko matakatifu ya Mwenyezi Mungu ni jambo la busara kutolipa kisasi na nature itafanya kazi yake kumlipa aliyekutendea ubaya mkubwa,ila kama ndo huwezi that's something else.
 
Shukran sanaa
Nimekuelewa
 
Hakuna umuimu wala faida ya kisasi zaidi ya kujiongezea dhambi tu mana maandiko yanasema tuwe watu wa kusamehe mara saba mara sabini yani maisha yetu yote mpaka tunaingia kaburini tuwe tunasamehe so hakuna faida ya kulipa kisasi
 
Nashukuru kusikia hvyo
 
Nafs imegoma kusamehe
Kila nikisamehe,,nafs inagoma
Na hat kunijia ndoton
okay sawa mkuu unaweza kusema ni nini alikutendea kama hutojali?kama hutoweza sawa mkuu,ila naomba kuuliza,kwa sababu umeshindwa kusamehe na mpaka ndotoni inakujia,unapanga kufanya nini? nini kinakupa haki ya kuamini kuwa huyo aliyekukosea hana haki ya kusamehewa na wewe?
 
Mfano
Mtu kakuharibia maisha,,kaharibu uhusiano na familia yako,,kaharibu urafik wa wenzio,,kwa kuwa yey ana mamlaka
How does it sound?
 
Kisasi ni cha Mungu Mwenyewe.
Kwa hiyo kisasi ni muhimu sana.
Mana ni kazi ya Mungu.
Mungu analipa mwenyewe hivyo ni wajibu wetu kumwomba Mungu alipe kisasi na asamehe pale anapombwa msamaha.

Dunia bila kisasi cha Mungu shetani ataonekana hadharani mana ana wanachama wengi sana.

Unajua hata Osama bin Laden au Carlos walilipa visasi sana lakini kuna mambo Mengi yamebadilika kwa sababu ya visasi vyao.
Mfano Mtizamo wa wazungu dhidi ya waarabu ulibadilika.
Mtizamo wa mabeberu dhidi ya wengine ulibadilika kutokana na Visasi za Carlos.
Lakini pia Visasi vya mataifa makubwa dhidi ya madikteta vimewasababisha watawala kuheshimu haki za wanadamu wenzao.
Vinginevyo Leo hii watawala wangekua wanakula nyama za watu na kupika mishkaki ya nyama za binadamu huku wakijipongeza kwa kuvuta cigar .
Tunaposema kisasi ni cha Mungu sio kwamba binadamu hana wakati wa kufanya kisasi Bali ni kuwa Mungu ndiye anayejua wakati sahihi wa kufanya kisasi.

Mfano kwa miaka mingi Taifa la Israel lilionewa sana lakini Mungu akaweka mstaifa Makubwa ya kulipigania na kuwapa uwezo wa kulipa kisasi.

Kuna wakati kusamehe kunakua ni njia bora sana hasa wakati wake ukiwa haujafika.

Mfano ni rahisi Marekani kurusha Kombora Komoro na kamoro wakasamehe lakini ni vigumu sana kwa Komoro kurusha kombora Marekani na Marekani wakasamehe. Kwa vyovyote Marekani watalipa kisasi mana ni wakati wao na kufanya hivyo na nguvu ya kulipa kisasi wanayo.

Mfano Yesu aliwaambia wanafunzi wake mtu akikupiga shavu la kulia mgeuzie la kushoto ; alikua na maana kubwa sana.
Unafikiri wafuasi wake wakati huo wangeweza kupambana na Mafarisayo ,masadukayo ,mayahudi na Majeshi ya Kirumi yaliyokuwa na nguvu kubwa za kila namna. Bila shaka injili ingeishia pale pale mana wangeonekana kama wahalifu na wasaliti na kukosa uungwaji mkono.
Imani yao ilikua ndogo na nguvu yao pia kidola na kimapambano ilikua ndogo sana.
Nabii Eliya na Mussa walikua na nguvu kubwa ya kiroho na kumapambano ya miujiza mikubwa hivyo hawakusita kulipa kisasi na kumuadhibu yeyote aliyejaribu kufanya dhulma.

Nchi yenye misingi mizuri ya kusimamia na kutenda haki kwa usawa inaweza kuzuia sana mawazo ya watu kulipizana visasi mana Serikali inasimama badala ya Mungu kuwaadhibu wakosaji .

Mfano Chama A kinapita na kuapiga wanachama wa chama B kwa sababu tu ya iburi chao na kuwa wanauwezo wa kuamuru majeshi yawe upande wao.
Hali kama hiyo inaishaje kama Serikali haisimami kama Mungu na kulipa kisasi na kuwakamata wahalifu wote na kuwatupa gerezani.
Mawazo ya visasi yanapotea hapo.

Mungu anaingilia na kulipa kisasi endapo hakuna mtu wa kujitokeza kumsaidia aliyedhulumiwa.
Mfano unapomdhulumu yatima na pakawa hakuna mtu wa kumsaidiwa wala serikali ,hakika Mungu anamlipia kisasi.
 
Nimekupata mkuu
 
Hata kwa mwanadamu pia kimeruhusiwa. 2Thes.1:6 " Kwakuwa ni haki mbele za Mungu KUWALIPA MATESO wale wawatesao ninyi"
Asante
Kweny quran kisas kimeruhusiwa
Ila kusamehe ni bora zaidi
I need a break
Nifikirie tena
 
Ila usije ingia kichwa kichwa bila kuambiwa na Mungu soma Esta na mjomba wake walipiga goti
siku 3 bila kula wala kunywa si mnyama wala mtoto angalia Mungu alichokifanya
Hata kwa mwanadamu pia kimeruhusiwa. 2Thes.1:6 " Kwakuwa ni haki mbele za Mungu KUWALIPA MATESO wale wawatesao ninyi"
Asante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom