Kisasi nini umuhimu wake

Kisasi nini umuhimu wake

Mfano
Mtu kakuharibia maisha,,kaharibu uhusiano na familia yako,,kaharibu urafik wa wenzio,,kwa kuwa yey ana mamlaka
How does it sound?
kwa mkuu kiukweli kabisa na kibinadamu inauma sana mkuu,especially kama yeye kwake maisha yanaendelea vizuri tu na ana raha zote

Ila mkuu weka hili akilini mwako Mungu alipouumba ulimwengu aliweka na kanuni za maisha vile vile za namna gani mwanadamu aishi na mwanadamu mwenzie,lakini pia kupitia maadniko yake matakatifu katoa mwongoz wa namna binadamu anastahili kuishi na wanadamu wenzie,hivyo basi yeyote atakayevunja kanuni hizo hawezi kukosa matokeo yatokanayo na matendo yake au uvunjifu wa kanuni hizo.

lakini pia ujue mwenye haki ya kuamua ikiwa tumetenda vizuri au vibaya ni Mungu ambaye ndiye hututuwekea viwango viizuri na vibaya,huenda ukaona una haki ya kuhisi hivyo au kuhisi kuwa yule mtu aliyekutendea hivyo alikuonea tu,lakini kumbe huenda huyo mtu aliwahi kutendewa vibaya pia labda na mtu wa familia yako na hivyo akaona njia hiyo kuwa sahihi kutuliza nafsi yake,mwisho wa yote jitahidi kumwachia Mungu yote yaliyokukuta kwa maana ni Mungu pekee ndiye anayejua ukweli wote wa mambo sisi wanadamu tunaona kwa nje tu

Mwisho jitahidi kujiborresha wewe na utu wako kwa kuzidi kumkaribia Mungu anayetoa faraja na tulizo la kweli,akuepushie kisasi ulichonacho,lakini pia badala ya kutumia muda mwingi kumfikira mkosaji wako tumia muda huo kuboresha pale pote ambapo mkosaji wako ameharibu.
 
Hata kwa mwanadamu pia kimeruhusiwa. 2Thes.1:6 " Kwakuwa ni haki mbele za Mungu KUWALIPA MATESO wale wawatesao ninyi"
Asante
Ukitaka kuelewa hicho kifungu soma sura yote, Agano jipya halina visasi zaidi ya kuambia geuza na shavu lako la pili,
ila kabla hajaja mwana wa Mungu walikuwa wanaruhusiwa ila mpaka wapewe maagizo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kisasi ni cha Mungu Mwenyewe.
Kwa hiyo kisasi ni muhimu sana.
Mana ni kazi ya Mungu.
Mungu analipa mwenyewe hivyo ni wajibu wetu kumwomba Mungu alipe kisasi na asamehe pale anapombwa msamaha.

Dunia bila kisasi cha Mungu shetani ataonekana hadharani mana ana wanachama wengi sana.

Unajua hata Osama bin Laden au Carlos walilipa visasi sana lakini kuna mambo Mengi yamebadilika kwa sababu ya visasi vyao.
Mfano Mtizamo wa wazungu dhidi ya waarabu ulibadilika.
Mtizamo wa mabeberu dhidi ya wengine ulibadilika kutokana na Visasi za Carlos.
Lakini pia Visasi vya mataifa makubwa dhidi ya madikteta vimewasababisha watawala kuheshimu haki za wanadamu wenzao.
Vinginevyo Leo hii watawala wangekua wanakula nyama za watu na kupika mishkaki ya nyama za binadamu huku wakijipongeza kwa kuvuta cigar .
Tunaposema kisasi ni cha Mungu sio kwamba binadamu hana wakati wa kufanya kisasi Bali ni kuwa Mungu ndiye anayejua wakati sahihi wa kufanya kisasi.

Mfano kwa miaka mingi Taifa la Israel lilionewa sana lakini Mungu akaweka mstaifa Makubwa ya kulipigania na kuwapa uwezo wa kulipa kisasi.

Kuna wakati kusamehe kunakua ni njia bora sana hasa wakati wake ukiwa haujafika.

Mfano ni rahisi Marekani kurusha Kombora Komoro na kamoro wakasamehe lakini ni vigumu sana kwa Komoro kurusha kombora Marekani na Marekani wakasamehe. Kwa vyovyote Marekani watalipa kisasi mana ni wakati wao na kufanya hivyo na nguvu ya kulipa kisasi wanayo.

Mfano Yesu aliwaambia wanafunzi wake mtu akikupiga shavu la kulia mgeuzie la kushoto ; alikua na maana kubwa sana.
Unafikiri wafuasi wake wakati huo wangeweza kupambana na Mafarisayo ,masadukayo ,mayahudi na Majeshi ya Kirumi yaliyokuwa na nguvu kubwa za kila namna. Bila shaka injili ingeishia pale pale mana wangeonekana kama wahalifu na wasaliti na kukosa uungwaji mkono.
Imani yao ilikua ndogo na nguvu yao pia kidola na kimapambano ilikua ndogo sana.
Nabii Eliya na Mussa walikua na nguvu kubwa ya kiroho na kumapambano ya miujiza mikubwa hivyo hawakusita kulipa kisasi na kumuadhibu yeyote aliyejaribu kufanya dhulma.


Nchi yenye misingi mizuri ya kusimamia na kutenda haki kwa usawa inaweza kuzuia sana mawazo ya watu kulipizana visasi mana Serikali inasimama badala ya Mungu kuwaadhibu wakosaji .

Mfano Chama A kinapita na kuapiga wanachama wa chama B kwa sababu tu ya iburi chao na kuwa wanauwezo wa kuamuru majeshi yawe upande wao.
Hali kama hiyo inaishaje kama Serikali haisimami kama Mungu na kulipa kisasi na kuwakamata wahalifu wote na kuwatupa gerezani.
Mawazo ya visasi yanapotea hapo.

Mungu anaingilia na kulipa kisasi endapo hakuna mtu wa kujitokeza kumsaidia aliyedhulumiwa.
Mfano unapomdhulumu yatima na pakawa hakuna mtu wa kumsaidiwa wala serikali ,hakika Mungu anamlipia kisasi.
Nimeamua kusamehe
Thanks wana jf
 
Back
Top Bottom