safuher
JF-Expert Member
- Feb 11, 2019
- 11,169
- 15,851
ohoo..Ewaaaaah,.kisamvu kitamm jomonii hasa kikilala
ohoo..Ewaaaaah,.kisamvu kitamm jomonii hasa kikilala
Hata mm kisamvu hakinichoshi nakipenda saaana,.ni kitam jamanii ukipata na samaki wa kukaanga au firigisi,.dooh😋😋
Uwwii vyote vyoteee😋😋Cha nazi au cha karanga? 😋😋😋
Leo nakipika na jodari wa nazi na wali😋😋na hiki kimvua karibu sanaaa🤓😋😋😋😋
OkMamboo wapenzi wa mahanjam,mambo matam matam ya jikoni,mambo ya chakula kizuuuri chenye ladha isiyo chosha.....Asalam Alaykhum,.
Leo nataka tujifunze mboga hii jinsi ya kuitengeneza na kuipika,.kisamvu ni moja ya mboga za majani na ni maarufu sana kwa nchi zetu za Africa na hata baadhi ya nchi za ulaya hutumia pia kama mboga ya majani,.YES kisamvu kina utam wake waliowahi kula mboga hii wanaelewa hasa kikiwa kimepikika kwelikweli kikapikika,.aisee ni kitam sanaaa
Basi tupike mboga yetu hii ya kisamvu; kwanza utachuma kisamvu chako kitekekiteke (mimi nimekipanda kwangu)utakichambua kwa kutenganisha jani la kisamvu na kikonyo,utaweka kwenye kinu chako kisafi, kisha utamenya kitunguu saumu na utakiweka kwenye kinu pamoja na kisamvu (wengine huweka na tangawizi)japo si lazima sana,.ukitwangia kitunguu saumu kinafanya kisamvu chako kinukie vizuri.
Twanga kisamvu na kitunguu saumu mpaka kilainike sana,tumia kinu kikubwa na kipana kwa sababu kisamvu kikianza kulainika huruka-ruka na kumwagika....kikisha lainika kitoe kwenye kinu kiweke kwenye sufuria pana,weka maji kwenye kinu kisuuze vizuri hayo maji yaweke kwenye sufuria lenye kisamvu chako tayari kwa kuweka jikoni kichemke,.wakati huu unaweza kuchanganya na kunde mbichi vikachemka pamoja,..
Kisamvu chako kikishaiva pamoja na kunde (kama utatumia,sio lazima sana kuweka kunde japo huvutia zaidi)epua hakikisha kimeiva na hakina majimaji mengi(kiwe kimekauka kidogo)weka sufuria nyingine kavu jikoni,ikipata moto weka mafuta ya kupikia kiasi na wakati huu unakuwa umekuna nazi yako iliyokomaa vizuri na kuichuja matui mawili jepesi na zito (tui bubu)au utatumia tui la karanga..
Mafuta yakipata moto weka kitunguu maji kikaange mpaka kiwe cha rangi ya brown,weka kisamvu chako kikaange pamoja na kitunguu mpaka viingiliane,halafu weka tui lako jepesi acha vichemke kwa dk 5-6 ukiwa umefunika,baada ya hapo punguza moto kidogo halafu weka karoti iliyokatwa katwa vipande vya wastani pamoja na chumvi na pilipili mbuzi kama utapenda,geuza kwa pamoja halafu weka tui zito na uache kichemke taratibu kwa dk 4-5...
Epua kisamvu chako na kitakuwa tayari kwa kuliwa,mboga hii unaweza kula kwa ugali,wali,ndizi,makande na hata chapati ukipenda,.
Mpaka wakati mwingine babaaiina weekend njema!!!
Si useme tu ulichotegemea sicho ulichokikuta
Nimechekaa sana daah🤣🤣umemuwezajeeSi useme tu ulichotegemea sicho ulichokikuta
Hahahah. Furaha yako ni wengine kuwezwa?Nimechekaa sana daahumemuwezajee
Wala...ila mawazo yako yanaonekana yalikuwa hasi ndio maana pengine ulikuja fasta kwenye kisamvu...am sorry😊Hahahah. Furaha yako ni wengine kuwezwa?
Mbona nilisoma kisha nikasema OK. Au OK nayo mawazo hasi?. Hahahah. Au unaamanisha mawazo hasi ni nini?. Take it easy don't panic wala siyo kasi?Wala...ila mawazo yako yanaonekana yalikuwa hasi ndio maana pengine ulikuja fasta kwenye kisamvu...am sorry
SHETSNI KANITAWALA SANA YAAANI NILIENDA MBALI SANA NANKISAMVU CHANGU DAAA HERI KISAMVU CHA KWELIMnya mnya mnya but niwie radhi mno... Heading ilinichanganya kidogo nikadhani ni kisamvu kile cha kopo... Kisamvu cha pilau
Jr
Sasa nani kapanic😃...potezea basi kama mtu kweli..Mbona nilisoma kisha nikasema OK. Au OK nayo mawazo hasi?. Hahahah. Au unaamanisha mawazo hasi ni nini?. Take it easy don't panic wala siyo kasi?
Hahahahah. Nisipopotezea nitakuwa siyo mtu kweli?Sasa nani kapanic...potezea basi kama mtu kweli..
Ndioo...utakuwa RobocopHahahahah. Nisipopotezea nitakuwa siyo mtu kweli?
Hahhaha. PoaNdioo...utakuwa Robocop
najua mawazo yake huyuNimechekaa sana daahumemuwezajee
Ya kisheitwain ndio maana kaishia kusema ok lol😆najua mawazo yake huyu