Kisamvu...

Mother Confessor

Mother Confessor

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2016
Messages
12,313
Likes
25,793
Points
280
Mother Confessor

Mother Confessor

JF-Expert Member
Joined Jan 7, 2016
12,313 25,793 280
Mamboo wapenzi wa mahanjam,mambo matam matam ya jikoni,mambo ya chakula kizuuuri chenye ladha isiyo chosha.....Asalam Alaykhum,.

Leo nataka tujifunze mboga hii jinsi ya kuitengeneza na kuipika,.kisamvu ni moja ya mboga za majani na ni maarufu sana kwa nchi zetu za Africa na hata baadhi ya nchi za ulaya hutumia pia kama mboga ya majani,.YES kisamvu kina utam wake waliowahi kula mboga hii wanaelewa hasa kikiwa kimepikika kwelikweli kikapikika,.aisee ni kitam sanaaa๐Ÿ˜‹๐Ÿ˜‹

Basi tupike mboga yetu hii ya kisamvu; kwanza utachuma kisamvu chako kitekekiteke (mimi nimekipanda kwangu)utakichambua kwa kutenganisha jani la kisamvu na kikonyo,utaweka kwenye kinu chako kisafi, kisha utamenya kitunguu saumu na utakiweka kwenye kinu pamoja na kisamvu (wengine huweka na tangawizi)japo si lazima sana,.ukitwangia kitunguu saumu kinafanya kisamvu chako kinukie vizuri.

Twanga kisamvu na kitunguu saumu mpaka kilainike sana,tumia kinu kikubwa na kipana kwa sababu kisamvu kikianza kulainika huruka-ruka na kumwagika....kikisha lainika kitoe kwenye kinu kiweke kwenye sufuria pana,weka maji kwenye kinu kisuuze vizuri hayo maji yaweke kwenye sufuria lenye kisamvu chako tayari kwa kuweka jikoni kichemke,.wakati huu unaweza kuchanganya na kunde mbichi vikachemka pamoja,..

Kisamvu chako kikishaiva pamoja na kunde (kama utatumia,sio lazima sana kuweka kunde japo huvutia zaidi)epua hakikisha kimeiva na hakina majimaji mengi(kiwe kimekauka kidogo)weka sufuria nyingine kavu jikoni,ikipata moto weka mafuta ya kupikia kiasi na wakati huu unakuwa umekuna nazi yako iliyokomaa vizuri na kuichuja matui mawili jepesi na zito (tui bubu)au utatumia tui la karanga..

Mafuta yakipata moto weka kitunguu maji kikaange mpaka kiwe cha rangi ya brown,weka kisamvu chako kikaange pamoja na kitunguu mpaka viingiliane,halafu weka tui lako jepesi acha vichemke kwa dk 5-6 ukiwa umefunika,baada ya hapo punguza moto kidogo halafu weka karoti iliyokatwa katwa vipande vya wastani pamoja na chumvi na pilipili mbuzi kama utapenda,geuza kwa pamoja halafu weka tui zito na uache kichemke taratibu kwa dk 4-5...

Epua kisamvu chako na kitakuwa tayari kwa kuliwa,mboga hii unaweza kula kwa ugali,wali,ndizi,makande na hata chapati ukipenda,.

Mpaka wakati mwingine babaaii๐Ÿ˜‰๐Ÿ˜‰na weekend njema!!!
 
Attachments:

Mother Confessor

Mother Confessor

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2016
Messages
12,313
Likes
25,793
Points
280
Mother Confessor

Mother Confessor

JF-Expert Member
Joined Jan 7, 2016
12,313 25,793 280
Mboga niipendayo miaka yote. Kisamvu ugali, kisamvu wali halafu pembeni kuwe na samaki wa kukaanga.
Hata mm kisamvu hakinichoshi nakipenda saaana,.ni kitam jamanii ukipata na samaki wa kukaanga au firigisi,.dooh๐Ÿ˜‹๐Ÿ˜‹
 
Vladimirovich Putin

Vladimirovich Putin

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2017
Messages
14,677
Likes
19,466
Points
280
Vladimirovich Putin

Vladimirovich Putin

JF-Expert Member
Joined Feb 6, 2017
14,677 19,466 280
Hahaha Vladimir una wazimu wewe,.utakula kisamvu tuu mimi kunikula ni ndoto mfyuu
Mbona unakua mchoyo jamaaan, maana kwa haya maelezo ya kisanvu, unaonekana ni mwanamke msafi, unamapaja paja, nyonyo zilizojaa ,sura taaaamu...

Naanzaje kutopenda nikukule????khaaaaa embu acha uchoyooo, dunia enyewe ndo IPO mwishon, huo uchoyo wann ????
 
Mother Confessor

Mother Confessor

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2016
Messages
12,313
Likes
25,793
Points
280
Mother Confessor

Mother Confessor

JF-Expert Member
Joined Jan 7, 2016
12,313 25,793 280
Mbona unakua mchoyo jamaaan, maana kwa haya maelezo ya kisanvu, unaonekana ni mwanamke msafi, unamapaja paja, nyonyo zilizojaa ,sura taaaamu...

Naanzaje kutopenda nikukule????khaaaaa embu acha uchoyooo, dunia enyewe ndo IPO mwishon, huo uchoyo wann ????
Nyau wewe wa kijivu,.una nini lakini leo...umefumaniwa eee ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
 
Hornet

Hornet

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2013
Messages
15,707
Likes
14,098
Points
280
Hornet

Hornet

JF-Expert Member
Joined Apr 29, 2013
15,707 14,098 280
Safi
Mie huwa nakichemsha
Kikianza kuwiva nakatia kitunguu maji

Naacha vinachemkia
Naweka karoti (box shape)

Naacha kidogo
Naweka nazi ya kwanza

Kisha nazi ya pili

Nachemsha mpaka kikauke...

Nimekimiss Leo nikipike lol
 
Mother Confessor

Mother Confessor

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2016
Messages
12,313
Likes
25,793
Points
280
Mother Confessor

Mother Confessor

JF-Expert Member
Joined Jan 7, 2016
12,313 25,793 280
Safi
Mie huwa nakichemsha
Kikianza kuwiva nakatia kitunguu maji

Naacha vinachemkia
Naweka karoti (box shape)

Naacha kidogo
Naweka nazi ya kwanza

Kisha nazi ya pili

Nachemsha mpaka kikauke...

Nimekimiss Leo nikipike lol
Unaweza kukichemsha leo ukakipika kesho kwa utuvu..kisamvu kikilala nacho kinautam wake eti,..hahah
 
Mother Confessor

Mother Confessor

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2016
Messages
12,313
Likes
25,793
Points
280
Mother Confessor

Mother Confessor

JF-Expert Member
Joined Jan 7, 2016
12,313 25,793 280
"Baby chuma Kisamvu!"
"Baby chuma Kisamvu!"
"Baby chuma Kisamvu!"
"Haya... Haya.... Waonyesheeee!

"Baby chuma Kisamvu!"
"Baby chuma Kisamvu!"

Q Chilla!

Sent using Jamii Forums mobile app
Naww unapenda kisamvu๐Ÿ™ˆ๐Ÿ™ˆ๐Ÿ™ˆ
 
Triple G

Triple G

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2011
Messages
1,094
Likes
423
Points
180
Triple G

Triple G

JF-Expert Member
Joined Aug 12, 2011
1,094 423 180
Hata mm kisamvu hakinichoshi nakipenda saaana,.ni kitam jamanii ukipata na samaki wa kukaanga au firigisi,.dooh๐Ÿ˜‹๐Ÿ˜‹
hahahhaaha...kisamvu kiko poa sana...alafu pia kuna kitu kinaitwa mlenda na samaki au nyama ya kukaanga na ugali hapo ndo huwa naona nimekula na nimeshiba...daaah
 
Mother Confessor

Mother Confessor

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2016
Messages
12,313
Likes
25,793
Points
280
Mother Confessor

Mother Confessor

JF-Expert Member
Joined Jan 7, 2016
12,313 25,793 280
hahahhaaha...kisamvu kiko poa sana...alafu pia upate na mlenda na samaki au nyama ya kukaanga...daaah
Jamanii jamaniii mate yananchuruzika,na wengine hapa tunavyopenda kula vitu vitamm basii nishawaza hadi kesho itakuwaje hahah
 
Mshana Jr

Mshana Jr

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Messages
104,629
Likes
125,251
Points
280
Mshana Jr

Mshana Jr

JF-Expert Member
Joined Aug 19, 2012
104,629 125,251 280
Mamboo wapenzi wa mahanjam,mambo matam matam ya jikoni,mambo ya chakula kizuuuri chenye ladha isiyo chosha.....Asalam Alaykhum,.

Leo nataka tujifunze mboga hii jinsi ya kuitengeneza na kuipika,.kisamvu ni moja ya mboga za majani na ni maarufu sana kwa nchi zetu za Africa na hata baadhi ya nchi za ulaya hutumia pia kama mboga ya majani,.YES kisamvu kina utam wake waliowahi kula mboga hii wanaelewa hasa kikiwa kimepikika kwelikweli kikapikika,.aisee ni kitam sanaaa

Basi tupike mboga yetu hii ya kisamvu; kwanza utachuma kisamvu chako kitekekiteke (mimi nimekipanda kwangu)utakichambua kwa kutenganisha jani la kisamvu na kikonyo,utaweka kwenye kinu chako kisafi, kisha utamenya kitunguu saumu na utakiweka kwenye kinu pamoja na kisamvu (wengine huweka na tangawizi)japo si lazima sana,.ukitwangia kitunguu saumu kinafanya kisamvu chako kinukie vizuri.

Twanga kisamvu na kitunguu saumu mpaka kilainike sana,tumia kinu kikubwa na kipana kwa sababu kisamvu kikianza kulainika huruka-ruka na kumwagika....kikisha lainika kitoe kwenye kinu kiweke kwenye sufuria pana,weka maji kwenye kinu kisuuze vizuri hayo maji yaweke kwenye sufuria lenye kisamvu chako tayari kwa kuweka jikoni kichemke,.wakati huu unaweza kuchanganya na kunde mbichi vikachemka pamoja,..

Kisamvu chako kikishaiva pamoja na kunde (kama utatumia,sio lazima sana kuweka kunde japo huvutia zaidi)epua hakikisha kimeiva na hakina majimaji mengi(kiwe kimekauka kidogo)weka sufuria nyingine kavu jikoni,ikipata moto weka mafuta ya kupikia kiasi na wakati huu unakuwa umekuna nazi yako iliyokomaa vizuri na kuichuja matui mawili jepesi na zito (tui bubu)au utatumia tui la karanga..

Mafuta yakipata moto weka kitunguu maji kikaange mpaka kiwe cha rangi ya brown,weka kisamvu chako kikaange pamoja na kitunguu mpaka viingiliane,halafu weka tui lako jepesi acha vichemke kwa dk 5-6 ukiwa umefunika,baada ya hapo punguza moto kidogo halafu weka karoti iliyokatwa katwa vipande vya wastani pamoja na chumvi na pilipili mbuzi kama utapenda,geuza kwa pamoja halafu weka tui zito na uache kichemke taratibu kwa dk 4-5...

Epua kisamvu chako na kitakuwa tayari kwa kuliwa,mboga hii unaweza kula kwa ugali,wali,ndizi,makande na hata chapati ukipenda,.

Mpaka wakati mwingine babaaiina weekend njema!!!
Mnya mnya mnya but niwie radhi mno... Heading ilinichanganya kidogo nikadhani ni kisamvu kile cha kopo... Kisamvu cha pilau

Jr
 
Forum statistics

Threads 1,251,651
Members 481,811
Posts 29,778,891