Kisa kizuri chenye mafunzo

Kisa kizuri chenye mafunzo

king majah

Member
Joined
Jan 10, 2013
Posts
61
Reaction score
50
SIMULIZI YENYE MAZINGATIO
Aboubakar ni mwajiriwa katika kampuni moja ya usambazaji wa nyama.
Siku moja jioni baada ya kumaliza kazi zake za siku aliamua aingie katika chumba baridi cha kuhifadhia nyama kukagua kitu na kwa bahati mbaya mlango ukajifunga huku akiwa ndani.
Alijaribu kugonga mlango na hata kupiga kelele za kuomba msaada kwa muda mrefu lakini jitihada zake hazikufanya lolote kwani kutokana na barafu zilizomo ndani na jinsi kulivyozibwa kuzuia ubaridi kutotoka nje haikuwa rahisi kilio chake cha kuomba msaada kusikika.
Haikuwa rahisi kusikika sauti yake kutoka katika chumba hicho na kila mfanyakazi alikuwa ameshaondoka.
Masaa manne baadae Aboubakar alikuwa kama yuko katika bonde la umauti akisubiri kifo chake huku akimwomba Mungu wake kwa sala yenye unyenyekevu mkubwa.
Akiwa katikati ya sala yake mara akashtushwa kuona mlango wa chumba hicho ukifunguliwa na mlinzi wa kampuni hiyo akiingia na kumwokoa.
Wakiwa katika chumba kingine huku Aboubakar akiwa kapewa msaada wa moto ili kuupasha mwili wake joto na kahawa ikiwa Mezani, Aboubakar akaamua amuulize yule mlinzi ni kitu gani kilimfanya akifungue chumba kile.
Mlinzi akamjibu, " nimefanya kazi katika kampuni hii kwa miaka 21 na katika kipindi hiki mamia ya wafanyakazi wamekuwa wakiniona kama mtu nisiye na maana na ni wachache sana wanaonisalimia kwa kuniambia HABARI ZA ASUBUHI wakiwa wanaingia kazini na KAZI NJEMA wanapoondoka jioni kurudi makwao.
Leo asuhuhi ulipoingia ulinisalimia kwa furaha kama kawaida yako na jioni wakati watu wanaondoka kurudi kwao nikaisubiri sauti yako kunifariji tena kwa kusema KAZI NJEMA kama siku nyingine lakini sikuisikia ndio nikaamua kuanza kupitia kila chumba kuona nini kimekupata na ndio nikakuona kwenye chumba kile ukiwa umefungiwa"
Aboubakar kwa furaha yenye maumivu alibubujikwa na machozi katika macho yake.
Funzo
Mthamini aliyejuu na aliye chini yako, kwani yajayo huyajui, bali unayajua yalopita tuu.
Tuishi maisha ya kupendana na kuwajali wale watuzungukao kwani huwezi jua ni namna gani kwa kufanya hivyo tunawapa furaha katika maisha yao na kuwafariji.
UPENDO NI NGUZO MUHIMU KTK MAISHA.
PIGA 07562628899 ILI UPATE BLOG NZURI YENYE MVUTO KWA BEI NAFUUU
 
Back
Top Bottom