Wadau,
Nimepata data muda si mrefu.
Inasikitisha ila habari ndiyo hiyo
Rais mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi leo jumanne pale katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam amelambwa kofi na Muumini kwa kile kinachoelezwa kama kutetea matumizi ya KONDOMU kwa waumini.
Alikuwa akizungumza katika baraza la Maulid lililofanyika jioni hii.
=====
UPDATES:
Kijana aliyemzaba kibao Rais Mwinyi afunguka
Machi 12, 2009
Wakati taasisi mbalimbali za kidini, wananchi wa kawaida na Kamati ya Bunge zikilaani kitendo cha Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi, kupigwa kofi shavuni, muumini aliyefanya kitendo hicho, Ibrahim Said, ameeleza kuwa alifanya hivyo kupinga matumizi ya kondomu kwa waumini wa dini ya Kiislamu kwa madai kwamba, yanachochea vitendo vya zinaa.
Pia alisema alifanya kitendo hicho kupinga kuwapo kwa umoja kati ya Waislamu na Wakristo wakati wa kusherehekea sikukuu zao (Maulid, Idd, Krismas na Pasaka), uliozungumzwa na Mwinyi katika hotuba zake alizozitoa wakati wa mkesha Jumatatu usiku na kwenye Baraza la Maulid, jijini Dar es Salaam juzi.
Alisema hakuwa na nia ya kumdhuru Mwinyi na wala hamchukii, bali alikuwa na lengo la kufanya kituko chochote ili ujumbe wake uwafikie watu wengi.
Alitoa maelezo hayo alipohojiwa na polisi saa chache baada ya kufanya kitendo hicho wakati Mwinyi alipokuwa akihutubia Baraza la Maulid, katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam juzi jioni.

Last edited by a moderator: