Kisa cha MwanaHALISI kufungiwa ni Habari ya "Nani anastahili kuombewa kati ya Lissu au Magufuli"

Huwezi shindana na SERIKALI yoyote duniani ukafanikiwa,mbaya zaidi serikali ya Tanzania,kilichomponza Lissu ni kutafuta sifa na kuwafurahisha baadhi ya watu,ndo hicho hicho kilichowaponza MWANAHALISI tofauti ni kuwa mwanahalisi wali target pia mauzo makubwa,mwisho wa siku nani anaumia???
Rubbish
 
Bora kufa kuliko kuwa mnafki tena ndani ya Taifa lako...

Kulamba miguu viongozi kinafki
Kuamini nyuesi ni nyeupe ili kufurahisha viongozi ni unafki alioukataa Zitto ila wanaCcm wanautumia Kama mtaji kujikomba kwa wenye mamlaka.

Stupid minds of Ccm's
 
Hivi kwa akili zako unaweza ukaombea mpuuzi mmoja
uache Rais wa Taifa zima!!

Naona kwanza bado wana lipa kichwa hili gazeti
lilipaswa kufutiliwa kabisa kwenye uso wa Dunia
Kama unadhani kwa Mungu kuna raisi wa nchi na mpuuzi mmoja, na wewe unatakiwa kuombewa akili yako ifunguke.
 
Mungu nie
Leo Gazeti la Mwanahalisi limefungiwa kwa muda wa miaka miwili. HII NDIO MAKALA ILIYOPELEKEA MWANAHALISI KUFUNGIWA!

Tumwombee Magufuli au Tundu Lissu?

Na Ansbert Ngurumo

TANGU Tundu Lissu alipoanza kusisitiza mara kwa mara kwamba mambo mengi yanayofanywa na Rais John Magufuli ni ya kukurupuka, na yataleta hasara kubwa kwa taifa, rais na baadhi ya wafuasi wake wamekuwa wakisisitiza kuwa yeyote anayempinga rais ni msaliti.

Hata majuzi, katika moja ya hotuba zake mubashara za hivi majuzi, Rais Magufuli alisema:

“Nilipokuwa nikizungumza, ndugu zangu, kwamba hii ni vita ya uchumi, na vita ya uchumi ni mbaya kuliko vita ya kawaida.

“Vita ya kawaida, adui unamuona. Na saa nyingine msaliti anapowasiliti mkiwa katika vita ya kawaida, askari wanajua kazi yao huwa wanafanya nini.

“Huwezi kuwa msaliti halafu ukawa… uka-survive (ukanusurika, yaani ukaachwa uishi).”

Kwa Rais Magufuli na baadhi ya wapambe wake, Lissu ni msaliti, si mzalendo.

Katika mtandao mmoja wa kijamii, wiki kadhaa zilizopita, kuna mtu alithubutu kumshambulia Lissu kwa maneno hayo makali, akisema kuwa mbunge huyo wa Singida Mashariki si mzalendo.

Lissu hakusubiri mtu huyo ajibiwe na watu wengine. Alijibu mwenyewe akisema:

"Na mimi ni Mtanzania pia. Tofauti kati yangu mimi na wewe na Magufuli ni hii. Mimi nimepigania nchi yangu katika masuala haya (ya madini) tangu mwaka 1999.

Wakati huo, tulikuwa na mgodi mmoja tu wa dhahabu – Resolute Golden Pride Nzega. Bulyanhulu ilikuwa haijajengwa. Geita ndio kwanza walikuwa wanafukuza wanakijiji wa Mtakuja.

Nadhani nilikuwa wa kwanza katika nchi hii kupiga yowe kwamba tutaibiwa sana kwenye sekta ya madini.

Wewe sijui ulikuwa wapi wakati huo. Najua Magufuli alikuwa wapi. Alikuwa upande wa CCM na wawekezaji hawa.

Nimepigana na wawekezaji hawa mahakamani, kwenye medani ya kisiasa ndani na nje ya nchi hii kwa zaidi ya miaka 15. Nimetetea wananchi bila kudai malipo Bulyanhulu, Tarime, Nzega, Geita, na kadhalika.

Sijui wewe ulikuwa wapi, lakini najua Magufuli alikuwa upande wa nani – alikuwa upande wa CCM na wanyonyaji hawa.

Soma gazeti la Rai la tarehe 17 Julai, 2001, uone tulimwambia nini (Rais Benjamin) Mkapa siku alipokwenda kuzindua Mgodi wa Bulyanhulu.

Sijui ulikuwa wapi, lakini najua Magufuli alikuwa wapi. Alikuwa anatetea “tumbo lake” na matumbo ya wanyonyaji hawa.

Nilikamatwa na kushitakiwa kwa uchochezi kwa sababu ya (kutetea wananchi wa) Bulyanhulu. Hiyo ilikuwa December 2002. Nilikaa na kesi hiyo mahakamani Kisutu kwa miaka sita.

Sijui ulikuwa wapi, ila najua Magufuli alikuwa wapi. Alikuwa upande wa watesi wa wananchi na wanyonyaji wa rasilimali zetu.

Leo Magufuli anajifanya mzalendo, na anahoji uzalendo wa yeyote anayepingana naye. Ni muongo.

Anatafuta umaarufu wa kisiasa kwa wasiojua na wasiokumbuka. Ataupata kwa siku chache tu. Zingatia maneno yangu. Ataumbuka, na (nyie mnaomtetea) mtaumbuka.

Mimi ninampinga hadharani. Mimi si mnafiki, na sijahongwa. Ninampinga kwa sababu atatusababishia matatizo makubwa zaidi kuliko tuliyonayo sasa.

Huo mchanga (makinikia) atauachia upelekwe ambako umepelekwa kwa miaka 16 iliyopita. Kama sheria ndiyo hiyo na mikataba ndiyo hiyo, hana pa kwenda.

Tatizo ninaloliona ni kwamba wakati atakapokuwa anawarudishia mchanga wao, Tanzania itakuwa imekuwa hohe hahe kama Zimbabwe.

Na tutakuwa tumelipishwa fedha nyingi ya fidia na mahakama za usuluhishi za kimataifa kwa kuvunja mikataba na wawekezaji hawa.

Kama kuna anayefikiri uzalendo ni kufumbia macho masuala haya, basi huyo na amuunge mkono Magufuli kwenye upofu wake wa kujitakia.

Ripoti ya Prof. (Abdulkarim) Mruma haitamaliza hata nusu saa, iwapo itachunguzwa kwa kina.

Zaidi ya majina ya maprofesa walioiandaa, ripoti hii haina msingi wowote wa kuaminika. Ni kazi ya kisiasa iliyopakwa rangi ya usomi.

Kama umefuatilia taarifa za kitaalamu za Bulyanhulu hata kabla ya Barrick Gold kuingia mwaka 1999, utajua ninasema nini.

Sutton Resources, Outukumpu Oy, na hata STAMICO walishafanya utafiti mkubwa juu ya utajiri wa Bulyanhulu.

Taarifa zipo na zimekuwepo kwa hata mbumbumbu wa jiolojia ya madini kama mimi.

Hiki alichoambiwa Magufuli ni ujinga, hata kama ni wa kiprofesa. Hatuibiwi kwenye mchanga.

Huo ni ujinga unaoweza kukubaliwa tu na watu mbumbumbu. Tunaibiwa kwenye sheria. Kama hamuoni hilo, basi, Mungu na atusamehe!"

Kama serikali inasaini mikataba mibovu, na Lissu anapiga kelele kwamba mikataba hii ni mibovu na itaingiza taifa katika hasara, msaliti ni yeye anayesema au maofisa wa serikali waliosaini mikataba hiyo?

Msaliti ni yeye au rais anayetaka kumnyamazisha ili nchi isisikie sauti yake ya kinabii?

Kama viongozi wetu wamevunja mikataba; uamuzi wa viongozi wetu ukasababisha tushitakiwe, tukashindwa katika mahakama za usuluhishi; msaliti ni Lissu anayesema tumeshitakiwa na tumeshindwa?

Kama tunadaiwa na makampuni ya nje, yakakamata ndege yetu, Lissu akasema ndege yetu imekamatwa kwa sababu ya uamuzi mbovu wa viongozi wetu, na akasema watakaolipa fedha hizo si viongozi bali ni wananchi maskini; msaliti ni yeye au hao waliosababisha madhira hayo?

Kama rais anatoa amri zinazopoka uhuru wa wananchi kufikiri, kujieleza na kukusanyika – kinyume cha katiba – na Lissu anajitokeza kusema huu ni udikteta uchwara; inatosha kumuita msaliti?

Na katika mazingira ya “ugomvi” tunaoshuhudia mfululizo kati ya serikali na Lissu, na kwa kuzingatia matamko mabaya ya viongozi wakuu wa serikali dhidi yake; na sasa amepigwa risasi mchana kweupe, tutarajie nani awe mtuhumiwa wa kwanza dhidi ya Lissu?

Nimesikia kauli tata za viongozi wa jeshi la polisi na jeshi la wananchi. Wanazungumza kisiasa na kwa jeuri isiyotarajiwa, kubeza wananchi wanaohoji unyama aliofanyiwa Lissu.

Kwa hili la Lissu, serikali na wapambe wake watatunga propaganda za kutoa watu mstarini, lakini tayari naona Mungu amewakatalia.

Rais Magufuli, katika hotuba zake kadhaa, amekuwa anataka tumwombee. Sasa, kwa matukio haya, taifa limetambua nani anastahili kuombea – ni Tundu Lissu.
Mungu niepushe na shetani
 
Hivi kwa akili zako unaweza ukaombea mpuuzi mmoja
uache Rais wa Taifa zima!!
Naona kwanza bado wana lipa kichwa hili gazeti
lilipaswa kufutiliwa kabisa kwenye uso wa Dunia
Hapo ndo mnapoanzia kujidanganya,mnadhani wananchi wengi wapo nyuma ya CHADEMA na Kubenea,juzi jumapili kuna watu waliprint t-shirt kibao za PRAY 4LISSU,wakidhani wangeuza hata 100,waliishia kuuza tshirt 3 au 4 tu.Wafuasi na uma mnaousemea umebaki JF tu.Mtaani watu wapo bize na kupambana na hali zao,kujipatia kipato.
Mbona wenye mbwa walihangaika kuzuia hizo tisheti zisisambazwe?
 
Kilichoandikwa na gazeti hili ni lipi linalowapotosha Watanzania? Kipi ambacho haturuhusiwi kufahamu na kwa kuifahamu tunavunha sheria za Tanzania?
 
Leo Gazeti la Mwanahalisi limefungiwa kwa muda wa miaka miwili. HII NDIO MAKALA ILIYOPELEKEA MWANAHALISI KUFUNGIWA!

Tumwombee Magufuli au Tundu Lissu?

Na Ansbert Ngurumo

TANGU Tundu Lissu alipoanza kusisitiza mara kwa mara kwamba mambo mengi yanayofanywa na Rais John Magufuli ni ya kukurupuka, na yataleta hasara kubwa kwa taifa, rais na baadhi ya wafuasi wake wamekuwa wakisisitiza kuwa yeyote anayempinga rais ni msaliti.

Hata majuzi, katika moja ya hotuba zake mubashara za hivi majuzi, Rais Magufuli alisema:

“Nilipokuwa nikizungumza, ndugu zangu, kwamba hii ni vita ya uchumi, na vita ya uchumi ni mbaya kuliko vita ya kawaida.

“Vita ya kawaida, adui unamuona. Na saa nyingine msaliti anapowasiliti mkiwa katika vita ya kawaida, askari wanajua kazi yao huwa wanafanya nini.

“Huwezi kuwa msaliti halafu ukawa… uka-survive (ukanusurika, yaani ukaachwa uishi).”

Kwa Rais Magufuli na baadhi ya wapambe wake, Lissu ni msaliti, si mzalendo.

Katika mtandao mmoja wa kijamii, wiki kadhaa zilizopita, kuna mtu alithubutu kumshambulia Lissu kwa maneno hayo makali, akisema kuwa mbunge huyo wa Singida Mashariki si mzalendo.

Lissu hakusubiri mtu huyo ajibiwe na watu wengine. Alijibu mwenyewe akisema:

"Na mimi ni Mtanzania pia. Tofauti kati yangu mimi na wewe na Magufuli ni hii. Mimi nimepigania nchi yangu katika masuala haya (ya madini) tangu mwaka 1999.

Wakati huo, tulikuwa na mgodi mmoja tu wa dhahabu – Resolute Golden Pride Nzega. Bulyanhulu ilikuwa haijajengwa. Geita ndio kwanza walikuwa wanafukuza wanakijiji wa Mtakuja.

Nadhani nilikuwa wa kwanza katika nchi hii kupiga yowe kwamba tutaibiwa sana kwenye sekta ya madini.

Wewe sijui ulikuwa wapi wakati huo. Najua Magufuli alikuwa wapi. Alikuwa upande wa CCM na wawekezaji hawa.

Nimepigana na wawekezaji hawa mahakamani, kwenye medani ya kisiasa ndani na nje ya nchi hii kwa zaidi ya miaka 15. Nimetetea wananchi bila kudai malipo Bulyanhulu, Tarime, Nzega, Geita, na kadhalika.

Sijui wewe ulikuwa wapi, lakini najua Magufuli alikuwa upande wa nani – alikuwa upande wa CCM na wanyonyaji hawa.

Soma gazeti la Rai la tarehe 17 Julai, 2001, uone tulimwambia nini (Rais Benjamin) Mkapa siku alipokwenda kuzindua Mgodi wa Bulyanhulu.

Sijui ulikuwa wapi, lakini najua Magufuli alikuwa wapi. Alikuwa anatetea “tumbo lake” na matumbo ya wanyonyaji hawa.

Nilikamatwa na kushitakiwa kwa uchochezi kwa sababu ya (kutetea wananchi wa) Bulyanhulu. Hiyo ilikuwa December 2002. Nilikaa na kesi hiyo mahakamani Kisutu kwa miaka sita.

Sijui ulikuwa wapi, ila najua Magufuli alikuwa wapi. Alikuwa upande wa watesi wa wananchi na wanyonyaji wa rasilimali zetu.

Leo Magufuli anajifanya mzalendo, na anahoji uzalendo wa yeyote anayepingana naye. Ni muongo.

Anatafuta umaarufu wa kisiasa kwa wasiojua na wasiokumbuka. Ataupata kwa siku chache tu. Zingatia maneno yangu. Ataumbuka, na (nyie mnaomtetea) mtaumbuka.

Mimi ninampinga hadharani. Mimi si mnafiki, na sijahongwa. Ninampinga kwa sababu atatusababishia matatizo makubwa zaidi kuliko tuliyonayo sasa.

Huo mchanga (makinikia) atauachia upelekwe ambako umepelekwa kwa miaka 16 iliyopita. Kama sheria ndiyo hiyo na mikataba ndiyo hiyo, hana pa kwenda.

Tatizo ninaloliona ni kwamba wakati atakapokuwa anawarudishia mchanga wao, Tanzania itakuwa imekuwa hohe hahe kama Zimbabwe.

Na tutakuwa tumelipishwa fedha nyingi ya fidia na mahakama za usuluhishi za kimataifa kwa kuvunja mikataba na wawekezaji hawa.

Kama kuna anayefikiri uzalendo ni kufumbia macho masuala haya, basi huyo na amuunge mkono Magufuli kwenye upofu wake wa kujitakia.

Ripoti ya Prof. (Abdulkarim) Mruma haitamaliza hata nusu saa, iwapo itachunguzwa kwa kina.

Zaidi ya majina ya maprofesa walioiandaa, ripoti hii haina msingi wowote wa kuaminika. Ni kazi ya kisiasa iliyopakwa rangi ya usomi.

Kama umefuatilia taarifa za kitaalamu za Bulyanhulu hata kabla ya Barrick Gold kuingia mwaka 1999, utajua ninasema nini.

Sutton Resources, Outukumpu Oy, na hata STAMICO walishafanya utafiti mkubwa juu ya utajiri wa Bulyanhulu.

Taarifa zipo na zimekuwepo kwa hata mbumbumbu wa jiolojia ya madini kama mimi.

Hiki alichoambiwa Magufuli ni ujinga, hata kama ni wa kiprofesa. Hatuibiwi kwenye mchanga.

Huo ni ujinga unaoweza kukubaliwa tu na watu mbumbumbu. Tunaibiwa kwenye sheria. Kama hamuoni hilo, basi, Mungu na atusamehe!"

Kama serikali inasaini mikataba mibovu, na Lissu anapiga kelele kwamba mikataba hii ni mibovu na itaingiza taifa katika hasara, msaliti ni yeye anayesema au maofisa wa serikali waliosaini mikataba hiyo?

Msaliti ni yeye au rais anayetaka kumnyamazisha ili nchi isisikie sauti yake ya kinabii?

Kama viongozi wetu wamevunja mikataba; uamuzi wa viongozi wetu ukasababisha tushitakiwe, tukashindwa katika mahakama za usuluhishi; msaliti ni Lissu anayesema tumeshitakiwa na tumeshindwa?

Kama tunadaiwa na makampuni ya nje, yakakamata ndege yetu, Lissu akasema ndege yetu imekamatwa kwa sababu ya uamuzi mbovu wa viongozi wetu, na akasema watakaolipa fedha hizo si viongozi bali ni wananchi maskini; msaliti ni yeye au hao waliosababisha madhira hayo?

Kama rais anatoa amri zinazopoka uhuru wa wananchi kufikiri, kujieleza na kukusanyika – kinyume cha katiba – na Lissu anajitokeza kusema huu ni udikteta uchwara; inatosha kumuita msaliti?

Na katika mazingira ya “ugomvi” tunaoshuhudia mfululizo kati ya serikali na Lissu, na kwa kuzingatia matamko mabaya ya viongozi wakuu wa serikali dhidi yake; na sasa amepigwa risasi mchana kweupe, tutarajie nani awe mtuhumiwa wa kwanza dhidi ya Lissu?

Nimesikia kauli tata za viongozi wa jeshi la polisi na jeshi la wananchi. Wanazungumza kisiasa na kwa jeuri isiyotarajiwa, kubeza wananchi wanaohoji unyama aliofanyiwa Lissu.

Kwa hili la Lissu, serikali na wapambe wake watatunga propaganda za kutoa watu mstarini, lakini tayari naona Mungu amewakatalia.

Rais Magufuli, katika hotuba zake kadhaa, amekuwa anataka tumwombee. Sasa, kwa matukio haya, taifa limetambua nani anastahili kuombea – ni Tundu Lissu.
Sasa naelewa. CHADEMA na Tundulissu kinachowauma ni kuwa kaja shujaa mwingine kama yeye. Yeye (Lissu) nia yake awe shujaa pekee. Sasa kaja mpambanaji wa dhati, makini zaidi, si mropokaji. Inawauma. Ni kama ruwaya ya Shakespear: Mfalme Macbeth alimuua Jemedari waje Macduff kwa vile "ananipunguzia sifa kwa wananchi".

Ushujaa wa Lissu ni wa kijambazi - wao wazungu huita extortion. Ni wazi anajua kuwa hana madaraka ya kutekeleza matakwa yake, wakati Rais anayo madaraka hayo. Lissu anasema, Magufuli anatenda. Hata kwa Professor Mruma anaona wivu huo huo: Prof katoa data ya wizi na thamani yake, Lissu ni blablabla tu, no data no nothing. Lussi awaka: anawaita eyi "Professorial rubbish". Can you believe that? Jamani, lugha ya kibunge hiyo? Lissu hajawahi na hatawahi kuwa Professor: inamuuma maskini!

Anachofanya Lissu ni kuwaogofya Barrick ili baadaye wampe chochote kitu; au apate sifa aombe kura za wananchi wasiojua undani wa mambo zaidi ya kelele zake na lugha ya matusi, awe mbunge ili ashibe tumbo lake.

Keleleza chura hazimzuii fisi ku ywa maji: Barrick wako pale pale. Magufuli kaweka ngumu, Rais wao kaja Dar kwa ndege ya bei mbaya toka Toronto, kututaka suluhu; lakini Lissu tangu 1999, ni Wakurugenzi wa Barrick wamekuja? Mara ngapi? Neri!

Lakini kelele na kejeli na matusi? Hapo umefika. Kwa uchungu mkubwa, bila aibu, kama mtoto wa kindimu akifungwa goli, hukimbia na mpira kwapani. Kaamua kutemea mate mpira, kutusaliti kwa kuwapa nyaraka za mahakama maadui wetu ili wakamate bombadier yetu. Mzee Duni Haji angesema: Aiiiibuuuu!!!

Lissu tulimuona wazi akishangilia ndege yetu kushikwa: uzalendo gani huo? Kama mtoto mtukutu, kaamua kutema mate kwenye chapati ili tukose wote.

Yuda Iskarioti. Hiyo ndiyo tafakari yangu ya hoja ya Ansbert Ngurumo.
Bill Marconi.
 
Mkuu una maswali mazuri na fikirishi.. Sipendi nionekane najitetea au natetea serikali kuhusu hili.Nakupa mfano mmoja.,ukiwa unagombana na mkeo kila mara kwa sauti,huku ukiwa unampiga mikwara kibao.Huku majirani wakitega sikio na kusikiliza ugomvi wenu,siku ikitokea akapatwa na madhara moja kwa moja,majirani watajua kuna namna unahusika kutokana na ugomvi wenu wa mara kwa mara,wakati huo huo kutokana na ugomvi wenu kama kuna jirani yako yeyote alikuwa na visa binafsi na mkeo anaweza kumdhuru mkeo akijua wote watakuhisi wewe.Tukirudi kwenye ishu ya Lissu,kwa mtiririko wake wa kisiasa alikuwa anajenga hali tofauti,kumbuka tupo kwenye vita kali sana.Huwezi kunishawishi kwamba adui wa Lissu ni serikali ya TZ,hakuna mtu mwingine anaweza kuwa adui yake.So,yawezekana serikali ikahusika au akawa mtu mwingine,ila mimi hapa JF naongelea kwa ujumla Lissu angekosoa bila kejeli,na madharau na kuwa mwiba kwa serikali,asingetoa mwanya kwa serikali au mtu yeyote kumshoot kwa kisingizio chochote,inaweza isiwe serikali na bado aliyempiga risasi asipatine wala kujulikana milele,hata ungewaita CIA au scotland yard,aliyemuua JF Kennedy aliwahi patikana?,aliyemuua 2Pac aliwahi kujulilkana?,tukubali ukweli kuwa Lissu alisahau yeye sio Raisi wa Jamhuri,ingawa upo sahihi kauli nyingine za Raisi sio nzuri.

Hapo kwenye red mmempeleka sana Mahakamani lakini hajawahi kukutwa na hatia..Labda kama tuna hukumu kwa maono yetu kimtaa...

Hapo kwenye blue asante kwa kuwa muungwana kwa kukubali mapungufu ya Raisi ,ulicho sahau ni kumkemea Lissu na kumuacha Mh Raisi as if yupo sahihi kwa kauli zake tata na mbaya ktk jamii...
 
Jmc06, nafarijika na jambo moja tu: Watanzania wa aina yako ni wachache sana. Karibu wote wameguswa na kutiwa simanzi na huu uovu unaofurahia wewe. Huu siyo utamaduni wa siasa za Tanzania na haukubaliki kwa sababu yoyote ile. Hawajapata kuona wala kufikiria kuwa uovu kama huu unaweza kufanyika mbele ya macho yao na hawautaki. Sasa ninyi mliomwagika humu jf kwa kutumwa au kujituma wenyewe kuuhami utawala unaonyoshewa vidole ndio kwanza mnatuamabia eti 'huwezi kushindana na serikali'! Hiyo ndiyo lugha ya kuzungumza nao! Kwa hiyo serikali ndiyo inafanya uovu huu? Very very primitive propaganda, to say the least. It is horrible that this once great country has descended so low so fast.
 
Ndugu zangu wana JF, tupo katika kipindi kigumu cha vita vya uchumi , kwa hiyo tutasikia mengi sana na yatatokea mengi, lakini hatimaye tutashinda.
 
Back
Top Bottom