Kisa cha MwanaHALISI kufungiwa ni Habari ya "Nani anastahili kuombewa kati ya Lissu au Magufuli"

Kwahiyo kwasababu kuna majambazi mengi ambayo yapo jela baada ya kupelekwa mahakamani,tuamini mtaani hakuna majambazi sababu hayajakamatwa na kudhibitishwa?,

Bahati mbaya sana, ni Hakimu au Jaji tu ndiye ana uwezo wa kumhukumu, na 'kumpa' majina kama jambazi n.k.

Endapo kuna mtu anatuhumiwa kwa ujambazi, kwa sababu amehusika ama kuhisiwa kuhusika na ujambazi, polisi uwa wanamsaka mtuhumiwa huyo ili afikishwe Mahakama na kushitakiwa kwa ujambazi. Ambapo tuhuma zaweza kunadilika na kuwa makosa yenye kustahili adhabu.

Hivyo, kwa mtu anayejielewa ukishamwita au kumtuhumu mtu na ujambazi, dawa ni mtu huyo kufikishwa Mahakamani. It is that simple bro.

hivi huwa mnatoa wapi ujasiri wa kumtetea Lowassa wakati viongozi wenu wote walisema hadharani EL ni fisadi na ushahidi wanao na video zipo Youtube???,au ndo maana mlipewa lile jina la wanyama wa Serengeti??

Wapi nimtetea Lowassa? Viongozi wangu ni akina nani hao? Tulipewa mimi na nani? Nimeongea niku-address wewe, unajibu kwa kunijumuisha sijui na kundi gani?!?

Btw, the iron is CHADEMA alleged Lowassa for ufisadi (putting him in the List of Shame), but CCM defended Lowassa, even campaigned for him in Monduli several times. Now CCM acts like it has never defended Lowassa when he was shamed for ufisadi!! Only imbeciles would understand these wacky politics.
 
Huwezi shindana na SERIKALI yoyote duniani ukafanikiwa,mbaya zaidi serikali ya Tanzania,kilichomponza Lissu ni kutafuta sifa na kuwafurahisha baadhi ya watu,ndo hicho hicho kilichowaponza MWANAHALISI tofauti ni kuwa mwanahalisi wali target pia mauzo makubwa,mwisho wa siku nani anaumia???

....Kwa hiyo akina late Nyerere, Mandela and the like wangeitikia mawazo yako leo tungekuwa huru? Kama watu wangekaa kimya leo mabilioni ya Escrow, EPA etc si ndiyo ingekuwa basi tena?
 
Ngurumo asante kwa makala haya na RoU asante kwa kuyabandika hapa JF. Nilichofanya ni kuya- Copy & Paste in case JF inafungiwa. Ninafahamu haipiti muda mrefu JF itaondoka. Wajukuu na vitukuu wataona kuwa si babu na bibi zao wote walikuwa wendawazimu.
 
Taratibu taratibu tunageuka kuwa 'a police state'. Sishangai hata hao wanaomtetea maana hata akina Hitler,Mobutu nk walikua na wafuasi wengi tu
 
Leo Gazeti la Mwanahalisi limefungiwa kwa muda wa miaka miwili. HII NDIO MAKALA ILIYOPELEKEA MWANAHALISI KUFUNGIWA!

Tumwombee Magufuli au Tundu Lissu?

Na Ansbert Ngurumo

TANGU Tundu Lissu alipoanza kusisitiza mara kwa mara kwamba mambo mengi yanayofanywa na Rais John Magufuli ni ya kukurupuka, na yataleta hasara kubwa kwa taifa, rais na baadhi ya wafuasi wake wamekuwa wakisisitiza kuwa yeyote anayempinga rais ni msaliti.

Hata majuzi, katika moja ya hotuba zake mubashara za hivi majuzi, Rais Magufuli alisema:

“Nilipokuwa nikizungumza, ndugu zangu, kwamba hii ni vita ya uchumi, na vita ya uchumi ni mbaya kuliko vita ya kawaida.

“Vita ya kawaida, adui unamuona. Na saa nyingine msaliti anapowasiliti mkiwa katika vita ya kawaida, askari wanajua kazi yao huwa wanafanya nini.

“Huwezi kuwa msaliti halafu ukawa… uka-survive (ukanusurika, yaani ukaachwa uishi).”

Kwa Rais Magufuli na baadhi ya wapambe wake, Lissu ni msaliti, si mzalendo.

Katika mtandao mmoja wa kijamii, wiki kadhaa zilizopita, kuna mtu alithubutu kumshambulia Lissu kwa maneno hayo makali, akisema kuwa mbunge huyo wa Singida Mashariki si mzalendo.

Lissu hakusubiri mtu huyo ajibiwe na watu wengine. Alijibu mwenyewe akisema:

"Na mimi ni Mtanzania pia. Tofauti kati yangu mimi na wewe na Magufuli ni hii. Mimi nimepigania nchi yangu katika masuala haya (ya madini) tangu mwaka 1999.

Wakati huo, tulikuwa na mgodi mmoja tu wa dhahabu – Resolute Golden Pride Nzega. Bulyanhulu ilikuwa haijajengwa. Geita ndio kwanza walikuwa wanafukuza wanakijiji wa Mtakuja.

Nadhani nilikuwa wa kwanza katika nchi hii kupiga yowe kwamba tutaibiwa sana kwenye sekta ya madini.

Wewe sijui ulikuwa wapi wakati huo. Najua Magufuli alikuwa wapi. Alikuwa upande wa CCM na wawekezaji hawa.

Nimepigana na wawekezaji hawa mahakamani, kwenye medani ya kisiasa ndani na nje ya nchi hii kwa zaidi ya miaka 15. Nimetetea wananchi bila kudai malipo Bulyanhulu, Tarime, Nzega, Geita, na kadhalika.

Sijui wewe ulikuwa wapi, lakini najua Magufuli alikuwa upande wa nani – alikuwa upande wa CCM na wanyonyaji hawa.

Soma gazeti la Rai la tarehe 17 Julai, 2001, uone tulimwambia nini (Rais Benjamin) Mkapa siku alipokwenda kuzindua Mgodi wa Bulyanhulu.

Sijui ulikuwa wapi, lakini najua Magufuli alikuwa wapi. Alikuwa anatetea “tumbo lake” na matumbo ya wanyonyaji hawa.

Nilikamatwa na kushitakiwa kwa uchochezi kwa sababu ya (kutetea wananchi wa) Bulyanhulu. Hiyo ilikuwa December 2002. Nilikaa na kesi hiyo mahakamani Kisutu kwa miaka sita.

Sijui ulikuwa wapi, ila najua Magufuli alikuwa wapi. Alikuwa upande wa watesi wa wananchi na wanyonyaji wa rasilimali zetu.

Leo Magufuli anajifanya mzalendo, na anahoji uzalendo wa yeyote anayepingana naye. Ni muongo.

Anatafuta umaarufu wa kisiasa kwa wasiojua na wasiokumbuka. Ataupata kwa siku chache tu. Zingatia maneno yangu. Ataumbuka, na (nyie mnaomtetea) mtaumbuka.

Mimi ninampinga hadharani. Mimi si mnafiki, na sijahongwa. Ninampinga kwa sababu atatusababishia matatizo makubwa zaidi kuliko tuliyonayo sasa.

Huo mchanga (makinikia) atauachia upelekwe ambako umepelekwa kwa miaka 16 iliyopita. Kama sheria ndiyo hiyo na mikataba ndiyo hiyo, hana pa kwenda.

Tatizo ninaloliona ni kwamba wakati atakapokuwa anawarudishia mchanga wao, Tanzania itakuwa imekuwa hohe hahe kama Zimbabwe.

Na tutakuwa tumelipishwa fedha nyingi ya fidia na mahakama za usuluhishi za kimataifa kwa kuvunja mikataba na wawekezaji hawa.

Kama kuna anayefikiri uzalendo ni kufumbia macho masuala haya, basi huyo na amuunge mkono Magufuli kwenye upofu wake wa kujitakia.

Ripoti ya Prof. (Abdulkarim) Mruma haitamaliza hata nusu saa, iwapo itachunguzwa kwa kina.

Zaidi ya majina ya maprofesa walioiandaa, ripoti hii haina msingi wowote wa kuaminika. Ni kazi ya kisiasa iliyopakwa rangi ya usomi.

Kama umefuatilia taarifa za kitaalamu za Bulyanhulu hata kabla ya Barrick Gold kuingia mwaka 1999, utajua ninasema nini.

Sutton Resources, Outukumpu Oy, na hata STAMICO walishafanya utafiti mkubwa juu ya utajiri wa Bulyanhulu.

Taarifa zipo na zimekuwepo kwa hata mbumbumbu wa jiolojia ya madini kama mimi.

Hiki alichoambiwa Magufuli ni ujinga, hata kama ni wa kiprofesa. Hatuibiwi kwenye mchanga.

Huo ni ujinga unaoweza kukubaliwa tu na watu mbumbumbu. Tunaibiwa kwenye sheria. Kama hamuoni hilo, basi, Mungu na atusamehe!"

Kama serikali inasaini mikataba mibovu, na Lissu anapiga kelele kwamba mikataba hii ni mibovu na itaingiza taifa katika hasara, msaliti ni yeye anayesema au maofisa wa serikali waliosaini mikataba hiyo?

Msaliti ni yeye au rais anayetaka kumnyamazisha ili nchi isisikie sauti yake ya kinabii?

Kama viongozi wetu wamevunja mikataba; uamuzi wa viongozi wetu ukasababisha tushitakiwe, tukashindwa katika mahakama za usuluhishi; msaliti ni Lissu anayesema tumeshitakiwa na tumeshindwa?

Kama tunadaiwa na makampuni ya nje, yakakamata ndege yetu, Lissu akasema ndege yetu imekamatwa kwa sababu ya uamuzi mbovu wa viongozi wetu, na akasema watakaolipa fedha hizo si viongozi bali ni wananchi maskini; msaliti ni yeye au hao waliosababisha madhira hayo?

Kama rais anatoa amri zinazopoka uhuru wa wananchi kufikiri, kujieleza na kukusanyika – kinyume cha katiba – na Lissu anajitokeza kusema huu ni udikteta uchwara; inatosha kumuita msaliti?

Na katika mazingira ya “ugomvi” tunaoshuhudia mfululizo kati ya serikali na Lissu, na kwa kuzingatia matamko mabaya ya viongozi wakuu wa serikali dhidi yake; na sasa amepigwa risasi mchana kweupe, tutarajie nani awe mtuhumiwa wa kwanza dhidi ya Lissu?

Nimesikia kauli tata za viongozi wa jeshi la polisi na jeshi la wananchi. Wanazungumza kisiasa na kwa jeuri isiyotarajiwa, kubeza wananchi wanaohoji unyama aliofanyiwa Lissu.

Kwa hili la Lissu, serikali na wapambe wake watatunga propaganda za kutoa watu mstarini, lakini tayari naona Mungu amewakatalia.

Rais Magufuli, katika hotuba zake kadhaa, amekuwa anataka tumwombee. Sasa, kwa matukio haya, taifa limetambua nani anastahili kuombea – ni Tundu Lissu.
Msaliti yoyote vitani unauwawa.
 
Huyo Luwasa Sioni Sehemu Katajwa Kwnye Ufisadi,napia C Mlianzisha Mahakama Za Kifisadi?Kwnn Msimpeleke Huko?
IMG_20170901_212840.jpg

Sasa lengo la hawa viongozi lilikuwa ni nini?
mimi hapa ndipo wananasiasa huwa wananichosha kabisa.
 
Mkuu naheshimu mawazo yako na nakupa heko kwa kujaribu kuwa neutral.Kwanza JPM asingeweza kupiga kelele zozote kuhusu madini akiwa waziri wa kawaida,matokeo yake CCM wangeogopa hata kumpitisha kugombea kiti cha uraisi.Na huyu Lissu siku zote ambazo anaita media au kwenye tweeter zake hakuna siku hata moja amewahi kukubali au kupongeza jambo lolote alilowahi kufanya JPM,hii inakupa picha gani?,wewe mbona kuna mahali hapa umekubali mazuri au nia nzuri ya JPM?.. hii haikuwahi kuwepo kwa Lissu,,kuhusu kupigania madini huko nyuma,sote tunakubali alikuwa mpiganaji mzuri,sasa tulitegemea kipindi hiki aungane na serikali huku akitoa maoni kistaarabu namna ya kuendeleza mapambano,.,hivi mtu akikutishia TUTANYOLEWA KWA CHUPA,unapata picha gani?,mtu anaposimama mbele ya vyombo vya habari akasema tuna SERIKALI YA OVYO inaleta picha gani? serikali ya ovyo unamaanisha Jeshi la ovyo,polisi ovyo,magereza ovyo,mahakama ovyo,na taasisi zote za serikali ovyo.,hii ni SAWA?,.Katika wanasiasa na wanaharakati wote wa dunia hii ukianzia na akina Nyerere,Sokoine,Mandela,Kwame Nkhuruma,Odinga na wengine wote,nipe mfano wa aliyekuwa na lugha kama za Lissu aliyepata mafanikio na kufika mbali?,tatizo hamtaki kukubali Lissu alizidiwa na jeuri na kitu inaitwa kujifanya ni mjuaji sana pengine kuliko mwanasiasa yeyote TZ na nyie mkawa mnampamba kumtia ujinga.

Mimi alipoiita report ya wasomi wenzake akina Prof Mruma kuwa ni takataka hakika nilimshangaa sana!, maana huwezi kuwa arrogant wa kiwango hicho mpaka ifike mahala ushindwe kutambua mchango wa watz wenzako na kuamini kile usemacho wewe ndio sahihi,hata kama zilikuwa na mapungufu, lugha iliyotumika kwakweli haifai kwa kiongozi.
 
Mimi niliongea neno moja tu kutokana na kauli zake,huyu kuna kitu anakitafuta na very soon atakipata.Nilikuwa naona kundi lolote kutoka upande wowote likichukulia udhaifu wake huo kumjeruhi.Kwa nia yoyote waijuayo,lakini nilijua hilo swala lipo njiani.Kuna vijana walianzisha namna fulani ya kampeni kwenye mitandao wakaanzisha slogani ya Lissu4 2020,naona hii ndo ilimpa kichwa akawa anajichukulia kama Raisi mtarajiwa.Huwezi simama ukasema tuna raisi wa ovyo,au tuna serikali ya ovyo,na zile ripoti za makinikia akaziita ni proffesorial rubish,tena mbele za media.Na bado kuna watu wanadai huo ndo uzalendo... Hakufunzwa na ***** ngoja afunzwe na ulimwengu.
 
Huwezi shindana na SERIKALI yoyote duniani ukafanikiwa,mbaya zaidi serikali ya Tanzania,kilichomponza Lissu ni kutafuta sifa na kuwafurahisha baadhi ya watu,ndo hicho hicho kilichowaponza MWANAHALISI tofauti ni kuwa mwanahalisi wali target pia mauzo makubwa,mwisho wa siku nani anaumia???
Sasa hapa unataka kusema nini? Kwamba tunapaswa kunyamaza? Tusihamaki, tusinune, tusivimbishe mashavu kwa hasira, tusihoji, tusiulize wala tusiongee? Una maanisha nini?
 
Sasa hapa unataka kusema nini? Kwamba tunapaswa kunyamaza? Tusihamaki, tusinune, tusivimbishe mashavu kwa hasira, tusihoji, tusiulize wala tusiongee? Una maanisha nini?
Mkuu tuwe wawazi na wakweli mbona tupo huru sana kufanya mambo mengi tu nchini mwetu?,ila kuna baadhi ya watu katika nafasi zao wanasahau kuwa kila uhuru una mipaka.Huwezi mwambia baba yako kama kiongozi wa familia kuwa anaongoza familia ovyo ovyo,hata kama anakosea kuna namna ya kufikisha ujumbe sio kwa kejeli tena mbele za watu.
 
Mfano wa baba na familia yake hauakisi nilichohoji. Baba hutafuta kwa jasho kuilisha /kuitunza familia. Serikali ya Tanzania hutwaa kodi na kukopa (walipaji ni wananchi) ili kuendesha nchi. Kwa nini isihojiwe, isipewe changamoto, isinuniwe, na hata kupingwa (kuwa na wakinzani)?
Na ni vema mumshauri (kama ameanza kushaurika) aelewe kuwa kuongoza nchi si sawa kabisa na kuongoza familia. Havifafanani.
 
Huwezi shindana na SERIKALI yoyote duniani ukafanikiwa,mbaya zaidi serikali ya Tanzania,kilichomponza Lissu ni kutafuta sifa na kuwafurahisha baadhi ya watu,ndo hicho hicho kilichowaponza MWANAHALISI tofauti ni kuwa mwanahalisi wali target pia mauzo makubwa,mwisho wa siku nani anaumia???
umesoma History ya wapi ww?
 
Una akili kama Daudi Albert BASHITE lile jizi la vyeti. Mwalimu nyerere angewaogopa wakoloni we usingekuwepo hapo lumumba, Mandela angekuwa na akili kama za kwako leo kuburu bado angendelea kuwepo nchini kwake hivi kwa akili zako za kawaida ni wapi lisu alishawahi kushindana na serikali? Hujawahi kujiuliza kwann kila siku mawio, mwanahalisi na mseto tu? Hujawahi kujiuliza kwann yule mzee.wa.mabehewa mabovu. Ndugu mwakiembe alipiga marufuku uchambuzi wa magazeti kwenye radio? Kama hujui jua serikali haitaki watu waamke. Nawe unaaminishwa upuuzi
Huwezi shindana na SERIKALI yoyote duniani ukafanikiwa,mbaya zaidi serikali ya Tanzania,kilichomponza Lissu ni kutafuta sifa na kuwafurahisha baadhi ya watu,ndo hicho hicho kilichowaponza MWANAHALISI tofauti ni kuwa mwanahalisi wali target pia mauzo makubwa,mwisho wa siku nani anaumia???
 
Nibora wangelikuwa wapuuzi hata Mia 7
Walau sasa huyo Lissu awe zaidi ya Rais kweli!
Hueleweki hapa? Ni kwanini asiwe maarufu kuliko rais? Mandela alikuwa maarufu kuliko marais wa S. A kipindi kile! Kina Ronaldo na Messi kuliko marais wao na Lissu kuwa maarufu hakumfanyi mumpige risasi! Njoo kivingine na somo la umaarufu.
 
Huwezi shindana na SERIKALI yoyote duniani ukafanikiwa,mbaya zaidi serikali ya Tanzania,kilichomponza Lissu ni kutafuta sifa na kuwafurahisha baadhi ya watu,ndo hicho hicho kilichowaponza MWANAHALISI tofauti ni kuwa mwanahalisi wali target pia mauzo makubwa,mwisho wa siku nani anaumia???
Haya ni mawazo ya kiuoga na ya kijinga kabisa na yasiyo na faida kwa nchi yoyote duniani
 
Back
Top Bottom