Kisa cha "Mjamaika" kimezua jambo! - | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kisa cha "Mjamaika" kimezua jambo! -

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mzee Mwanakijiji, May 28, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  May 28, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Nusura nipost sehemu ya mwisho ya "Kumbatio" ndipo nimekutana na email ndefu yenye kunilalamikia na kunidokeza kuwa kisa hiki kimetokana na kisa cha kweli na kuwa yawezekana nimesimuliwa na mtu wa karibu wa wahusika. Na kwamba licha ya kujaribu kugeuza mambo mbalimbali kisa hicho ni kweli kimemkuta bosi fulani ambaye ni mwanasiasa maarufu.

  Baada ya kuandika kwa kirefu, mwandishi (ambaye anajina la huyo bosi na nikitaja tu wote mtamjua) anamalizia kwa kunipa wito, kunitaka, kuniamuru or whatever have you...
  Baada ya kurudia rudia kijibarua hicho nimejikuta nina utata na kuanza kujiuliza maswali kwani ni kweli kisa hicho kimevuviwa na tukio la kweli japo simulizi lake ni la kutunga na manjonjo yamo humo humo lakini kwa asilimia 100 jina la huyo bwana halihusiani na kisa labda matukio yamefanana tu. Lakini hata hivyo kama anaamini ndiyo yeye basi ninajikuta kwenye utata. KUendelea na kumalizia au kujaribu kukibadilisha zaidi na kuruka simulizi la Jumamosi au kulibadilisha kabisa?

  Naomba mpige kura kwa kuzingatia kiwango cha ukweli kilichomo ndani. Nataka nifikir uamuzi ifikapo J'pili ili kama kisa kitakuwa kimeisha niwaambia au kama ndio nikiposti kiishe niwapostie maana Jambo limezua Jambo!
   
 2. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #2
  May 28, 2010
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Mie jibu langu ni SIJUI( nadhani inaruhusiwa kama vipimajoto vya itv)
   
 3. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #3
  May 28, 2010
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  AAAHHHHHHHHHHHHHHHHHHHHHH!!
  Kwani kuna kisa ambacho ni cha kipekee hapa duniani? Maisha is just a big rehearsal and performance inafuata hahahah
  Huyu Waziri au sijui mwanasiasa aanze mbele huko! SISI TUPATIE ILE KITU ROHO INATAKA..... HATA KAMA NI MAMA/BABA YANGU MZAZI MLIPUE TU!
   
 4. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #4
  May 28, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Mmmh Mwanakijiji umeniacha hoi ...hee kumbe haya mambo yapo eeh?
  Huo ni utunzi wako we endelea kutupa burudani,hadithi nyingi huwa ni mifano halisi iliyopo na inayoendelea kutokea
  Gud Lucky
   
 5. L

  Lady JF-Expert Member

  #5
  May 28, 2010
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 280
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Usivunjike moyo Mzee Mwanakijiji, Keep on going!
   
 6. JS

  JS JF-Expert Member

  #6
  May 28, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  MMJ mambo kama hayo mbona yapo hata kama ni kiongozi gani yapo. We endelea tu kutupa uhondo wetu tujifunze na mambo mengine hususan ya ndoa kwa wale ambao bado hatujaingia anga hizo. haijalishi kama ni boss au nani yeye atulize tu.
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  May 28, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Pigeni kura..mnisaidie kuamua.. sitoweza kusoma kila posti..
   
 8. K

  Kwayu JF-Expert Member

  #8
  May 28, 2010
  Joined: Nov 8, 2007
  Messages: 487
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kura za nini bwana? we tupe burudani
   
 9. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #9
  May 28, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  hahaha acha uvivu bwana kura tunapiga na kupost tunaendelea don worry
   
 10. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #10
  May 28, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Mpaka hapa hamna alisema usiendelee kwahiyoooo...tupe ile kitu roho inapenda!!:rofl:
   
 11. Egyps-women

  Egyps-women JF-Expert Member

  #11
  May 28, 2010
  Joined: Feb 5, 2010
  Messages: 499
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Tupe uhondo Mwanakijiji..
   
 12. Homo Habilis

  Homo Habilis Senior Member

  #12
  May 28, 2010
  Joined: Jul 2, 2009
  Messages: 189
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mwaga uhondo Mwanakijiji mwenzangu ikiwezekana toa kitabu kabisa ikishindikana mi naprint kopi zangu nikaweke kwenye ki maktaba changu hata junior wangu akikua akikute hichi kisa ili naye apate somo hapo.
   
 13. daughter

  daughter JF-Expert Member

  #13
  May 28, 2010
  Joined: Jun 22, 2009
  Messages: 1,274
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  haya mambo yapo na yataendelea kuwepo,huyo yaliyomkuta leo hatakuwa wa mwisho.
  aandike kuumia,tupe burudani kama kawa
   
 14. ngonzi zomukama

  ngonzi zomukama Senior Member

  #14
  May 28, 2010
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 170
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  lete uhondo
   
 15. A

  AmaniGK JF-Expert Member

  #15
  May 28, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,101
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Mwanakijiji labda kwa akili tu za kawaida unadhani ni watu wangapi watakaosema usiendelee?hiyo Poll yako haina tofauti na zile za ITV zinazojua majibu lakini wanaendelea tu kuuliza.
   
 16. shejele

  shejele Senior Member

  #16
  May 28, 2010
  Joined: Aug 5, 2008
  Messages: 140
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mwanakijiji ongeza; Asilimia 90 ukweli 10 Uongo- iendelee.

  dhumuni ni kutuburudisha na kutuelimisha, kwa hivyo mi naona iendelee tu.
   
 17. Mom

  Mom JF-Expert Member

  #17
  May 28, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  majibu ya poll ushayapata tuendelee basi mwanakijiji
   
 18. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #18
  May 28, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Mwanakijiji nadhani katika watu wa kwanza kuisoma na kuvutiwa moja kwa moja na kuichagiza kuwa usiiache kuandika hadithi hapa jukwaani mie ni mojawapo!

  Maoni yangu ni kama ifuatavyo!

  1. hadithi kama sehemu moja wapo ya fasihi inatumika kufundisha; hivyo iwavyo vyovyote lazima itachukua mifano halisia! sisi kama hadhira yako tunajifunza mengi humo na waliomo kwenye ndoa wataungana nami! Hivyo unao wajibu kwa hadhira yako!

  2. Malipo ya dhambi ni mauti; ukisoma katikati ya mistari sio lazima ufe kwa maana ya kupoteza uhai; hata hayo majuto na machungu ndio sehemu ya malipo ya dhambi yako : Kwako MWANASIASA; Mwanakijiji hatekelezi hukumu yeye sio Mungu na wala hana nafasi ya ku-compromise nawe kuhusu hilo! jamii itamsuta na atakuwa ametenda dhambi kwa kutomalizia mafundisho yake; unapaswa ukamwombe Msamaha Mungu wako naye ndiye mwenye kukuponya na machungu yako utakapoupokea msamaha wa kweli na si kwa kuufunika uovu wako NO!

  Mwanakijiji Kanyaga Twende mwanawane!
   
 19. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #19
  May 28, 2010
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,646
  Likes Received: 1,473
  Trophy Points: 280
  hadithi iendelee mi nilikuja kudownload chapter 6 ya jumamosi manake ndo fainali pale:drum:
   
 20. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #20
  May 28, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  siamini kama wewe huwa unasoma hadithi ..inawezekana unaprint unapeleka kwa wife anasoma kisha anakusimulia...
   
Loading...