Kisa cha majuha watatu.

Kisa cha majuha watatu.

Abu-Musab

Senior Member
Joined
Oct 27, 2011
Posts
156
Reaction score
92
1.- Katika kijiji cha Kazamoyo, aliishi mkulima mmoja ambaye alikuwa masikini akiwa na mke wake na binti yao mwenye umri wa takriban miaka 16 hivi. Mtu huyu alikuwa akiitwa Makolo, akimili kibanda cha udongo kilichoezekwa nyasi, huku akiwa ng'ombe mmoja jike. Alijishughulisha na kilimo katika shamba alilorithi kutoka kwa wazazi wake ambalo lilikuwa umbali wa kiasi cha maili mbili na nusu kutoka kijijini kwake.

Siku moja Makolo alitoka alfajiri kama kawaida yake na kwenda shambani ambapo aghalabu alikuwa akirejea jioni, huku nyuma mke wake akasikia kwikwi kutokea chumbani kwa binti yao. Hima akaenda chumbani kwa binti kujua kilichojiri na kupelekea binti huyo kulia. Aligonga mlango na kujikita ndani ya chumba bila kusubiri neno karibu. Alipomhoji binti kisa cha kulia, ndipo binti alipobainisha kuwa ati alota ndoto kwamba amejifungua mtoto wa kiume na mtoto akafariki baada tu ya kuzaliwa...ghafla mama naye akaangua kilio kikuu kilichoalika majirani hatimaye wanakijiji wengi. (Itaendelea)
 
Nini hii?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom