Kisa cha kweli cha binti kutoka Bukoba

Kisa cha kweli cha binti kutoka Bukoba

Rich Pol

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2013
Posts
7,880
Reaction score
5,725
Nilipoingia katika mahusiano nayenilimuamini, nikampa kila kitu nilichoweza. Nakumbuka enzi zile nyumbani tulikuwa tuna ng'ombe, niliiba maziwa kila siku na kumpelekea kwao.

Akanenepa!! Penzi letu likawa huru alipoanza maisha yake mwenyewe. Sikuwa najua lolote kuhusu mapenzi. Alinifundisha. Nikaegemeza maisha yangu yote kwake. Akanifany a nikawa mtumwa wa ngono kila nikienda chumbani kwake.

Kama haikutosha sasa akaanza kunifundisha kunywa pombe, niliamini kuwa ndiye mume wangu mtarajiwa, kwa nini nikatae? Nilimkubalia kila kitu. Alinilazimisha ngono hata nilipokuwa katika siku zangu.

Kweli nilikuwa msomi na niliyajua madhara ya kufanya hivyo lakini sikutaka kumuudhi huyo niliyeamini kuwa ni mume wangu. Nilipenda tututmie kinga lakini aliipinga sana.

Nikapata mimba yakwanza!! Hakuwa na pesa lakini alinilazimisha niitoe. Nikaiba pesa nyumbani nikafanyaalivyo taka. Kwa mara ya kwanza nikatoa mimba. Haikuniuma sana!! Niliamini kuwa ni yeye atakuja kunioa na atanifichia aibu hii.

Nilitegemea sasa tutaanza kutumia kinga. Lakini hapana haikuwa hivyo. Aliendelea kunilaghai. Tayari aliujua udhaifu wangu. Alinishika hapa na pale. Nikishtuka tayari amefanya anavyojua.

Pombe kidogo na nyingine kidogo. Nikazoea lakini nikawa nawahi kulewa. Akautumia udhaifu huu kunifanyia jambo baya lililonifanyaniandike haya kwako. Akaniingiliakinyume na maumbile. Alinilawiti!!

Nilishindwa kumshtaki popote. Nikavumilia kwa kuwa alikuwa mume wangu mtarajiwa. Mume asiyejulikana hata kwa wazazi. Mchezo ule ukaendelea. Akajitetea eti hataki nipate mimba tena, hivyo hiyo ni mbinu mbadala. Najuta kumuamini!! Lakini huyo alikuwa mume wangu.

Miaka ikapita, ule urembo wangu niliozoea kuuona katika kioo ukatoweka, simu za mara kwa mara kutoka kwake zikatoweka, akawa mkali sana kwangu. Hakutaka niende kwake.

Wakati huo nilikuwa nasoma chuo. Pesa ya mkopo ikitoka ananitafuta na tunakuwa marafiki tena. Anasema ananipenda na atanioa. Ananilewesha na kunitumia kinyume na maumbile.

Pesa ikiisha na mapenzi yanaisha nabakimwenyewe katika msoto. Sasa akaanza kubadilisha wasichana waziwazi. Ningesema nini mimi? Ninajua alishindwa kusema neno moja tu. Tuachane!!Nilijua tayari ameniacha!!!

Afya yangu ikadolola sana, nikalazimika kwenda kupima hospitali. Sikuwa na virusi. Nikapewa ushauri nikautumia. Siku zikasonga nikampata mwanaume mwingine.

Huyu alikuwa ananijali sana. Nikaanza kumsahau yule aliyenitenda. Nilipomaliza chuo akajitambulisha nyumbani na alitaka kunioa. Akanioa kweli. Maisha yakaanza.

Mwaka wa kwanza, mwaka wa pili na hadi wa tatu. Sikuwa nabeba mimba. Mume wangu alikuwa mvumilivu sana, hakuwa hi kunilaumu. Lakini niliumizwa na mawifi.

Nikaamua kwenda hospitali. Nikaambiwa kizazi changu kiliharibiwa kwa kutoa mimba mara kwa mara. Pia mapenzi ya kinyume na maumbileyamenivuruga kabisa.

Nililia sana huku nikimkumbuka yule aliyeuleta uchungu huu kwangu. Dunia haikuwa mahali pangu sahihi. Nimekuandikia barua hii mdogo wangu.

Uisome mwenyewe!! Lakini uwasimulie wengi baada yakifo changu. Uwasimulie bila kuchoka wasichana wa kileo wanaodanganyika na kufanya mambo magumu kuwaridhisha wapenzi wao.

Waambie watakufa kwa mateso kama mimi. Wasipokusikiliza usijisikie vibaya maana hata mimi nilikuwa siwasikilizi watu waliponambia lolote kuhusu yule mume mdanganyifu . Sitajiua lakini nitakufa kabla ya wakati!!!

Nimekuandikia wewe kwa kuwa u mwandishi. Japo kwa sasa u mtoto mdogo najua utaipata nafasi siku moja ya kuwafikishia wasichana hawa.

Usilie kwa sababu nitakufa. Lia kwasababu mwanaume mwenzako AMENITENDA HIVI!!
 
INASIKITISHA SANA! Pole sana na ninaomba usichukue hatua za kujiua kwani Mungu mwenyewe atatafuta njia mbadala ya kuktuliza kwa hayo uliyotendewa. Pia ninashukuru kwa kuliweka wazi ili wengine waweze kusalimika na visanga vya namna hii. Pole sana mkuu RICH POL
 
kisa chenye mafunzo makuu, natamani niwasimulie wadogo zangu wa kike, tatizo naanzaje????
 
Hii sio akili ni matope,unatoa Kabaang ili uolewe!
 
INASIKITISHA SANA! Pole sana na ninaomba usichukue hatua za kujiua kwani Mungu mwenyewe atatafuta njia mbadala ya kuktuliza kwa hayo uliyotendewa. Pia ninashukuru kwa kuliweka wazi ili wengine waweze kusalimika na visanga vya namna hii. Pole sana mkuu RICH POL[/QUOTE]

Mbona huyo unaemtaja kama mwanaume?
 
INASIKITISHA SANA! Pole sana na ninaomba usichukue hatua za kujiua kwani Mungu mwenyewe atatafuta njia mbadala ya kuktuliza kwa hayo uliyotendewa. Pia ninashukuru kwa kuliweka wazi ili wengine waweze kusalimika na visanga vya namna hii. Pole sana mkuu RICH POL[/QUOTE]

Mbona huyo unaemtaja kama mwanaume?

Hajasoma headlines huyo achana nae mkuu.
 
Akili za wadada wanajijua wenyewe aisee,,,Kweli akili ndio Serikali yako!


Sent from my iPad Air using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom