Kisa cha Engineer Rashid

Kisa cha Engineer Rashid

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,636
Reaction score
220,438
Rashid ni mtoto wa kwanza kuzaliwa kati ya watoto watatu. Wapili alipata scholarship kwenda kusoma nje ya nchi na watatu yuko chuo bado hapa hapa nchini.

Engineer Rashid amehitimu masomo yake na amepata ajira humuhumu mjini Dar. Kwa sasa bado anaishi nyumbani kwenye kile chumba cha wavulana. Baba na mama engineer ni wastaafu walioitumikia serikali ya awamu ya kwanza, ya pili na ya tatu.

Kwa nature ya kazi yake anakwenda sana field. Katika miezi mitatu ya kwanza ya ajira Rashid alijikuta ana milioni 20 balance ikiwa ni malipo ya mshahara na masurufu ya safari. Tangu anaanza kazi mzee alimfahanisha kuwa haihitaji pesa yake. Pesa yake aanze kupanga maisha yake.

Rafiki yangu Rashid alianza kununua TV ya 40” kwaajili ya chumbani kwake, hii ni maalum kwa kuangalia mpira hasa msure akiwa home na anaangalia mambo ya siasa.

Alinunua eclectric bed, unaweza kupandisha mgongo au miguu. Kitanda hiki si kwa apeche alolo.

Siku mizigo inafika na mzee alikuwepo. Baba yake alimuuliza Rashid hivi vitu ni vya nani? Alijibu kuwa ni vya kwake. Mzee aliuliza tena, vinakwenda wapi? Akasema chumbani kwangu. Mzee alipatwa na hasira akamwambia hivi wewe, mimi ningenunua masofa nikiwa kwa baba yangu ningekulelea wapi wewe?

Ndipo hapo Rashid alipoanza kutafuta kiwanja na kujenga nyumba yake akiwa kwa wazazi wake.
 
Akili ya Rashid ndio akili ya vijana wengi Sana wanaoanza ajira.

Anapanga mshahara wake ukitoka anunue sabufa, kasofa, flat screen ,simu kali , kafriji na vitu ambavyo hata usipokuwa navyo hupungukiwi kitu.
Hii yote watu wakija ghetto kwake hasa nyie wanwake "mshoboke" na kusema jamaa Ana maisha.
Lakini kumbe angesave huo mshahara hata kwa mwaka mzima pengine angepata hata mtaji wa biashara au hata kununua shamba.

Vijana wengi akili huwa zinapotea hapo.
 
Daahh so sad ".. vijana wa taifa hili baadhi yao ni empty set
 
Kwa mtazamo wangu engineer Rashid yupo sahii, kama ana balance ya 20m kutoa 3m kununua hivyo vitu ni sawa. Muda mwingi yupo field huko huwa mazingira sio rafiki(wanaofanya kazi za field wanaelewa) nyumbani ndio sehemu ya yeye kupumzika na kufurahia. TV kwa ajili ya kuangalia mpira ili asiwasumbue wengine na electric bed kupata pumziko alitakalo.
Tunaishi mara moja tu kwenye hii dunia ukipata nafasi ya kufurahia maisha unaitumia. Tatizo sisi watanzania tumeshazoea shida, vitu vya kawaida tunaona anasa.
 
Duuuuuuuuuu.Mwenyezi Mungu nakuomba baba, sisi vijana tusiwe kama Rashid,japokuwa wengi wetu ni akina Rashid.
 
Muda mwingi yupo field huko huwa mazingira sio rafiki(wanaofanya kazi za field wanaelewa) nyumbani ndio sehemu ya yeye kupumzika na kufurahia. TV kwa ajili ya kuangalia mpira ili asiwasumbue wengine na electric bed kupata pumziko alitakalo.
Tunaishi mara moja tu kwenye hii dunia ukipata nafasi ya kufurahia maisha unaitumia.
Mwenye macho haambiwi tazama
 
Rashid ni mtoto wa kwanza kuzaliwa kati ya watoto watatu. Wapili alipata scholarship kwenda kusoma nje ya nchi na watatu yuko chuo bado hapa hapa nchini.

Engineer Rashid amehitimu masomo yake na amepata ajira humuhumu mjini Dar. Kwa sasa bado anaishi nyumbani kwenye kile chumba cha wavulana. Baba na mama engineer ni wastaafu walioitumikia serikali ya awamu ya kwanza, ya pili na ya tatu.

Kwa nature ya kazi yake anakwenda sana field. Katika miezi mitatu ya kwanza ya ajira Rashid alijikuta ana milioni 20 balance ikiwa ni malipo ya mshahara na masurufu ya safari. Tangu anaanza kazi mzee alimfahanisha kuwa haihitaji pesa yake. Pesa yake aanze kupanga maisha yake.

Rafiki yangu Rashid alianza kununua TV ya 40” kwaajili ya chumbani kwake, hii ni maalum kwa kuangalia mpira hasa msure akiwa home na anaangalia mambo ya siasa.

Alinunua eclectric bed, unaweza kupandisha mgongo au miguu. Kitanda hiki si kwa apeche alolo.

Siku mizigo inafika na mzee alikuwepo. Baba yake alimuuliza Rashid hivi vitu ni vya nani? Alijibu kuwa ni vya kwake. Mzee aliuliza tena, vinakwenda wapi? Akasema chumbani kwangu. Mzee alipatwa na hasira akamwambia hivi wewe, mimi ningenunua masofa nikiwa kwa baba yangu ningekulelea wapi wewe?

Ndipo hapo Rashid alipoanza kutafuta kiwanja na kujenga nyumba yake akiwa kwa wazazi wake.
Simple and clear. Asiyekuelewe ama ana mtindio wa ubongo au yeye ndio rashidi halisi
 
Kwa mtazamo wangu engineer Rashid yupo sahii, kama ana balance ya 20m kutoa 3m kununua hivyo vitu ni sawa. Muda mwingi yupo field huko huwa mazingira sio rafiki(wanaofanya kazi za field wanaelewa) nyumbani ndio sehemu ya yeye kupumzika na kufurahia. TV kwa ajili ya kuangalia mpira ili asiwasumbue wengine na electric bed kupata pumziko alitakalo.
Tunaishi mara moja tu kwenye hii dunia ukipata nafasi ya kufurahia maisha unaitumia. Tatizo sisi watanzania tumeshazoea shida, vitu vya kawaida tunaona anasa.
Fanya ya msingi wanza. Hayo mengine yatafuata baada ya kukamilisha ya msingi.
Baada ya kupata kazi, fanya hivi:_
Hama home
Nunua kiwanja, anza kujenga japo rooms 2
anzisha biashara,
jiendeleze kwenya karia yako
oa,
nunua gari
 
Mkuu kwani ni lazima kuhama home(kupanga) ndio uanze kujenga kwako?
Kwa hali aliyonayo huyo engineer anaweza kuendelea kukaa kwao akawa anajenga nyumba yake.
 
Mzee wake anabusara, ameishi mjini muda mrefu, hana njaa ya pesa. Angemshirikisha mzee katika maongezi hata kusimamia ujenzi
 
Kwa mtazamo wangu engineer Rashid yupo sahii, kama ana balance ya 20m kutoa 3m kununua hivyo vitu ni sawa. Muda mwingi yupo field huko huwa mazingira sio rafiki(wanaofanya kazi za field wanaelewa) nyumbani ndio sehemu ya yeye kupumzika na kufurahia. TV kwa ajili ya kuangalia mpira ili asiwasumbue wengine na electric bed kupata pumziko alitakalo.
Tunaishi mara moja tu kwenye hii dunia ukipata nafasi ya kufurahia maisha unaitumia. Tatizo sisi watanzania tumeshazoea shida, vitu vya kawaida tunaona anasa.
Electric bed inasnzia milioni 15 ndiyo maana nilisema si cha apeche alolo.
Mzee ameona kama anaanza hivi Rashid atakuwa pale kwa muda mrefu sana. Ajenge kwanza ndiyo election bed ifuatie.
 
Tatizo la Baba Rashid ni kumuonya tu bila vitendo, alitakiwa amchape makofi na kumfukuza nyumbani siku ile ile aliyoleta haya madude yake bila kukumbuka hayana sehemu ya kuweka.
Tatizo kubwa la bwana mdogo Rashid ni kupenda sifa hata kama hazimsaidii.
Wito: Rashid aanza kujenga kwanza kabla ya kuleta furniture za kizungu kwenye vijumba vibovu vya baba, kama vip anza na ujenzi wa hivyo vijumba then furniture na tv za kizungu baadae
 
Back
Top Bottom