Kisa cha Engineer Rashid

Kisa cha Engineer Rashid

Electric bed inasnzia milioni 15 ndiyo maana nilisema si cha apeche alolo.
Mzee ameona kama anaanza hivi Rashid atakuwa pale kwa muda mrefu sana. Ajenge kwanza ndiyo election bed ifuatie.
Hapo mzee wake yupo sahihi.
 
Rashid ni mtoto wa kwanza kuzaliwa kati ya watoto watatu. Wapili alipata scholarship kwenda kusoma nje ya nchi na watatu yuko chuo bado hapa hapa nchini.

Engineer Rashid amehitimu masomo yake na amepata ajira humuhumu mjini Dar. Kwa sasa bado anaishi nyumbani kwenye kile chumba cha wavulana. Baba na mama engineer ni wastaafu walioitumikia serikali ya awamu ya kwanza, ya pili na ya tatu.

Kwa nature ya kazi yake anakwenda sana field. Katika miezi mitatu ya kwanza ya ajira Rashid alijikuta ana milioni 20 balance ikiwa ni malipo ya mshahara na masurufu ya safari. Tangu anaanza kazi mzee alimfahanisha kuwa haihitaji pesa yake. Pesa yake aanze kupanga maisha yake.

Rafiki yangu Rashid alianza kununua TV ya 40” kwaajili ya chumbani kwake, hii ni maalum kwa kuangalia mpira hasa msure akiwa home na anaangalia mambo ya siasa.

Alinunua eclectric bed, unaweza kupandisha mgongo au miguu. Kitanda hiki si kwa apeche alolo.

Siku mizigo inafika na mzee alikuwepo. Baba yake alimuuliza Rashid hivi vitu ni vya nani? Alijibu kuwa ni vya kwake. Mzee aliuliza tena, vinakwenda wapi? Akasema chumbani kwangu. Mzee alipatwa na hasira akamwambia hivi wewe, mimi ningenunua masofa nikiwa kwa baba yangu ningekulelea wapi wewe?

Ndipo hapo Rashid alipoanza kutafuta kiwanja na kujenga nyumba yake akiwa kwa wazazi wake.
Ni funzo kwa vijana wa leo...
Hasa hasa tunaoshindwa kujua priorities katika maisha.
ASANTE
 
Engineer alipaswa aelewe, yeye ana nunua eclectic bed kwenye nyumba ya mzee wake!
Alishindwa kutofautisha kwetu na kwangu...

Vijana wengi tunaweza kutofautisha hata mnyamwezi na msukuma kwa kuangalia tu lakini kutofautisha "kwetu" na "kwangu" pepa gumu sana...
 
Ujumbe kuntu kwa watozi wa kileo. Lakini unadhani suruwali zinazobana korodani zinaruhusu ubongo kufanyakazi ipasavyo?

Bazazi
 
Bibi mbona naona code code tu? nimesoma Mara tatu lakini waapi au una mzio wa wk end? 😀😀:
Du!.. Mzio...mzio... hili neno jipya, niliwahi kulisikia sana mahali!.🙄
 
Rashidi aunge mkono juhudi za rais ahame kwa baba yake ahamie Lumumba au nyumbani kwa Makonda
 
Back
Top Bottom