Kisa cha dada mmoja aliyerubuniwa na mwanaume Dar

Kisa cha dada mmoja aliyerubuniwa na mwanaume Dar

balibabambonahi

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2015
Posts
16,700
Reaction score
15,436
Siku ya jumatano, aliaga alikopanga Tabata. Njiani alisimamishwa na jamaa mmoja aliyekuwa anaendesha gari flani, yule jamaa akaomba namba ya simu kila mtu akaenda zake.

Huyu dada akapanda gari kwenda Ubungo mara yule jamaa akapiga simu na kumuomba ashuke na kwamba angemrusha kwenda Ubungo.

Jamaa kweli akafika dada akapanda.Walipofika kituo cha mafuta cha External,kulia as you are going to ubungo jamaa akaingia akanunua heinken ktk ki sub supasoko akampa moja mdada,dada alikataa kunywa lkn baadae akanywa then wakaingia external, shungashunga, mabibo hadi Sinza na baadae sayansi, wakasimama kununua chips.

Dada hakumbuki kilichofuata hadi mida ya saa tatu usiku alipojikuta yuko katikati ya watu kinyerezi mwisho. Wasamaria wakambeba bahati nzuri wakamfikisha kwenye grosery fulani ambako kna mtu alitokea kumfahamu, ikabidi watafute bodaboda ya kumfikisha kwake,asubuhi yake aliamka amevimba.

To cut the story short, walilamba simu, laki na nusu, cheni nk, baada ya vipimo dr alithibitisha hawakumtenda vibaya.

Nampa pole sana.
 
Miaka hii bado watu wanapanda lifti??? Huna hela ya bodaboda heri kutembea

Miaka hii bado unanunuliwa kitu cha kutia mdomoni na stranger unakula?????

Anyway pole yake

Binadamu wamekuwa wanyama sana siku hizi muwe makini
 
Kweli ni kupitwa na wakati. Wakati uko mbele wewe upo nyuma .
 
Pole zake...
Hivi hata km ni shida ya usafiri ndo upande gari la mtu usiye mfahamu kweli..!!!
Isitoshe alishapanda zake daladala shida iko wapi mpaka unakubali kushuka kwa lift ya stranger jamani...!!!
Ananunua kinywaji unajifanya kukataa then unakunywa... Mtu haumfahamu aaagh!!
Yaan huyo dada haogopi kufanyiwa unyama kisa mtu ana gari loh...
 
Ni ujinga kwa hapa Dar kung'ang'ania lifti usizozijua, afadhali kama mko zaidi ya mmoja. Pia ni vyema ukaangalia na mazingira ujiridhishe mwenyewe if it is safe.

Juzi kati mwezi august nilisafiri mikoani na nilienda na usafiri wangu. Sasa kuna siku nikawa naendesha gari mida ya jioni kama saa kumi naenda sehemu fulani. Nikiwa alone sikuwa na plan ya kupakia abiria, lakini kwa kuwa ni vijijini sikuogopa sana kivile. Nikafika sehemu mama mmoja akanisimamisha nikakubali kumpakia. Nikaenda mbele kidogo, kuna sista mmoja wa kanisa la Katoliki akanisimamisha nikampakia japo nikamwambia nina mizigo mingi sikuwa na plan ya kupakia abiria, ila kwa shida ya usafiri najikaza tu. Basi mbele tena nikasimamishwa, walikuwa wanaume wawili na dada mmoja. Nikasema nafasi haitoshi nina mizigo, wakang'ang'ania nikakubali kumbeba mdada. Tulipoondoka basi wakaanza story, wa kwanza akasema aliogopa hata kusimamisha gari maana aliona niko peke yangu na hanifahamu, sista naye akaunga mkono kuwa aliogopa lakini alijipa moyo tuu maana hakuwa na namna.

Nikawaambia jamani sasa niko peke yangu ningepata wapi mwingine wa kusafiri naye wakati nimekuja peke yangu? In short tulienjoy safari, na mwishoni hawakuamini macho yao hata nauli sikuwatoza japo walikuwa tayari kunipa. Tukaishia kufahamiana.

Its very risky, ni wachache wenye hofu ya Mungu
 
yupo mmoja alipakiwa sinza akakutwa gongo la mboto .yeye alipuliziwa madawa ya kulevya .wakamnyanganya simu hela na kumla front door na back door
 
Miaka hii bado watu wanapanda lifti??? Huna hela ya bodaboda heri kutembea

Miaka hii bado unanunuliwa kitu cha kutia mdomoni na stranger unakula?????

Anyway pole yake

Binadamu wamekuwa wanyama sana siku hizi muwe makini
Nami nimeshangazwa na jambo hili!
 
Wangembaka tu,maana akili hizi hazitakiwi hasa wakati huu tukielekea uchaguzi.

Wewe mdada unapandaje gari hovyo hovyo tu usawa huu!!!!!????

Na mimi ipo siku...napenda sana lifti sijui kwa nini
 
Chonde chonde shogangu.......kuna kunyonyesha kobe...........oooh, God forbid.........

Hahaha, umenikumbusha story ya kuchonga ya huko njiro chuga kunyonyesha Kobe! Hivi hii kitu ilitokeaga kweli?

Anyway, pole zangu kwa huyo dada na madhila yaliyompata, iwe tahadhari kwa wengine.
 
Ashukuru Mungu hawakumtenda vibaya. Hivyo Vitu vingine vitatafutwa tu cha muhimu ni uhai
 
Hahaha, umenikumbusha story ya kuchonga ya huko njiro chuga kunyonyesha Kobe! Hivi hii kitu ilitokeaga kweli?

Anyway, pole zangu kwa huyo dada na madhila yaliyompata, iwe tahadhari kwa wengine.

ile story ilikuwa kweli...........japo sikuona.......ila mmmmh........bora niendelee kupanda Toyo.........
 
ile story ilikuwa kweli...........japo sikuona.......ila mmmmh........bora niendelee kupanda Toyo.........

Ooh sawa, ilikuwa kweli...ila hukuona! Ile ilikuwa zuga tu ili kero za kuomba lifti zipungue! Si unajua lift zina kero sometimes.
 
Ooh sawa, ilikuwa kweli...ila hukuona! Ile ilikuwa zuga tu ili kero za kuomba lifti zipungue! Si unajua lift zina kero sometimes.

Watu ni wabishi..........ila la muhimu ni kutumia formula ya........kutokupanda au kumpa lift mtu usiemjua..........kwa karne hii.........ni ulofa mkubwa..........
 
Watu ni wabishi..........ila la muhimu ni kutumia formula ya........kutokupanda au kumpa lift mtu usiemjua..........kwa karne hii.........ni ulofa mkubwa..........

Kweli, manake unaweza kutoa lift na ukalizwa wewe pia kwa ukarimu wa kutoa lift kwa usiemfahamu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom