Kisa cha Abunuasi na nguo ya Sultan isiyonekana kwa wenye dhambi

Zakaria Lang'o

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
2,593
2,767
Wakongwe wa hadithi naomba niwakumbushe juu ya kisa hiki cha kale. Najua kimesimuliwa sana, ila nafikiri si vibaya nikiwasimulia tena.

Siku moja Abunuasi alienda kwa Sultan. Katika mazungumzo akamweleza Sultan jinsi yeye Abunuasi alivyokuwa fundi hodari wa kushona nguo za kila aina. Akamwambia Sultan kwamba alikuwa anapendekeza amshonee vazi maalum ambalo linaonekana tu na wale wasiokuwa waovu. Yaani wasio na dhambi. Sultan akakubali kwa kuwa ni jambo jema tena la fahari. Hivyo Abunuasi akapata contract ya pesa nono. Kazi ikaanza.

Ilipita miezi kadhaa, Sultan akamtuma Waziri akamuulize Abunuasi juu ya maendeleo ya kazi. Waziri akafika na kumkuta Abunuasi yuko busy kazini, huku akiizungusha cherehani kwa bidi, jasho likimtoka. Waziri akamuuliza juu ya maendeleo ya mashono ya vazi la mfalme. Abunuasi akamjibu kwamba si aliona jinsi vazi lilivyokuwa likipita kwenye cherehani na Uzi ukiunganisha kila sehemu kwa umaridadi!!? Waziri alijaribu kutazama bila kuona kitu, lakini ili asionekane mwovu mbele ya Sultan, aliwakilisha ujumbe kwamba kazi ilikuwa ikiendelea vizuri, na kuwa ingekamilika hivi karibuni.

Sultan alifurahi na baada ya miezi kadhaa alimtuma Waziri Mkuu aende kiwandani kwa Abunuasi ili kufahamu maendeleo ya ushonaji wa vazi lisiloweza kuonwa na mtu mwovu au mwenye husuda yeyote. Waziri Mkuu alfika kwa Abunuasi na Kama kawaida alimkuta akiwa anatokwa jasho kwa kazi nzito ya kushona vazi la Sultan. Waziri Mkuu alijaribu kuangalia kwa makini ili aone hicho alichokuwa akishona Abunuasi, hakukiona kitu. Naye akamrudia mfalme na kumwambia kuwa vazi lilikuwa limekamilika, hivyo ipigwe mbiu ili kutangaza siku rasmi ambayo Sultan atalivaa vazi lake maalum na kupita katika njia kuu huku akishangiliwa na raia wake.

Hatimaye siku ikafika, Abunuasi akalileta vazi kwa Sultan. Sultan akajaribu kutazama lakini hakuliona vazi, ila kwa hofu ya kufikiriwa uovu, akamruhusu Abunuasi amvalishe vazi jipya maalum ili aende barabarani akiwa pia amepanda gari jipya la Kisultan apate kushangiliwa na Wananchi.

Kila alipopita Sultan watu walimwona akiwa hana nguo, lakini hakuna aliyethubutu kusema ili asionekane mdhambi mwenye husuda kwa mfalme. Viongozi wote kuanzia Waziri Mkuu, Mawaziri, Magavana hadi watu wa kawaida walimshangilia Sultan kwa nguvu hadi pale mtoto mdogo aliyekuwa amebebwa begani alipomwambia baba yake kwa sauti ya juu: "Baba mbona mfalme yuko uchi leo?"

Kwa nasibu mfalme alisikia sauti ya mtoto yule, kwani gari ilikuwa ikipita karibu. Ndipo Sultan kwa haraka akachutama garini na kumwamuru Dereva kukimbiza gari haraka na kurejea katika kasri la kifalme.

Iliaminiwa katika nchi ile kuwa mtoto mdogo hana dhambi kwa sababu hajaweza kutenda kosa. Je, yu wapi mtoto mdogo leo atakayepiga kelele kumwambia Sultan kuwa yu uchi, akasikilizwa?
 
mtoto tayari ameishamwambia baba yake kuwa mfalme yupo uchi, ila mfalme kaziba masikio
 
Back
Top Bottom