Kipindi: Malumbano ya hoja (ITV); kitadumu

POMPO

JF-Expert Member
Mar 12, 2011
6,690
2,400
kituo cha Television cha ITV kimerudisha kipindi maalum cha "malumbano ya hoja" kipindi naweza kusema kipya tofauti na kile cha zamani 1990s, kuna tofauti kubwa . anyway.... Hoja ya leo ni kuwa UMASIKINI TANZANIA NI LAANA?
nimefurahia kipindi hiki , mosi kuwa LIVE pia wachangiaji.

my take: wana JF tutumia pia hilo " Jukwaa" la malumbano ya hoja on ITV kama mtu anapata Time better to be there ...... Aluta cont`
 
Nàngalia na nimefurahia Greyson nyakarungu alivyonyoosha habari,pamoja na mwanaharkati mwingine dada ambaye sikumkariri jina,anaomba walaaniwe viongozi wote waliotufikisha hapa tulipo.

Kuna watu wamechomekwa na ccm na unaona live hoja zao za kiupaupande eti wanasiasa wanawafundisha vijana kulalamika na kila mtanzania ajiwezeshe kwanza badala ya kukaa na kulalamika bila kutumia opporunities zilizopo.
 
nimefurai kusikia hii habari.plz mkuu endelea kutupa updates cz wengine tupo nje ya nchi
 
Hakika kipindi ni chenyewe na ina wapiganaji wenye uchu. Lakini kuna yule Profesa Wangwe kwa mtazamo wangu wa haraka mi naona ndiyo wale wale Mapapa ila anajaribu kuficha makucha. Wadau nimetoa hoja tu.
 
...mfumo uliopo haumwezeshi mtanzania kutumia opportunities zilizopo. unawaneemesha zaidi wageni na kuwafanya watanzania watumwa kwenye nchi yao.
 
Hakika kipindi ni chenyewe na ina wapiganaji wenye uchu. Lakini kuna yule Profesa Wangwe kwa mtazamo wangu wa haraka mi naona ndiyo wale wale Mapapa ila anajaribu kuficha makucha. Wadau nimetoa hoja tu.

umemshtukia eeeh! Anadai umaskini umepungua! dah!
 
Asante kwa taarifa,watu wanataka mabadiliko maaana tumechoshwa
 
vijana watafanya nini wakati serikali awna police nzuri za kuwawezesha?wengi wa watanzania ni maskini,elimu ni duni,ajira hakuna,umeme ndo huo mgao,miundo mbinu ni mibovu kiasi ambacho mtu akilima,mazao yanaozea mashambani,inflation ni kubwa. wanasema kilimo kwanza wakati viongozi wanakula fedha za pembejeo za wakulima na kibaya zaidi wanaiba pesa na kuzificha kwenye mabenki ya nje.
 
Hongera Grayson kwa mchango uliotoa,Nimefurahishwa sana na mchango wa Dr.Lwaitama na dogo mmoja wa Udsm.Pia Prof.wangwe amehitimisha vizuri.

Fatma Almasi
na deo rweyunga wameendesha mjadala vizuri
 
dah!ebanaa eh!!!!!! wadau nimekimiss yaani av struggled nikiwahi but kazi na majukumu yalinizuia............ marudio ni lini? date na tym plz..
 
vijana watafanya nini wakati serikali awna police nzuri za kuwawezesha?wengi wa watanzania ni maskini,elimu ni duni,ajira hakuna,umeme ndo huo mgao,miundo mbinu ni mibovu kiasi ambacho mtu akilima,mazao yanaozea mashambani,inflation ni kubwa. wanasema kilimo kwanza wakati viongozi wanakula fedha za pembejeo za wakulima na kibaya zaidi wanaiba pesa na kuzificha kwenye mabenki ya nje.

una maana police askari au policy kama sera?
 
Dada Fatma A. Nyangasa na mwenzako (samahani jina sina) safi sana. Kipindi kina mashiko na kinafaa sana. Na mmeanza vizuri.

1.Jitahidini ku-moderate vyema yaani mkisema sasa tujadili TUFANYE NINI SASA KUONDOA UMASKINI basi muwarejeshe wote wanaochangia hapo ili kutumia muda vizuri na si kurudi tena katika swali la je umaskini ni laana au si laana.

2. Pateni Wanafunzi, Waadhiri mchanganyiko toka vyuo mbalimbali si tu UDSM na kutoka Asasi za Serikali na zisizo za Serikali na katika taaluma mbalimbali mf. Sheria, uchumi, Siasa, Ulinzi, Habari, Kilimo, Uhandisi, Afya, Thiolojia n.k. Hii ina faida kubwa sana kupata michango mingi kutoka mitizamo mbalimbali.

3. Epukeni vichwa vya mada (malumbano) ambavyo ni vyepesi na tayari vina mlalo dhaifu wa sehemu moja (kama yale maswali mengi yenye majibu yanayoeleweka ya kipima joto- ITV), kwa mfano hicho cha umaskini kuuona kama laana, hata hicho kijacho cha suluhu ya muda mfupi kamwe haiwezi kuwa suluhisho la tatizo la nishati TZ . Badala yake mwaweza kuwa na mada nzuri ziletazo migongano ya fikra kama vile :- Tanzania hatupigi hatua za ki-maendeleo kwa sababu tuna shida kubwa zaidi ya kutokuajibika na kimaadili kuliko sababu ya kuwa na katiba au sera au sheria zenye mapungufu. Au nyingine iwe: Ni nini kero kuu za Muungano wetu na nini kifanyike au mada nyingine iwe ni mbinu gani na kwa namna gani tupigane vita dhidi ya rushwa na ufisadi au nyingine iwe Vyombo vya Mawasiliano Tanzania vinasaidia kwa kiwango kikubwa katika kusukuma maendeleo ya jamii n.k

4. Ili kipindi kiwe na manufaa hakikisheni ninyi mods mnabaki na dakika 3 mwishoni kueleza kwa kifupi (summary) yale mazuri ya kusadia jamii yaliyoonekana au kujadiliwa.
 
miminimeona vijana walivyosimama, kama wanauchungu na ka'nchi haka, bila shaka tutafika mbaaali.

hahahaaaa jamaa wa washa taa mchana, anaongea kama mnyika, kwa mifano na anarudi palepale alipokuwa ameachia, looo na huyu nae anagombea bavicha, basi kazi ipo.
well done dogo Greyson, wavute vijana wenzako na ukishinda uwe na umoja na wenzako, na kura zako zisipotosha utoe ushirikiano kwa wenzako.


ila mfano wako wa baba na mtoto umeniacha hoi....naomba unitumie kwenye inbox nimeupenda aisee
 
If we believe poverty is unacceptable to us, and in a civilized society, we would have created apropriate insititutions and policy, to create poverty free country.


But, is there any political committments in poverty eradication?

Is there any leader feels shame from being in a country named poor?


In a well governed country, poverty is something to be ashamed of.


Grayson, 2011.
 
yeah niliangalia nilivutiwa na michango mbalimbali lakini nadhani tuna tatizo kubwa zaidi katika fikra za taifa letu.
 
Nimekikosa!...ila nadhani sio laana,hamna kitu kama hicho,tujiulize kwa mfano watanzania wangapi wanafanya kazi kwa masaa 16 kwa siku?
 
Haya ITV tembeleeni kila kona ya nchi halafu wekeni kwenye kipindi tuchambue kila kona hali ya maisha ya watanzania inakwendaje alafu mumwalike Nape na January waje kuleta sera tofauti za haya magamba waliovaa. Tusisahahu kupita na kuonyesha magari na nyumba za Ridhiwan na mafisadi wengine ili tujue wanaishi vipi.
 
Back
Top Bottom