Kipindi cha midundo ya kale AZAM tv

Kipindi cha midundo ya kale AZAM tv

Bakulutu

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2011
Posts
2,594
Reaction score
1,863
Niwape pongezi azam media kwa hiki kipindi, ni kipindi bora kabisa na cha kuvutia, kina uhalisia kabisa wa mziki hasa wa kitanzania kipindi hicho.
Ni "live band" ya nguvu, ni pongeze UTALII BAND, hii bendi inayo toa burudani kwenye hiki kipindi inaimba nyimbo zile za zamani hasa bendi zetu za nyumbani, ni balaa ina watu wana sauti za akina Rajab Marijani, Mbaraka Mwishe, Remmy Ongala, Malim Ngurumo, Rehan Bitchuka n.k

Kama ulitazama juzi Jumamosi kuna wimbo wa mwisho aliimba Charlez Baba ambao mtangazaji alimsifia sana, alisema uliimbwa na Remmy Ongala na Matimila Band Jina ni YOTE YANA MWISHO nimejaribu kutafuta sana huu wimbo ila hakuna jina la wimbo huo sijui kama kuna anaeufahamu au alikosea jina, mwenye namba ya Charles Baba ani PM tafadhali nikiupata nauleta hapa tu furahia pamoja.
 
Nakifuatilia pia..ni kipindi kizuri..ila cha juzi sikufanikiwa kukiangalia..
 
Tatizo wanajifanya wanaiga kumbe wanaweka play back wangetembelea na ma band mengine tu enjoy
 
Tatizo wanajifanya wanaiga kumbe wanaweka play back wangetembelea na ma band mengine tu enjoy
Unaangalia kipindi kweli jombaa au unasema tuu,? Yaani mtu kama Charlez baba umuwekee playback?[emoji2] Pia sio band moja tuu inakuwepo wanaalika na waimbaji binafsi ila vyombo ni vya utalii.
 
Unaangalia kipindi kweli jombaa au unasema tuu,? Yaani mtu kama Charlez baba umuwekee playback?[emoji2] Pia sio band moja tuu inakuwepo wanaalika na waimbaji binafsi ila vyombo ni vya utalii.
Hivi huwa wanapigia wapi siku nikija huko daslam niwatembelee
 
Midundo ya kali marudio iko live sahivi azam 2
 
Unaangalia kipindi kweli jombaa au unasema tuu,? Yaani mtu kama Charlez baba umuwekee playback?[emoji2] Pia sio band moja tuu inakuwepo wanaalika na waimbaji binafsi ila vyombo ni vya utalii.
PLAY BACK.... hawana lolote wale
 
Asee natizima hapa jingaaa kabisaaa asee kumbe kweli ni playback kabisaaa.. Ovyo ovyo
....Aisee..mi nilijua wanafanyia mazoezi hizo nyimbo...mwee..ngoja nimuulize Adam zuberi tupo group moja la miziki ya zamani la whatssapp..
 
....Aisee..mi nilijua wanafanyia mazoezi hizo nyimbo...mwee..ngoja nimuulize Adam zuberi tupo group moja la miziki ya zamani la whatssapp..
Muulize mkuu uje chap unijulishe tafadhali hata pm tuu mkuu..
 
Back
Top Bottom