Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 234
Kipindi cha mapitio cha magazeti kinachorushwa na kituo cha ITV asubuhi hakina mvuto kabisa na bora kisitishwe kwa ajili ya marekebisho.
Kwanza kabisa magazeti wanayopitia ni machache sana, mengi yakiwa ya IPP Media yenyewe. Isitoshe kuna ubaguzi sana kwani magazeti kama Mwananchi, Citizen na yale ya New Habari Corp hayasomwi kabisa. Hali kadhalika Mwanahalisi siku zote huwa halipitiwi.
Mpitia magazeti Raifred Masakao hana mvuto kabisa -- anaongea sana maneno yasiyokuwa na maana.
Halafu magazeti yanayopitiwa hayaonwi na watazamaji kurasa zake za mbele maana mpitiaji akisha soma vichwa vya habari huliweka pembeni, au hulionyesha kwa mbali ambapo mtazamaji hawezi kusoma vichwa vya habari vingine vilivyopo.
Hii ni tofauti sana na kipindi cha mapitio ya magazeti cha Ch Ten ambapo mpitiaji husoma vichwa vya habari huku ukurasa wote wa mbele unaonyeshwa kwa watazamaji.
Hongera sana Ch Ten kwa kipindi chenu cha mapitio ya magazeti.