safuher
JF-Expert Member
- Feb 11, 2019
- 11,170
- 15,851
Mapenzi ukitaka kuyapima basi angalia tu kuhusu mabaya kama unaweza/anaweza kuyabeba na kuyavumilia.
Asili yetu binadamu tumeumbwa na mambo mazuri na kupenda mazuri,hivyo mtu akikupenda kwa mazuri tu huyo hajakupenda bali ndio asili yake tokea kuumbwa.
Kuna watu wanadhani mfano mwanaume kukupenda basi akusaidie fedha,,akusaidie kazi,akuhurumie,awe mpole na kadhalika.
Hivi sio vipimo sahihi vya mapenzi. Kwa sababu wapo wanaume wanaweza kuwa wanahuruma kwako laikni huruma katoka nayo kwao ndio nature yake. hivyo atakuwa na huruma hata kwa asiyekuwa wewe.
Hivyo huruma yake sio kwa sababu anakupenda wewe,bali huruma yake ni kwa sababu roho yake ndivyo ilivyo hata kabla ya kuwa na wewe.
Wapo wanaume watakuwa wapole lakini upole wake sio kwa sababu kakupenda bali kwa sababu kazaliwa ama kalelewa hivyo.
Hivyo upole wakesio kwa sababu anakupenda bali ni kwa sababu ndio alivyo hata kabla yako,usijione kwamba anafanya kitu cha pekee kwako kumbe hata kwa wengine anafanya hivyo.
Wapo wanaume wanaweza kukusaidia kazi zako za nyumbani n.k,lakini anakusaidia sio kwa sababu anakupenda bali ndo kalelewa ama kakulia hivyo.
Kwa hiyo hapo usiseme kuwa anakuoenda kwa kuona anakufanyia kazi,bali anafanya hizo kazi kwa sababu moyo wake ndo upo hivyo tokea hapo.
Sasa unaweza kukutana na mwanaume ukadhani tabia zake anazofanya anafanya kwa kukupenda kumbe anafanya kwa sababu ndio tabia zake hivyo atamfanyia kila mtu.
Kwahiyo sio sawa kusema kuwa mtu fulani anakupenda kwa kuangalia matendo yake kumbe huyo mtu bwana ndo tabia yake iko hivyo.
Kwa mtu wa aina hii ni ngumu kung'amua kwa vipi anakupenda. Ili ujue kakupenda usiangalie anakufanyia nini. Ili ujue kakupenda angalia anayavumilia vipi mapungufu yako.
Mapungufu ndio msingi wa kuyajua mapenzi.
Karibu kwa mjadala.