Kipimo sahihi cha akili ya binadamu ni nini?

herikipaji

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2016
Posts
1,199
Reaction score
1,378
Salaamu kwenu!

Ninafahamu maana ya akili ni uwezo au weledi wa kutafuta jibu au utatuzi wa tatizo au changamoto.

Sasa je ni nini kipimo sahihi cha akili ya binadamu?

Watu huwa wanatumia kigezo kipi kuhitimisha kuwa "fulani ana akili nyingi sana"?

Nimetafakari sana juu ya kipimo sahihi kinachoweza kutumika na kubaini kwa usahihi akili ya binadamu na sijafanikiwa kupata jibu lake nimeona ni vema niwashirikishe wanajamvi.

Karibuni.
 
Binafsi ni utafakari/ufikiriaji wa mambo hicho ndo naona ni kipimo cha akili
 
Kipimo cha akili ni ule uwezo wa mtu kutafasiri na kuchambua taarifa mbali mbali zinazofikishwa kwenye ubongo kitaaluma yaani Abstract reasoning. Na ili uweze kupata kipimo sahihi cha akili ya mwanadamu unatakiwa umri wa akili ×100 halafu gawanya kwa umri wa kuzaliwa unapata jibu. Umri wa akili hupatikana kwa kukadiria matendo afanyayo mtu.

Kuna mwanasaikolojia Alfred Barnet 1904 alitambulisha nadharia ya namna ya kupima uwezo wa akili ya mwanadamu, kuwa ni kuwaanisha umri wa kuzaliwa wa mtoto na umri wa akili.
 
utaujuaje umri wa akili?? ww binafsi una umri gani wa akili?
 
Rafiki ujaelewa wapi? Nimesema kutambua au utajuaje kuwa una akili chukua umri wako na matendo utajua una una akili kiasi gani. Kwamba IQ(intelligent quotient) is the number that ranges from 0-200+ and ratio that is divided by comparing mental age to chronological age. The intelligence quotient is defined as 100 times the mental age(MA) divided by the chronological age (CA).

Hence IQ =mental age /chronological age ×100. Kwa mfano sasa wewe una miaka 25 nimeona kwenye profile yako, Lakini swali umeuliza kama mtoto mwenye miaka 15, Ili kutambua uwezo wako : 100 × 15 ÷25 fanya hesabu hiyo jibu utakalo Pata ndio uwezo wako kiakili, kumbuka jibu likiwa wastani wa 80-89 upo Chini ya wastani, ikiwa 70-79 una akili duni, ikiwa Chini ya 70 una utindio wa ubongo.
 
Kipimo kizuri cha akili ni pale mtu anapofanya invention na innovation ambazo zinaenda kuiokoa dunia nzima ijayo kama walivyofanya akina Galileo Galile, Sir Issack Newton,faraday,calculus e.t.c!
 
Haaaa! Kumbe kwanzia sasa sitapata tabu kuweza kujua uwezo wa Mtu kufikiria muhimu tu kujua umri wake Kwisha kaz
 
kipimo sahihi cha akili ya mwanadamu ni uwezo wake wa kujua baya na kuliacha pia kujua jema na kulitekeleza.
vilele ni uwezo wake wa kupambana na mazingira aliyomo kuendana na mabadiliko mbalimbali yatokeayo katika jamii ili aweze kufaidika sio kupata hasara
 
Mm nimepata jibu 10
Mkuu si'hatari hiyo au mimi sijaelewa?...ni typing error au nini au umemaanisha 100(Mia) coz jamaa anasema isiwe chini ya 89,yaani hapo ikishuka inakuwa sio dalili nzuri.
Rafiki ujaelewa wapi? Nimesema kutambua au utajuaje kuwa una akili chukua umri wako na matendo utajua una una akili kiasi gani. Kwamba IQ(intelligent quotient) is the number that ranges from 0-200+ and ratio that is divided by comparing mental age to chronological age. The intelligence quotient is defined as 100 times the mental age(MA) divided by the chronological age (CA).

Hence IQ =mental age /chronological age ×100. Kwa mfano sasa wewe una miaka 25 nimeona kwenye profile yako, Lakini swali umeuliza kama mtoto mwenye miaka 15, Ili kutambua uwezo wako : 100 × 15 ÷25 fanya hesabu hiyo jibu utakalo Pata ndio uwezo wako kiakili, kumbuka jibu likiwa wastani wa 80-89 upo Chini ya wastani, ikiwa 70-79 una akili duni, ikiwa Chini ya 70 una utindio wa ubongo.
Huu unaweza kuwa ukweli,nimefuata njia hii naona pana ukweli fulani.
 
Walaah! Hujakosea ni hivyo hivyo nimepata 10 mpaka nimeanza kujiogopa...labda mm ni..........au huyu jamaa aliyetoa hiki kipimo ni muongo maana akili yangu inachapa kaz vzr tu ila ndio 10 sasa
 
Mkuu si'hatari hiyo au mimi sijaelewa?...ni typing error au nini au umemaanisha 100(Mia) coz jamaa anasema isiwe chini ya 89,yaani hapo ikishuka inakuwa sio dalili nzuri.

Huu unaweza kuwa ukweli,nimefuata njia hii naona pana ukweli fulani.
Sio Pana ukweli huo ndio ukweli wenyewe ndugu, ukitaka kujua uwezo wa akili ya mtu Wala usipate tabu tumia njia hiyo nilitoa hapo juu. IQ score higher than 100 means that the person is mentally advanced for the age and has high IQ and IQ less than 100 means just the opposite.
 
Mkuu si'hatari hiyo au mimi sijaelewa?...ni typing error au nini au umemaanisha 100(Mia) coz jamaa anasema isiwe chini ya 89,yaani hapo ikishuka inakuwa sio dalili nzuri.

Huu unaweza kuwa ukweli,nimefuata njia hii naona pana ukweli fulani.
Hapa sio typing error
 
Walaah! Hujakosea ni hivyo hivyo nimepata 10 mpaka nimeanza kujiogopa...labda mm ni..........au huyu jamaa aliyetoa hiki kipimo ni muongo maana akili yangu inachapa kaz vzr tu ila ndio 10 sasa
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] wewe umepigajee hesabu mpaka upate hiyo 10? nahisi umekosea uwezi kupata 10 kumbuka ikiwa Chini ya 70 ina maana wewe ni unakili ndogo sana yaani tahira
 
Labda ngojanirudie ten a.
 
Salaamu kwenu!

Ninafahamu maana ya akili ni uwezo au weledi wa kutafuta jibu au utatuzi wa tatizo au changamoto.
Sasa je ni nini kipimo sahihi cha akili ya binadamu?
Nadhani ulianza na jibu!
Labda unataka kujua kama tafsiri yako hii ni sahihi au la!
ila kama unaamini hivi, then kipimo cha akili lazima kije kuwa ni kutazama matokeo ya weledi na usahihi wa matendo ya mtu ukizingatia umri (rika) na other influences ktk jamii husika, ikiwemo level ya elimu ya muhusika; mila na desturi zao!!
Degree za usahihi ktk kutenda hilo jambo then ndio kitakuwa kipimo cha ubora wa akili ktk task/jambo husika!
 
Back
Top Bottom