Kipimo cha treni ya SGR kwenda kasi ni kuchongoka kwa kichwa chake au mifumo ya ndani ya injini?

Umkonto

JF-Expert Member
Dec 27, 2018
2,102
3,615
Naomba kuuliza; Kipimo cha treni kwenda kasi ni kuchongoka kwa kichwa chake au mifumo ya ndani ya injini?

Nauliza hivyo kwa sababu nimeiona video siwezi kuidownload mkurugenzi wa TRC akisema kuwa tutaendelea kupokea vile vichwa vya mwendo kasi vya kuchongoka!

Kadogosa na yeye ameamua kwendana na wananchi kwa kusema "vichwa vya kuchongoka" kwa sababu huku mtaani tunaelezana kuwa ili treni iende kasi lazima kichwa chake kiwe kimechongoka!

Kwahiyoo, kwa mfano, TRC wakienda kiwandani wakafanya modifikesheni ya bodi la KICHWA BOX na kuweka bodi la KICHWA MCHONGOKO halafu injini ile ile, je spidi itaongezeka kwa sababu ya kuchongoka?
 
Kuchongoka ni muhimu sana ili iende kwa spidi kubwa, angalia mifano ya ndege na sports cars lakini hio sio factor pekee ya kuifanya iende kasi kwa sababu uwezo wake wa injini nao una mchango mkubwa sana. Kwa hiyo ukiweka kichwa mchongoko kwenye injini 'loko' ni Sawa na kujitekenya na kucheka mwenyewe
 
Waweke hata kichwa cha mwendawazimu ili ichangamke na kuongeza spidi
 
Naomba kuuliza; Kipimo cha treni kwenda kasi ni kuchongoka kwa kichwa chake au mifumo ya ndani ya injini?

Nauliza hivyo kwa sababu nimeiona video siwezi kuidownload mkurugenzi wa TRC akisema kuwa tutaendelea kupokea vile vichwa vya mwendo kasi vya kuchongoka!

Kadogosa na yeye ameamua kwendana na wananchi kwa kusema "vichwa vya kuchongoka" kwa sababu huku mtaani tunaelezana kuwa ili treni iende kasi lazima kichwa chake kiwe kimechongoka!

Kwahiyoo, kwa mfano, TRC wakienda kiwandani wakafanya modifikesheni ya bodi la KICHWA BOX na kuweka bodi la KICHWA MCHONGOKO halafu injini ile ile, je spidi itaongezeka kwa sababu ya kuchongoka?
Aerodynamics inataka hivyo.
 
Ukiongea Sayansi hasa kama fizikia inahusika kitu chenye mwendo Kasi lazima kichongoke kurahisisha kufikia spidi ya mwendo husika ,angalia mfano wa ndege, au burret 🚅 ,umbo bapa linakinzana na upepo wakati la mchongoko ulioanzia chini unarahisisha spidi na kufanya chombo king'ng'anie njia !ingawa Kwa spidi ya 160 mpaka 240k/hr umbo la mchongoko halina effect sana spidi kuanzia 400 au 500km/hr umbo la kichongoka lina maana
 
1712696144780.png
 
Back
Top Bottom