Right Marker
Senior Member
- Apr 30, 2018
- 194
- 624
Huku Afrika hata kama unaweza kuzungumza lugha ya kabila lako na lugha 10 za mataifa mbalimbali isipokuwa Kiingereza, Utachekwa. Hata kama unazungumza vizuri Kiswahili, Kihindi, Kiarabu, Kichina, Kithailand, n.k - lakini ukishindwa kuzungumza Kiingereza nchi nzima watakucheka.
Watakucheka kwelikweli! na tena watachimbua CV yako ili wajue umesoma wapi, ulihitimu shule/chuo gani, ulipata daraja gani, na kwanini hujui kuzungumza Kiingereza? Hata kama elimu yako yote ulisoma huko China utachekwa kwanini hujui Kiingereza.
Kipimo cha Msomi wa Afrika ni Kiingereza. Hata kama utaibadili nchi yako kuwa taifa bora kiuchumi kuliko mataifa yote Duniani, bado utaulizwa kwanini hujui Kiingereza. Ukiwa kwenye nafasi ya uongozi hata kama utakuwa fisadi mkubwa lakini kama unajua kuzungumza vizuri kiingereza halafu uweke na vionjo vya vifungu vya sheria, utasifiwa kwelikweli.
RIGHT MARKER
DAR ES SALAAM