Kipima Joto ITV,VAT kwenye miamala:TRA watoa udhuru

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,073
103,291
Kipima Joto kinaendelea usiku huu.Swali ni kuwa Marekebisho mbalimbali ya Kodi na tozo katika bajeti mpya?Kutokana na maswali mengi ya wananchi kukosa majibu toka kwa mtu wa TRA,mtangazaji Jackline Siremi anatoa taarifa kuwa mwalikwa wa TRA hakuweza kuja studio kutokana na ratiba ya zake kuingiliana!Mdau mmoja amepiga simu na kusema kuwa jambo la 18% kwenye mialama limekosa majibu,hata mwakilishi wa TRA akihojiwa Channel 10 alikuwa akijichanganya sana jambo ambalo linatafsirika kuwa wamekimbia kipindi.

Wachambuzi wametia shaka kuwa VAT kwenye miamala haikuwa shirikishi kwa wadau na ndio maana hakuna maelewano!Rais wa mawakala wa forodha anasema TRA imeshindwa kutoa elimu ya kodi.Amelaumu sana watalaam serikalini kutokuwa tayari kupata maoni ya wadau nje ya mfumo wa serikali kutokana na kujiona wanatosha kwa kila kitu!Wachangia wote kwa njia ya simu wamesisitiza kuwa VAT inamlenga mlaji

Wachambuzi wamehitimisha kuwa kwa TRA kukimbia vipindi kama hivi, ambavyo vingetumika kutoa ufafanuzi, inaleta tafsiri mbaya sana kwa wananchi kwamba kuna uwezekano wa TRA imefanya makosa kwenye maamuzi yao. Wamesisitiza rais asikie kilio hiki na TRA wasiogope kutumbuliwa wamuone na rais ili kupata utatuzi wa jambo hili

Aidha wabunge (ambao ni wabunge wa CCM, baada ya ukawa kukatazwa kuongea)wamelaumiwa pia kwa kushindwa kuwawakilisha wananchi ipasavyo na kushindwa kuishauri serikali
 
Shida kubwa sana ya nchi yetu ni mfumo. Haya tunayoyaona yanajadiliwa na kulumbaniwa yalipaswa kujadiliwa na kulumbaniwa BUNGENI na Wabunge na sisi kuletewa final product.

Kwa kuwa Bunge letu sasa limekuwa jumuiya ya CCM, kule bungeni mijadala imekoma badala yake watu wazima wanafunga safari kwenda kuwaombea wananchi wao MINARA YA KUMBUKUMBU ZA PUSH UP huku masuala ya msingi yakikosa mtu wa kuyajadili na yakaishia kuamuliwa kwa NDIOOOOOOOO.

Kodi ni suala la kisheria na sio mahaba. Uchumi wa nchi unaweza kuathiriwa vibaya au vizuri na maamuzi yeyote yale yanayohusu kodi na utekelezaji wake. VAT sio neno geni, tunalifahamu na limetung'ata kwa muda...kuna nini leo hii VAT ianze kuchagizwa kwa kuombewa tafsiri mpya kunusu anguko la maamuzi yaliyofanywa na watunga sera wa upande uliopewa dhamana?

Yaani Bunge sasa ni taasisi ya 'ndio mzee' na hoja ni kusifiasifia kila kitokacho kwa anayepaswa kusimamiwa badala ya kusimamia. Hivi, nyie wabunge wa CCM mnajisikiaje tunapoanza kufanya kazi yenu? Nawasema nyie kwa sababu, ni nyie ndio mliokabidhi 'kiti' kwa serikali, sasa serikali inaongoza bunge na hamna wa kuikosoa kiasi ukosoaji unakuja kufanywa na wananchi baada ya sera kupita.

Nafikiri sasa ndio Watanzania waone nchi hii bila upinzani inafananaje. Haya mambo bwana yalipaswa kujadiliwa bungeni. Hakuna chujio kule sasa tumeletewa juice ya pilipili tuinywe kwa mahaba
 
Aibu! Aibu! Aibu aya mambo ya mwendokasi, yameanza kujidhihilisha na tutegemee ya ovyo meng tu, wabunge wa ndioo... ndioo wametuingza kwenye haya magharama
 
Kwa kifupi mjadala wa leo ni kuongeza hasira na ukakasi katika maamuzi na usimamizi wa kauli za serikali ambazo inaonekana ni ukurupukaji. Kuna madhara makubwa sana kutokea katika siku za usoni katika nchi hiiiiiii.........
 
Kuna mtu amepata kusikia kauli ya Naibu Spika juu ya lawama hizi?hasa ukizingatiwa aliwatibua wabunge TIMAMU
 
Mjadala huu umewapa aibu ya mwaka Wabunge wa CCM waliopitisha sheria hii pasipo kujadili kwa kina na kutafakari wao walipiga makofi tu na kutamka naunga mkono 100%,
Wabunge wa CCM ni shiiida wao hupitisha chochote bila kutafakari na sasa wamedhihilisha kuwa ni vimeo.
 
Mjadala huu umewapa aibu ya mwaka Wabunge wa CCM waliopitisha sheria hii pasipo kujadili kwa kina na kutafakari wao walipiga makofi tu na kutamka naunga mkono 100%,
Waliotia aibu zaidi ni ukawa ambao wametumwa na wananchi wao kwa maagizo ya Lowasa wanatoka nje na kuwaacha wananchi bila ya uwakilishi
 
Nimesikiliza kwa makini kipindi na licha ya kuwa mshabiki wa serikali ya awamu ya tano, lazima nikiri kuwa TRA katika hili wameniangusha.
Wabunge wa CCM kule Dodoma ndiyo walipitisha hayo kama vipofu hawajali shida za wananchi wao wanaangalia matumbo yao tu huku kamati ya mkuchika ikiendesha udikteta kuwazuia upinzani kuweka mambo sawa.
 
Waliotia aibu zaidi ni ukawa ambao wametumwa na wananchi wao kwa maagizo ya Lowasa wanatoka nje na kuwaacha wananchi bila ya uwakilishi
Hata wakibaki bungeni hawapo huru na hawapewi nafasi ya kuchangia lolote wabaki kufanya nini bungeni? Lowasa anahusika nini na wabunge? Umekariri akili za madalali wa siasa wa CCM kila kitu unajua ni lowasa, Tambua kuwa bungeni sasa kuna udikteta mkubwa kuanzia Naibu spika mpaka kamati ya kidikteta ya mkuchika , wabunge wa ukawa hawapewi nafasi ya kuchangia chochote.
 
Maamuzi ya bunge la chama kimoja sasa yanawaua wananchi na njaa, wao wanashiba kwa posho wananchi wanataabika na kodi nyingi ambazo hazijafahamika zinakatajwe.
 
Back
Top Bottom