Kipilimba, Umekubali kuvuliwa nguo?

Hata mimi nimeinusa hiyo
Hapa mimi huwa ndiyo nashindwa kuelewa ''bongo'' zetu watanzania zikoje! Kama rais angetaka kumng'oa huyo mtu angeshindwa nini mpaka azunguke kwa kumtumia Musiba? Ni nani aliyemteua? Ni Musiba? Rais ana uwezo wa kutengua uteuzi wake muda wowote na hawezi kufanya ujinga wa kumtumia Musiba!
 
Hapa mimi huwa ndiyo nashindwa kuelewa ''bongo'' zetu watanzania zikoje! Kama rais angetaka kumng'oa huyo mtu angeshindwa nini mpaka azunguke kwa kumtumia Musiba? Ni nani aliyemteua? Ni Musiba? Rais ana uwezo wa kutengua uteuzi wake muda wowote na hawezi kufanya ujinga wa kumtumia Musiba!
Kwani wewe ubongo wako ukoje mkuu?
 
Leo tena mimi na wewe mzee wangu, usije kudhani nakuchukia baada ya wiki iliyopita kukuandikia makala nyingine. La hasha, ila nakuonea huruma sana. Ni Kama hujui umuhimu na uzito wa kazi ulionao.

Musiba si mjinga wala kichaa kama watu wanavyodhania, bali kuna mtu mwenye nguvu kubwa kuliko wote Tanzania ndo yupo nyuma ya Musiba.

Maneno anayoongea Musiba, hayaongei kwa bahati mbaya au kwa kuhisi, bali ni mkakati maalumu mzito ili kufanikisha jambo maalumu zito.

Bahati mbaya zaidi ofisi yako inadhalilishwa na Musiba, huyu ni mtu Hatari sana ambaye idara yako ilitakiwa kumnyamazisha kimya hata kwa njia zisizojulikana Kwa ajili ya usalama wa nchi.

Musiba amekuwa msiba Kwa watu, hivi hujui athari ya kauli zake na tuhuma zake Kwa watu zinaweza kuchafua usalama wa nchi?

Huyu mtu amefikia hatua ya kuwagusa hadi marais wastaafu. Unadhani ni hali ya kawaida hiyo?

Wewe Kama Mkurugenzi mkuu wa TISS, unajua majukumu yako, hakuna wa kukufundisha kazi, ila hali ilivyo inaonyesha kabisa unafundishwa kazi.

Hivi unajua kuwa vita vya ghuba vilisababishwa na mtu kama Musiba, mkimbizi wa Iraq aliyekuwa akiishi Germany?

Musiba kaumiza wengi, na anaendelea kuwaumiza, na hakuna wa kumgusa huyu mtu, yupo juu ya sheria, a strong man is behind him.

Kwanini TISS imekosa uadilifu mikononi mwako?

Nakushauri u resign ili ulinde heshima yako, vinginevyo utaendelea kuvuliwa nguo.

Nilitarajia ungeiendesha Idara kwa muundo wa CIA, MI6 au Mossad, haya mashirika yapo Kwa maslahi ya mataifa yao na watu wao, na hayatumiki na wanasiasa uchwara.

Watu wanahangaika kuipasua Tanzania, upo umekaa unawatizama tu.

Kwa hiyo unasubiri kushuhudia Tanzania ikipasuliwa na wakati uwezo wa kuzuia unao? Ni kituko cha karne mtu mmoja tu anayejiita mwanaharakati anafanya lolote atakalo na hakuna wa kumgusa.

Yetu macho, siku mkianza kuvuna mnachopanda msikimbie.

Labda Kitambi chake ambacho sasa kinazidi tu Kuongezeka Kikipungua Akili za Kuiendesha Kiuweledi kabisa TISS ( bila Kuingiliwa au Kushinikizwa na Mpumbavu yoyote yule ) zitamrudia ukichanganya na Malaika wake wanaopatikana kwa wingi katika Kanisa lake mahala fulani hivi Ufukweni Jijini Dar es Salaam na Yeye akiwa ndiyo Mwana Kondoo Mwandamizi hapo.
 
Umesema serikali imzime Musiba kwa njia zisizojulikana kwa usalama wa Taifa halafu unagusia CIA na MI6 kama mifano, don't be ridiculous, ongelea mambo yenu ya third world huku kunakonuka damu za raia chini ya mikono ya dola, sio Marekani,sio UK!

It is against Federal Law, ni kinyume cha sheria, kwa serikali ya Marekani ku assasinate mtu yeyote, raia, foreigner , kiongozi wa nchi nyingine, n.k., unless ametangazwa wazi wazi bungeni au na rais kwamba ni adui mpiganaji, enemy combatant!

Kwa hiyo tafadhali tumia mifano ya kwenu huku Burundi, Tanzania, Uganda, Kenya, Rwanda, Sudan, na kwingine Afrika kuchafu huku kunakovunda damu za wananchi.
Mkuu Marekani imeshiriki ku-assassinate viongozi wengi miaka ile ya 1960 wakati wa vuguvugu la mataifa ya afrika kutafuta uhuru.

Ingilia maslahi ya Marekani moja kwa moja halafu utaona kipi kitakachokukuta. Marekani anadukua maongezi ya simu ya karibu dunia nzima halafu ashindwe kumshughulikia mtu mmoja tu mwenye kujifanya mjuaji!.
 
Hii taasisi kwa sasa imejaza vilaza wa uvccm, hafai tena kuitwa intelligence
Kila mtu mwenye akili Nchi hii anajua kwa sasa Musiba yuko Juu ya Kapilimba, na Kapilimba hawezi kumfanya chochote Musiba, Nchi hii Ina viongozi wawili waandamizi kwa sasa, wa kwanza ni Bashite na wa pili ni Musiba. Huyu Musiba Ana nguvu kubwa, Ana uwezo wa kumzaba hata Waziri mkuu makofi na asiulizwe na yoyote.
 
Kwenye hili hakuna uhusika wa yule aliye pelekwa Tabora na DAB kweli?
Maana DAB amepewa naye mamlaka ya siri yaliyojaa visasi!
Mie nasema huyu DAB ataleta shida sana baada ya kujiona yeye ni NAIBU na kuna watu wanamdharau
Sina hakika sana bali natambua kwamba , wakati wa sakata la makontena , Musiba alikuwa miongoni mwa waliomshambulia Makonda , sijajua kama kuna kolabo yoyote au kila mmoja anacheza kivyake
 
Kwani wewe ubongo wako ukoje mkuu?
Ndiyo maana nauliza ''zijui bongo zetu zikoje''? Vitu vya kutumia mantiki ndogo sana tunashindwa. Hivi mnafikiria rais anaweza kuwa na mkuu wa usalama wa taifa ambaye hamwamini na anamtilia mashaka? Halafu eti akitaka kumwondoa mpaka amtume mtu mwingine aanze kumpiga vijembe ndipo apate kisingizio cha kumwondoa!!!
 
Kupata misosi yote mitatu bado sina uwakika, harafu nije ni comment hapa si ntakuwa najidanganya!!

Bora muda huu nimsaidie Mama watoto kuosha vyombo au kufua Nepi za Mtoto.
Bangi mbaya sana!!
Ona inavyokuathiri
 
Kweli Musiba amewakamata pabaya. Ajabu, hamuendi mahakamani mmeng'ang'ania TISS TISS. Tangu lini TISS ikaenda mahakamani? Kama mnahisi kavunja sheria mmepelekeni mahakamani. Muache kutupigia kelele za chura humu. Igeni mfano wa Sumaye na Membe. Sumaye aliwahi kulishtaki gazeti la Tanganyika Leokwa kumdhalilisha na akashinda. Leo hii Membe yuko mahakamani akidai haki yake. Hao ndio wanajua. Sio ninyi kutwa kucha TISS TISS! Handamaneni basi mwende huko TISS!
Hawajui wafanye nini, wanatapatapa tu.
 
Umesema serikali imzime Musiba kwa njia zisizojulikana kwa usalama wa Taifa halafu unagusia CIA na MI6 kama mifano, don't be ridiculous, ongelea mambo yenu ya third world huku kunakonuka damu za raia chini ya mikono ya dola, sio Marekani,sio UK!

It is against Federal Law, ni kinyume cha sheria, kwa serikali ya Marekani ku assasinate mtu yeyote, raia, foreigner , kiongozi wa nchi nyingine, n.k., unless ametangazwa wazi wazi bungeni au na rais kwamba ni adui mpiganaji, enemy combatant!

Kwa hiyo tafadhali tumia mifano ya kwenu huku Burundi, Tanzania, Uganda, Kenya, Rwanda, Sudan, na kwingine Afrika kuchafu huku kunakovunda damu za wananchi.
Umekurupuka Sana kuchangia mkuu, rudi tena kausome uzi Kwa utulivu utaelewa tu, Halafu assassination character ni tabia ya mashirika yote ya kijasusi Duniani kwa mtu yoyote aliye hatari Kwa usalama wa nchi nadhani hilo hulijui
 
Back
Top Bottom