Kipilimba, Umekubali kuvuliwa nguo?

Kipilimba, Umekubali kuvuliwa nguo?

Leo tena mimi na wewe mzee wangu, usije kudhani nakuchukia baada ya wiki iliyopita kukuandikia makala nyingine. La hasha, ila nakuonea huruma sana. Ni Kama hujui umuhimu na uzito wa kazi ulionao.

Musiba si mjinga wala kichaa kama watu wanavyodhania, bali kuna mtu mwenye nguvu kubwa kuliko wote Tanzania ndo yupo nyuma ya Musiba.

Maneno anayoongea Musiba, hayaongei kwa bahati mbaya au kwa kuhisi, bali ni mkakati maalumu mzito ili kufanikisha jambo maalumu zito.

Bahati mbaya zaidi ofisi yako inadhalilishwa na Musiba, huyu ni mtu Hatari sana ambaye idara yako ilitakiwa kumnyamazisha kimya hata kwa njia zisizojulikana Kwa ajili ya usalama wa nchi.

Musiba amekuwa msiba Kwa watu, hivi hujui athari ya kauli zake na tuhuma zake Kwa watu zinaweza kuchafua usalama wa nchi?

Huyu mtu amefikia hatua ya kuwagusa hadi marais wastaafu. Unadhani ni hali ya kawaida hiyo?

Wewe Kama Mkurugenzi mkuu wa TISS, unajua majukumu yako, hakuna wa kukufundisha kazi, ila hali ilivyo inaonyesha kabisa unafundishwa kazi.

Hivi unajua kuwa vita vya ghuba vilisababishwa na mtu kama Musiba, mkimbizi wa Iraq aliyekuwa akiishi Germany?

Musiba kaumiza wengi, na anaendelea kuwaumiza, na hakuna wa kumgusa huyu mtu, yupo juu ya sheria, a strong man is behind him.

Kwanini TISS imekosa uadilifu mikononi mwako?

Nakushauri u resign ili ulinde heshima yako, vinginevyo utaendelea kuvuliwa nguo.

Nilitarajia ungeiendesha Idara kwa muundo wa CIA, MI6 au Mossad, haya mashirika yapo Kwa maslahi ya mataifa yao na watu wao, na hayatumiki na wanasiasa uchwara.

Watu wanahangaika kuipasua Tanzania, upo umekaa unawatizama tu.

Kwa hiyo unasubiri kushuhudia Tanzania ikipasuliwa na wakati uwezo wa kuzuia unao? Ni kituko cha karne mtu mmoja tu anayejiita mwanaharakati anafanya lolote atakalo na hakuna wa kumgusa.

Yetu macho, siku mkianza kuvuna mnachopanda msikimbie.
Musiba atasababisha vita ya kimbari.Anaeneza chuki kila kukicha
 
TISS huwa hawafanyi kazi kwa shinikizo,kuna watu wabobezi na wa ana akili za kutisha
Kama Musiba ana kuudhi mpeleke mahakamani kama membe alivyofanya
Ilikuwa awamu ya kwanza ndo wenye akili walitumika, awamu zilizo fuata hasa ya sasa hivi, wamejaa wapigaji tu. Hawa wasio juwa utofauti kati ya taifa na serekali inayo ongoza taifa???
 
Musiba anatumika ili Kapilimba ang'olewe
Musiba kikubwa anachofanya ni kuwabomoa wote wanaoonekana kuwa waweza kuwa wagombea uraisi kwa tiketi ya CCM ndio lengo lake kuu. Kuwabomoa wao na wote anaohisi kuwa ni watu wao wa karibu na kubomoa anayohisi Ni mitandao yao. Hao wanaoonekana kuwa waweza kuwa wagombea uraisi ndio lengo na mkakati wake. Kwanini anawalenga hao, sijui ila sidhani Kama ni sahihi.

Kama Kuna mtu kamshauri Musiba atumie strategy hiyo kakosea Sana Tena Sana na end result mwisho wa siku itakuwa Sio nzuri.

Kuna msemo usemao ukiona Kobe kanyamaza kimya ujue anatunga Sheria.
 
Musiba kikubwa anachofanya ni kuwabomoa wote wanaoonekana kuwa waweza kuwa wagombea uraisi kwa tiketi ya CCM ndio lengo lake kuu. Kuwabomoa wao na wote anaohisi kuwa ni watu wao wa karibu na kubomoa anayohisi Ni mitandao yao. Hao wanaoonekana kuwa waweza kuwa wagombea uraisi ndio lengo na mkakati wake. Kwanini anawalenga hao, sijui ila sidhani Kama ni sahihi.

Kama Kuna mtu kamshauri Musiba atumie strategy hiyo kakosea Sana Tena Sana na end results mwisho wa siku itakuwa Sio nzuri.

Kuna msemo usemao ukiona Kobe kanyamaza kimya ujue anatunga Sheria.

Mkuu ni wewe kabisa uliyeandika kitu hiki au umeandikiwa na batu bakongo?.
 
Hivi kumbe Musiba anawasumbua sana vichwa ehee!! Na kama mkiendelea kumfuatilia, kumzungumzia basi atawatesa sana. Dawa ya mpumbavu ni kumpuuza tu.
Tiss kazi yao ni kutafuta habari popote pale, kuzichambua, na kushauri juu ya hatua za kufanya kwa serikali. Hawakamati,hawpigi, wala kufanya ishu yoyote ya action.....
 
Mkuu, fikiri tena sawa sawa ndio uje kuchangia hapa.
 
Musiba anatumika ili Kapilimba ang'olewe
Kwenye hili hakuna uhusika wa yule aliye pelekwa Tabora na DAB kweli?
Maana DAB amepewa naye mamlaka ya siri yaliyojaa visasi!
Mie nasema huyu DAB ataleta shida sana baada ya kujiona yeye ni NAIBU na kuna watu wanamdharau
 
Back
Top Bottom