Kipilimba, Umekubali kuvuliwa nguo?

Kipilimba, Umekubali kuvuliwa nguo?

Hizo taasisi ulizo zitaja mbona huwa zina waondoa watu wengi tu kimya kimya pasipo wao kujulikana. ..umesahau mkasa wa Patrick Lumumba na tuhuma za kuhusika kwa CIA ?
Umesema serikali imzime Musiba kwa njia zisizojulikana kwa usalama wa Taifa halafu unagusia CIA na MI6 kama mifano, don't be ridiculous, ongelea mambo yenu ya third world huku kunakonuka damu za raia chini ya mikono ya dola, sio Marekani,sio UK!

It is against Federal Law, ni kinyume cha sheria, kwa serikali ya Marekani ku assasinate mtu yeyote, raia, foreigner , kiongozi wa nchi nyingine, n.k., unless ametangazwa wazi wazi bungeni au na rais kwamba ni adui mpiganaji, enemy combatant!

Kwa hiyo tafadhali tumia mifano ya kwenu huku Burundi, Tanzania, Uganda, Kenya, Rwanda, Sudan, na kwingine Afrika kuchafu huku kunakovunda damu za wananchi.
 
Asante saana
poleni sana wana ccm kindakindaki.

nasikia hofu, uoga na mtifuano ambao mwenyekiti wenu wa sasa kausababisha ndani ya chama chenu unatisha sana na haujawahi kutokea tangu tz iingie kwenye mfumo wa vyama vingi.

yajayo yanasikitisha.
 
Acha uongo, dunia nzima secret service wana siri nzito za ku eliminate watu bila nyinyi kujua!

Sio kwenye nchi ya demokrasia ya vyama vingi. Senate Intelligence Committee ya Marekani, kwa mfano, ndio ina oversight juu ya CIA, ina siri zote za nchi. Kamati hii Mwenyekiti akiwa Republican makamu lazima awe democrat. Sasa Democrats hawawezi kukubali kuona republicans wanapanga mipango ya kum shuti mbunge wa upinzani nje ya nyumba za bunge halafu wakakaa kimya.

Sasa hapa kwetu bunge halina oversight juu ya Usalama wa Taifa, kwa sababu TISS iko Ikulu. Na kitu chochote kinachowekwa chini ya ofisi ya Rais hakihojiwi popote, kama vile shirika la ndege, bajeti ya Usalama, bajeti ya Ikulu, na yale mahela tunayoona Rais akiwa amesimama juu ya Land Cruiser anainama chini anapasiwa burungutu anagawa.

Siri za nchi hatuzijui. Spika Ndugai amesema alikuwa hajui kwamba Wachina wamepewa nchi Bagamoyo, anatunisha misuli pale mbele kulinda dola kumbe nyeti zote wanamficha masikini, hajui chochote. Mipango ya mauaji inaweza kusukwa bunge lisijue.
 
Umekurupuka Sana kuchangia mkuu, rudi tena kausome uzi Kwa utulivu utaelewa tu, Halafu assassination character ni tabia ya mashirika yote ya kijasusi Duniani kwa mtu yoyote aliye hatari Kwa usalama wa nchi nadhani hilo hulijui
Movie zinakudanganya dogo
 
Ngoma ya 2020 ishaiva na kipenga kimeshapulizwa Lumumba vikumbo wasiwazi...inaonekana kana kwamba watu wanakwenda kukibetua kigoda juu chini...

Wacha tuone dk bado zipo....
 
Ni kweli kabisa mkuu, 2020 ndo mwaka mbaya kuliko miaka yote ya uchaguzi Tanzania.
Hebu vuta hii picha, Mkapa, na Kikwete wanasimama jukwaani ili kumpigia kampeni mgombea Urais wa Upinzani, je? nini kitatokea? Kwa akili ndogo za jiwe anaweza kuamuru wakamatwe au wapigwe shaba, hapo hapo jeshi litachukua nchi na kusimamisha uchaguzi au jeshi litapasuka vipande,team mabeyo, loyal to Mr Stone na team upinzani loyal to wananchi.
Hakika TB JOSHUA ni mtumishi wa Mungu, baada ya jiwe kuteuliwa kugombea urais, Mungu alimwonyesha TB JOSHUA hatima mbaya kabisa ya Tanzania.
Ndipo alipokuja na ndege yake Tanzania, akiwa hana viatu miguuni kama ishara ya kuiteka ardhi ya Tanzania ili isimwage Damu.
Aliongea maneno Mazito sana juu ya nchi
Ndoto za abunuwasi
 
Leo tena mimi na wewe mzee wangu, usije kudhani nakuchukia baada ya wiki iliyopita kukuandikia makala nyingine. La hasha, ila nakuonea huruma sana. Ni Kama hujui umuhimu na uzito wa kazi ulionao.

Musiba si mjinga wala kichaa kama watu wanavyodhania, bali kuna mtu mwenye nguvu kubwa kuliko wote Tanzania ndo yupo nyuma ya Musiba.

Maneno anayoongea Musiba, hayaongei kwa bahati mbaya au kwa kuhisi, bali ni mkakati maalumu mzito ili kufanikisha jambo maalumu zito.

Bahati mbaya zaidi ofisi yako inadhalilishwa na Musiba, huyu ni mtu Hatari sana ambaye idara yako ilitakiwa kumnyamazisha kimya hata kwa njia zisizojulikana Kwa ajili ya usalama wa nchi.

Musiba amekuwa msiba Kwa watu, hivi hujui athari ya kauli zake na tuhuma zake Kwa watu zinaweza kuchafua usalama wa nchi?

Huyu mtu amefikia hatua ya kuwagusa hadi marais wastaafu. Unadhani ni hali ya kawaida hiyo?

Wewe Kama Mkurugenzi mkuu wa TISS, unajua majukumu yako, hakuna wa kukufundisha kazi, ila hali ilivyo inaonyesha kabisa unafundishwa kazi.

Hivi unajua kuwa vita vya ghuba vilisababishwa na mtu kama Musiba, mkimbizi wa Iraq aliyekuwa akiishi Germany?

Musiba kaumiza wengi, na anaendelea kuwaumiza, na hakuna wa kumgusa huyu mtu, yupo juu ya sheria, a strong man is behind him.

Kwanini TISS imekosa uadilifu mikononi mwako?

Nakushauri u resign ili ulinde heshima yako, vinginevyo utaendelea kuvuliwa nguo.

Nilitarajia ungeiendesha Idara kwa muundo wa CIA, MI6 au Mossad, haya mashirika yapo Kwa maslahi ya mataifa yao na watu wao, na hayatumiki na wanasiasa uchwara.

Watu wanahangaika kuipasua Tanzania, upo umekaa unawatizama tu.

Kwa hiyo unasubiri kushuhudia Tanzania ikipasuliwa na wakati uwezo wa kuzuia unao? Ni kituko cha karne mtu mmoja tu anayejiita mwanaharakati anafanya lolote atakalo na hakuna wa kumgusa.

Yetu macho, siku mkianza kuvuna mnachopanda msikimbie.
Hivi unafahamu majukumu ya TISS?? Kama ndiyo, basi tuelimishe nasi.
 
Nyie wazee pambaneni na hali zenu, msimtume mkuu wa taasisi nyeti kiaina kushughulikia hali zenu, pambaneni na Musiba wenyewe!!!
 
Leo tena mimi na wewe mzee wangu, usije kudhani nakuchukia baada ya wiki iliyopita kukuandikia makala nyingine. La hasha, ila nakuonea huruma sana. Ni Kama hujui umuhimu na uzito wa kazi ulionao.

Musiba si mjinga wala kichaa kama watu wanavyodhania, bali kuna mtu mwenye nguvu kubwa kuliko wote Tanzania ndo yupo nyuma ya Musiba.

Maneno anayoongea Musiba, hayaongei kwa bahati mbaya au kwa kuhisi, bali ni mkakati maalumu mzito ili kufanikisha jambo maalumu zito.

Bahati mbaya zaidi ofisi yako inadhalilishwa na Musiba, huyu ni mtu Hatari sana ambaye idara yako ilitakiwa kumnyamazisha kimya hata kwa njia zisizojulikana Kwa ajili ya usalama wa nchi.

Musiba amekuwa msiba Kwa watu, hivi hujui athari ya kauli zake na tuhuma zake Kwa watu zinaweza kuchafua usalama wa nchi?

Huyu mtu amefikia hatua ya kuwagusa hadi marais wastaafu. Unadhani ni hali ya kawaida hiyo?

Wewe Kama Mkurugenzi mkuu wa TISS, unajua majukumu yako, hakuna wa kukufundisha kazi, ila hali ilivyo inaonyesha kabisa unafundishwa kazi.

Hivi unajua kuwa vita vya ghuba vilisababishwa na mtu kama Musiba, mkimbizi wa Iraq aliyekuwa akiishi Germany?

Musiba kaumiza wengi, na anaendelea kuwaumiza, na hakuna wa kumgusa huyu mtu, yupo juu ya sheria, a strong man is behind him.

Kwanini TISS imekosa uadilifu mikononi mwako?

Nakushauri u resign ili ulinde heshima yako, vinginevyo utaendelea kuvuliwa nguo.

Nilitarajia ungeiendesha Idara kwa muundo wa CIA, MI6 au Mossad, haya mashirika yapo Kwa maslahi ya mataifa yao na watu wao, na hayatumiki na wanasiasa uchwara.

Watu wanahangaika kuipasua Tanzania, upo umekaa unawatizama tu.

Kwa hiyo unasubiri kushuhudia Tanzania ikipasuliwa na wakati uwezo wa kuzuia unao? Ni kituko cha karne mtu mmoja tu anayejiita mwanaharakati anafanya lolote atakalo na hakuna wa kumgusa.

Yetu macho, siku mkianza kuvuna mnachopanda msikimbie.
Mkuu umesema Musiba anapata nguvu from the strongest man in goverment,sasa Kipilimba atawezaje tena kum-contain?Nahisi Kipilimba anajua who Musiba is and what he,other stakeholders and the strongman are up to,ndio maana kanyamaza.Don't you think so.
 
Back
Top Bottom