Kipigo cha Dk. Ulimboka chazua balaa tiGO

KUTEKWA, kupigwa na kuteswa kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Chama cha Madaktari nchini, Dk. Steven Ulimboka na hatimaye kufungiwa kwa Gazeti la MwanaHalisi kwa muda usiojulikana, kumeleta kizaazaa katika kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Tanzania Daima Jumatano limebaini.

Habari kutoka ndani ya kampuni hiyo ya simu yenye mtandao mpana nchini, zinasema kuwa zaidi ya wafanyakazi 30 wamefukuzwa kazi na wengine wako kwenye uchunguzi wakituhumiwa kuvujisha mawasilino ya siri ya simu za wateja kwa Gazeti la MwanaHalisi.

Kwa mujibu wa habari hizo, taarifa za mawasiliano za simu zinazodaiwa kuvujishwa na wafanyakazi hao, zilikuwa kati ya Dk. Ulimboka, Afisa Usalama wa Ikulu na watu aliowasiliana nao kabla ya kutekwa.
Rais Jakaya Kikwete amepata kuliambia taifa mara mbili kwa njia ya televisheni, mwishoni mwa Juni na alipozungumza na wahariri wa vyombo vya habari wiki iliyopita, kwamba serikali yake haihusiki kuteka, kutesa na kumtupa daktari huyo porini.

Naye Waziri Mkuu Mizengo Pinda amepata kuliambia Bunge kuwa, serikali yake haihusiki na utekaji, utesaji na kuhoji, “...serikali imteke ili iweje?”

Hivi karibuni serikali ililifungia Gazeti la MwanaHalisi baada ya kuandika habari iliyomtaja ofisa mmoja wa Idara ya Usalama wa Taifa Ikulu (TISS), kuwa ndiye aliyetekeleza mpango wa kumteka, kumpiga na kumtesa hadi kumjeruhi Dk. Ulimboka, ambaye kwa sasa anaendelea na matibabu kwenye hospitali moja nchini Afrika Kusini.

Kwa mujibu wa habari hiyo ambayo serikali inadai kuwa ni ya uchochezi, MwanaHalisi ilianika namba ya simu ya ofisa huyo pamoja na watu wengine wanaodaiwa kuhusika katika tukio hilo linaloendelea kuchunguzwa na kamati maalumu iliyoundwa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI).
Vyanzo vya habari kutoka kwa baadhi ya wafanyakazi waliokumbwa na sekeseke hilo, zinasema kuwa waliofukuzwa wengi ni wafanyakazi wa kitengo cha IT ambao wanadaiwa kuhusika kutoa taarifa za siri ya mawasilino kati ya Dk. Ulimboka na watu wanaoaminika kuwa ni wabaya wake.
Mmoja wa wafanyakazi kutoka Kampuni ya Tigo, aliliambia gazeti hili kuwa mbali na kutuhumiwa kutoa siri kwa Gazeti la MwanaHalisi, wafanyakazi wengine wametimuliwa kwa madai ya kufanya udanganyifu kwenye huduma za Tigo Pesa na kujipatia fedha.

“Kweli watu wengi wamefukuzwa wakituhumiwa kutoa siri kwa Gazeti la MwanaHalisi, lakini wengine walikuwa wakishirikiana na mawakala wa Tigo Pesa kuiibia kampuni.

“Kwa mfano mfanyakazi alikuwa anakubaliana na wakala kumwingizia kiasi kama cha sh milioni moja, lakini anaweza kuingiza hadi sh milioni 1.5 na kati ya hizo sh 500,000 ni mali yake,” alisema mfanyakazi huyo.

Akizungumzia na Tanzania Daima Jumatano, Mhariri Mkuu wa Gazeti la MwanaHalisi, Jabir Idrissa alishangazwa na taarifa za Tigo kuwafukuza wafanyakazi wake kwa sababu ya habari iliyochapishwa na gazeti lake.

“Chanzo chetu cha habari hakikutoka kwa wafanyakazi wa Tigo. Kama wamefukuzwa kwa sababu ya MwanaHalisi, wamewaonea bure. Kama Tigo ndio waliotupa taarifa na zile za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), zilitoka wapi?” alihoji Jabir na kusisitiza wafanyakazi hao wameonewa bure.

Ofisa Uhusiano wa Tigo, Edward Shila, alipohojiwa kuzungumzia tukio hilo, hakukubali wala kukataa madai hayo na kumtaka mwandishi kumtumia maswali kupitia e-mail yake ili aweze kuyatolea majibu kiofisi.

“Kama una maswali naomba uniandikie kupitia e-mail yangu ambayo nakutumia sasa hivi…maana siko tayari kutoa kauli yoyote isiyokuwa ya kiofisi,” alisema.

Naye Omary Matulla ambaye amejitambulisha kuwa ni ofisa wa kitengo cha kumbukumbu katika kampuni hiyo, alikanusha kuwapo kwa taarifa za kufukuzwa wafanyakazi wa kampuni hiyo.
Alisema kuwa kila mfanyakazi ana mipaka ya kufanya kazi katika kampuni hiyo, na pia ni wajibu wa kila mtumishi kutunza siri kubwa.

“MwanaHalisi ana mbinu zake za kupata habari wala haiwezekani kupata habari kupitia kampuni yetu na hata hivyo jambo hilo si rahisi hata kidogo kutokea,” alikanusha Omary.

Dk. Ulimboka alitekwa usiku wa Juni 26, kusukumizwa kwenye gari, kupigwa, kufungwa mikono na miguu, kunyofolewa kucha na kutolewa meno na hatimaye kutupwa katika msitu wa Mabwepande nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Source: Tanzania Daima
 
mwanahalisi ilitoa ushahidi wa uhakika. nitashangaa kama dci hakuwa nao na kama ndivyo anapaswa kuufatilia.

Mkuu DCI Ndio serikali na anafata maagizo unadhani kesi ya ngiri ahukumu nguruwe unadhani kutakuwa na jipya? Majibu walisha yaandaa kabla ya investigation uchunguzi ni funika kombe tuu mkuu
 
Kwa hii Serikali ya kipuuzi mlionayo hapo nyumbani, msitarajie haki kupatikana hivi karibuni. Tuombe Mungu
 
Kwa hii Serikali ya kipuuzi mlionayo hapo nyumbani, msitarajie haki kupatikana hivi karibuni. Tuombe Mungu

wewe ndio mpuuzi uliekimbia nchi halafu kwa sasa unapandikiza chuki kutokea ughaibuni ukijua kuwa wewe huathiriki na matokeo yake.
 
mwanahalisi ilitoa ushahidi wa uhakika. nitashangaa kama dci hakuwa nao na kama ndivyo anapaswa kuufatilia.

ushahidi wa kijinga hata mtoto wa chekechea akienda tume ya uchaguzi au tgo anaupata.hawa waliofukuzwa tunahitaji kusikia wamepelekwa mahakamani
 
tutaacha kutumia tigo, kumbe mawasiliano tunayofanya saa yoyote yanaangukia barabarani!
 
Kwa jinsi wabongo walivyo hii ya Dr Ulimboka nayo itapita hivi hivi taratiibu, maovu mangapi serikali imefanya lakini its just a matter of time inakuja sinema mpya watu wanasahau ya zamani.
Kupigwa na kuteswa kwa Dr Ulimboka ni ktu kiko live bila chenga nani kahusika na Mwanahalisi walimalizia tu msumari wa mwisho kwenye hii stori, TISS hawako makini coz walitumia no zao za kawaida kwa shughuli kama hii na wameumbuka na its possible ni mipango ya Mungu tu ukatokea uzembe kama huu au hawa jamaa si wasomi wa kutosha na wanaojua kupanga na kutekeleza mambo makubwa kama haya, wanojua ipi ni loose end ya kuwakamatisha kirahiisi once wajanja wakiafatilia.
Ingependeza kama Mwanahalisi lingepelekwa mahakamani ili lishtakiwe kwa uchochezi hapo tungejua kweli serikali haihusiki bt kulifungia tuuu hivi hivi aaaaaaah hio hata mtoto angejua ni funika kombe tu coz habari ilioandikwa ukiisoma its just so real wandugu.

Kwanini MwanaHALISI wasiipinge amri hii mahakamani?
 
hivi hoyo ulimboka ana faida gani kwa nchii hii . Lets say angekufa nchi ingepata hasara gani? Ok au sasa awe amepona je nchi itapata faida gani?????? Watanzania tuache mambo yasiyo na faida . Mimi naona ni bora wangemuulia mbali tu huyo ulimboka

Unapoandika kitu, tulia utafakari kwanza, usikurupuke kama mwendawazimu.
 
hivi hoyo ulimboka ana faida gani kwa nchii hii . Lets say angekufa nchi ingepata hasara gani? Ok au sasa awe amepona je nchi itapata faida gani?????? Watanzania tuache mambo yasiyo na faida . Mimi naona ni bora wangemuulia mbali tu huyo ulimboka

Mmh, ndugu....uhai wako na wa Ulimboka wala hauna tofauti. Kwa kutumia kauli hii hii ya kwako, jaribu kuweka jina lako pale ulipoandika Ulimboka, uone panasomekaje.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom