Kipigo cha Dk. Ulimboka chazua balaa tiGO | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kipigo cha Dk. Ulimboka chazua balaa tiGO

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by King Kong III, Aug 8, 2012.

 1. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #1
  Aug 8, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,401
  Trophy Points: 280
  • Wafanyakazi 30 watimuliwa wakidaiwa kutoa mawasiliano ya siri kwa Gazeti la MwanaHalisi


  KUTEKWA, kupigwa na kuteswa kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Chama cha Madaktari nchini, Dk. Steven Ulimboka na hatimaye kufungiwa kwa Gazeti la MwanaHalisi kwa muda usiojulikana, kumeleta kizaazaa katika kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Tanzania Daima Jumatano limebaini.

  Habari kutoka ndani ya kampuni hiyo ya simu yenye mtandao mpana nchini, zinasema kuwa zaidi ya wafanyakazi 30 wamefukuzwa kazi na wengine wako kwenye uchunguzi wakituhumiwa kuvujisha mawasilino ya siri ya simu za wateja kwa Gazeti la MwanaHalisi.

  Kwa mujibu wa habari hizo, taarifa za mawasiliano za simu zinazodaiwa kuvujishwa na wafanyakazi hao, zilikuwa kati ya Dk. Ulimboka, Afisa Usalama wa Ikulu na watu aliowasiliana nao kabla ya kutekwa.

  Rais Jakaya Kikwete amepata kuliambia taifa mara mbili kwa njia ya televisheni, mwishoni mwa Juni na alipozungumza na wahariri wa vyombo vya habari wiki iliyopita, kwamba serikali yake haihusiki kuteka, kutesa na kumtupa daktari huyo porini.

  Naye Waziri Mkuu Mizengo Pinda amepata kuliambia Bunge kuwa, serikali yake haihusiki na utekaji, utesaji na kuhoji, "...serikali imteke ili iweje?"

  Hivi karibuni serikali ililifungia Gazeti la MwanaHalisi baada ya kuandika habari iliyomtaja ofisa mmoja wa Idara ya Usalama wa Taifa Ikulu (TISS), kuwa ndiye aliyetekeleza mpango wa kumteka, kumpiga na kumtesa hadi kumjeruhi Dk. Ulimboka, ambaye kwa sasa anaendelea na matibabu kwenye hospitali moja nchini Afrika Kusini.

  Kwa mujibu wa habari hiyo ambayo serikali inadai kuwa ni ya uchochezi, MwanaHalisi ilianika namba ya simu ya ofisa huyo pamoja na watu wengine wanaodaiwa kuhusika katika tukio hilo linaloendelea kuchunguzwa na kamati maalumu iliyoundwa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI).

  Vyanzo vya habari kutoka kwa baadhi ya wafanyakazi waliokumbwa na sekeseke hilo, zinasema kuwa waliofukuzwa wengi ni wafanyakazi wa kitengo cha IT ambao wanadaiwa kuhusika kutoa taarifa za siri ya mawasilino kati ya Dk. Ulimboka na watu wanaoaminika kuwa ni wabaya wake.

  Mmoja wa wafanyakazi kutoka Kampuni ya Tigo, aliliambia gazeti hili kuwa mbali na kutuhumiwa kutoa siri kwa Gazeti la MwanaHalisi, wafanyakazi wengine wametimuliwa kwa madai ya kufanya udanganyifu kwenye huduma za Tigo Pesa na kujipatia fedha.

  "Kweli watu wengi wamefukuzwa wakituhumiwa kutoa siri kwa Gazeti la MwanaHalisi, lakini wengine walikuwa wakishirikiana na mawakala wa Tigo Pesa kuiibia kampuni.

  "Kwa mfano mfanyakazi alikuwa anakubaliana na wakala kumwingizia kiasi kama cha sh milioni moja, lakini anaweza kuingiza hadi sh milioni 1.5 na kati ya hizo sh 500,000 ni mali yake," alisema mfanyakazi huyo.

  Akizungumzia na Tanzania Daima Jumatano, Mhariri Mkuu wa Gazeti la MwanaHalisi, Jabir Idrissa alishangazwa na taarifa za Tigo kuwafukuza wafanyakazi wake kwa sababu ya habari iliyochapishwa na gazeti lake.

  "Chanzo chetu cha habari hakikutoka kwa wafanyakazi wa Tigo. Kama wamefukuzwa kwa sababu ya MwanaHalisi, wamewaonea bure. Kama Tigo ndio waliotupa taarifa na zile za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), zilitoka wapi?" alihoji Jabir na kusisitiza wafanyakazi hao wameonewa bure.

  Ofisa Uhusiano wa Tigo, Edward Shila, alipohojiwa kuzungumzia tukio hilo, hakukubali wala kukataa madai hayo na kumtaka mwandishi kumtumia maswali kupitia e-mail yake ili aweze kuyatolea majibu kiofisi.

  "Kama una maswali naomba uniandikie kupitia e-mail yangu ambayo nakutumia sasa hivi…maana siko tayari kutoa kauli yoyote isiyokuwa ya kiofisi," alisema.

  Naye Omary Matulla ambaye amejitambulisha kuwa ni ofisa wa kitengo cha kumbukumbu katika kampuni hiyo, alikanusha kuwapo kwa taarifa za kufukuzwa wafanyakazi wa kampuni hiyo.

  Alisema kuwa kila mfanyakazi ana mipaka ya kufanya kazi katika kampuni hiyo, na pia ni wajibu wa kila mtumishi kutunza siri kubwa.

  "MwanaHalisi ana mbinu zake za kupata habari wala haiwezekani kupata habari kupitia kampuni yetu na hata hivyo jambo hilo si rahisi hata kidogo kutokea," alikanusha Omary.

  Dk. Ulimboka alitekwa usiku wa Juni 26, kusukumizwa kwenye gari, kupigwa, kufungwa mikono na miguu, kunyofolewa kucha na kutolewa meno na hatimaye kutupwa katika msitu wa Mabwepande nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

  Tangu kutokea kwa tukio la kutekwa kwa Dk. Ulimboka, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na wanaharakati wa kutetea haki za binadamu, wamekuwa wakiinyoshea kidole serikali kwamba ndiyo iliyohusika.

  Kamanda wa Kanda Maalumu ya Polisi mkoani Dar es Salaam, Suleiman Kova, hivi karibuni alitangaza kumfikisha mahakamani mtu mmoja aliyedai kukiri kuhusika na utekaji wa Dk. Ulimboka.

  Kova aliwaambia waandishi wa habari kuwa, polisi wamekamata mtu aitwaye Joshua Malundi kutoka Kenya ambaye amekiri kumteka na kumtesa Dk. Ulimboka.

  Alidai kuwa mtuhumiwa alikwenda kutubu katika Kanisa la Ufufuo na Uzima, Kawe, Dar es Salaam.

  Lakini hata hivyo, mchungaji wa kanisa hilo, Josephat Gwajima alikana kauli ya Kova juu ya mtuhumiwa huyo, akisema hajakwenda kutubu kwao.


  Source: Tanzania Daima
   
 2. saragossa

  saragossa JF-Expert Member

  #2
  Aug 8, 2012
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 2,141
  Likes Received: 147
  Trophy Points: 160
  Data zipi mkuu! Tiririka!
   
 3. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #3
  Aug 8, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  tiGO ndiyo mtandao sasa
   
 4. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #4
  Aug 8, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  duh! Pole zao
   
 5. TODO

  TODO JF-Expert Member

  #5
  Aug 8, 2012
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 219
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  tiss wameula wa chuya
   
 6. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #6
  Aug 8, 2012
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Kwa hiyo kubenea ana mashahidi 30 kibindoni plus document, Naona mchezo huu sasa ni half time
   
 7. b

  bogota the king Member

  #7
  Aug 8, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 56
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ZOKA na Kova wanahusika na hili!
   
 8. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #8
  Aug 8, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Kwa hiyo baada ya kushindwa kumuua Ulimboka ndo wamehamishia hasira zao huko!?
   
 9. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #9
  Aug 8, 2012
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 760
  Trophy Points: 280
  Tiss au hawa vijana 30 wahitimu wa sosholoji UDSM na agroeconomy SUA? Halafu jitu likimwagiwa tindikali wanasema serikali.
   
 10. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #10
  Aug 8, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Mbona kama wameingilia uhuru wa mahakama?Hii kesi iko mahakamani,haitakiwi kujadiliwa!!!
   
 11. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #11
  Aug 8, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,269
  Likes Received: 22,029
  Trophy Points: 280
  Tigo hawana akili.
   
 12. m

  markj JF-Expert Member

  #12
  Aug 8, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 1,756
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  afadhali wafukuzwe! labda na sisi tutapanta ajira!
   
 13. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #13
  Aug 8, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,401
  Trophy Points: 280
  MwanaHALISI limegundua kabla ya Dk. Ulimboka kutekwa, Rama alianza kufanya mawasiliano naye saa 12: 25 jioni. Mawasiliano hayo yaliendelea 3:29 usiku, saa 4: 52, saa 5: 27, saa 5:40 na mwisho ilikuwa saa 5:52 usiku.

  •MwanaHALISI limegundua kuwa siku mbili kabla ya Dk. Ulimboka kufanyiwa unyama huo (24 Juni 2012), simu ya Rama iliingizwa salio la Sh. 252,849. Hili ni salio kubwa pekee kuingizwa kwenye simu hiyo tangu mwanzo wa mwaka huu.

  Nyaraka zinaonyesha tarehe 4 Mei 2012 simu ya Rama iliwahi kuishiwa salio kabisa hadi kufikia kiwango cha Sh. 1.
   
 14. jobe ayoub

  jobe ayoub JF-Expert Member

  #14
  Aug 8, 2012
  Joined: Jan 30, 2012
  Messages: 206
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  wamelifungia mwanahalisi,
  wanawatimua wafanyakazi-tigo.
  kama wanaubavu watufate na sie tuliosoma mwanahalisi.
  msg have been sent n delivered,wamechelewa.
   
 15. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #15
  Aug 8, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,640
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Too late. Mbona kumeshapambazuka. Huwezi jificha kwenye kivuli cha mti ukijua huonekani.
   
 16. jobe ayoub

  jobe ayoub JF-Expert Member

  #16
  Aug 8, 2012
  Joined: Jan 30, 2012
  Messages: 206
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  we haupo dunia hii,au?
   
 17. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #17
  Aug 8, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,069
  Likes Received: 7,281
  Trophy Points: 280
  Haitasaidia,
  Ukweli tushaujua!!
   
 18. Arushaone

  Arushaone JF-Expert Member

  #18
  Aug 8, 2012
  Joined: Mar 31, 2012
  Messages: 14,351
  Likes Received: 613
  Trophy Points: 280
  mkubwa saragossa ina maana huelewi kuhsu alichoandika saeed kubenea kuhusu jamaa wa tiss na namba zao za tigo? Tafuta data bana. Kwanza hujui nini kisa cha kufungiwa gazeti la mwanahalisi?
   
 19. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #19
  Aug 8, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,703
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Mungu yupo kazini kufichua kila kiovu kilichofichwa, Tayari mass tumeshajua ukweli kuhusu Dr.Ulimboka, hata wafanyaje na kuviolate haki za hao wafanyakazi wa Tigo lakini still ule uovu walioupanda serikali utawarudia wenyewe tu.
   
 20. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #20
  Aug 8, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,640
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Unamaanisha wa format bongo zetu zifute memory?
   
Loading...