Kipi ni hatari zaidi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kipi ni hatari zaidi

Discussion in 'JF Doctor' started by semmy samson, Dec 28, 2010.

 1. semmy samson

  semmy samson Member

  #1
  Dec 28, 2010
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  WASALAAAAM WANA JF WOTE NA POLENI NA SHUGHULI ZA KILA SIKU.

  JAMANI NAOMBENI MSAADA WA KITAALAM, ETI KATI YA SIGARA NA POMBE KIPI KINAMADHARA MAKUBWA ZAIDI KATIKA AFYA YA MTUMIAJI? LONG TERM EFFECTS AND SHORT TERM EFFECTS.  tHE mAN fRoM nO wHeRe
   
 2. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #2
  Dec 28, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Hakuna kilichonafuu. Vyote ni hatari. Achana navyo.
   
 3. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #3
  Dec 28, 2010
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  I think kila kitu, ukitumia kwa uingi ni hatari kwa afya yako. ila kuna vitu vingine, hata ka dose kadogo ni hatari tayari.
  Pombe sio mg=baya kwa afya kama unatumia kidogo (get a definition of pombe kidogo kwa Dr). Ila sigara, hata kidogo ni mbaya tayari. kwanza ile nicotine inaleta addiction, pia ule moshi unaganda ndani ya mapafu na unaweza kusababisha magonjwa mengi ikiwemo cancer.
  Pia dini nyingi zina kataza madawa ya kulevya, na lazma kuna sababu hapo. Kama inawezakana bora zote ziitwe mbaya but if you have to keep one kumbe bora pombe (from a health perspective)
   
 4. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #4
  Dec 28, 2010
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,404
  Likes Received: 3,728
  Trophy Points: 280
  Sigara ni hatari zaidi
   
 5. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #5
  Dec 28, 2010
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,404
  Likes Received: 3,728
  Trophy Points: 280
  Hujaelewa au hutaki kuelewa swali.................. Hivyo viwili havina viwango sawa vya hatari......... kuna kimoja kipo juu,,,,,,,, ambacho ni SIGARA
   
 6. semmy samson

  semmy samson Member

  #6
  Dec 28, 2010
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ninahitaji kujua kinachozidi kingine na sio jibu tofauti ndio maana nikauliza wataalam wa JF.
   
 7. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #7
  Dec 28, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Smoking generally affects a smoker's health, harming nearly every organ of the body, and causing many diseases.


  • heart attacks and stroke
  • gallstones
  • aneurysms
  • leads to less stamina
  • cancer
  • peptic ulcers
  • bronchitis
  • damage a woman's reproductive health
  • accelerates the development of the macular degeneration
   
 8. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #8
  Dec 28, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Alcohol impairs behavior, judgment, memory, concentration and coordination.

  • inflammation
  • neuropsychological deficits
  • brain damage
  • physical behaviour
  • menopause and menstrual irregularities
  • throat cancer
  • affects on the sleep cycle
   
 9. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #9
  Dec 28, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  We tumia tu mwaya hakuna atakaeshi milele:A S crown-1:
   
 10. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #10
  Dec 28, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Ujui kuwa kutumia hivyo vitu ni kujiuwa mapema?

  Ni familia ngapi zimesambaratika kwa sababu ya ulevi...!?

  Watoto wangapi wameachwa yatima, wanawake wangapi wameachwa wajane kwa sababu ya matumizi ya ulevi na uvutaji wa sigara!?
   
 11. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #11
  Dec 28, 2010
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,739
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Hata too much sex ni hatari tu kama ilivyo too much ulabu and fegis. Kila kitu muwe na kiasi!
   
 12. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #12
  Dec 28, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Ulabu na sigara, hata ukitumia kidogo ni hatari kwa afya yako.
   
 13. semmy samson

  semmy samson Member

  #13
  Dec 29, 2010
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  YEEEEEEEEs that is wat i want it, thanx for that but Friend wat persist long among the two.
   
 14. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #14
  Dec 29, 2010
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,404
  Likes Received: 3,728
  Trophy Points: 280
  Ujui kuwa kutumia hivyo vitu ni kujiuwa mapema? ................ Kwa kulinganisha na tarehe ipi ambayo mtu alitakiwa afe.....??

  Ni familia ngapi zimesambaratika kwa sababu ya ulevi...!? .............. Unadhani wasio walevi ndoa zao hazisambaratiki....????

  Watoto wangapi wameachwa yatima, wanawake wangapi wameachwa wajane kwa sababu ya matumizi ya ulevi na uvutaji wa sigara

  .............. Yatima wanatoka kwa wasiovuta na wanaovuta sigara, kwa walevi na wasio walevi
   
 15. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #15
  Dec 29, 2010
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Sigara hatari zaidi

  enjoy alcohol kiasi kwa afya na uchangamfu wa akili
   
 16. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #16
  Dec 29, 2010
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,739
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Fegi ni kweli hazifai. Ila the main carcinogen iliyopo kwenye fegi ni 'tar" ambayo ipo kwenye smoke from any burnt plant materials. sasa fikiria sources zingine za moshi.

  Ulabu kidogo hauna madhara, unless unaungalia from moral and religious point of view. Physiologically, hata kama hupati ulabu moja kwa moja, bado mwili wako una ulabu ndani. Pia misosi kibao kama maandazi na mikate ina contents za ulabu japo kidogo. Science, imeonyesha pia kuwa "wine" ni nzuri kwa moyo wako. Of course, usifakamie saaaana. Kiduchu tu inatosha,
   
 17. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #17
  Dec 29, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ukiweza kabisa acha....especially Sigara
  Uishidwa basi tumia kidogo sana...Pombe! Ila kwanini ushindwe yote yawezekana kwa imani
  Zote Sigara na Pombe zina madhara...Japo sigara ina madhara zaidi!
   
 18. m

  mpweke Member

  #18
  Dec 29, 2010
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 48
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 15
  mbona mnatutisha jamani? Tuacheni wenyewe tuendelee kuburudika si hata mabango yao yanaeleza athari za uvutaji? Sasa si mtuache tufe wenyewe mapema? Alaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaah!
   
 19. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #19
  Dec 29, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Sawa mkuu nimekuelewa...! Vipo vya mapema nina maanisha Life expectancy, ambao ni wastani wa kuishi wa mwanadamu, kulingana na overall quality of life... Baadhi ya vitu vinavyochangia ili kupata wastani wa kuishi kulingana na nchi hadi nchi, kama nilivyo eleza hapo juu ni ubora wa maisha wa mtu mmoja mmoja na kwa ujumla... hapa kuna maradhi na mazingira anayo ishi mtu....!

  Mtanzania wa kawaida anategemea kuishi kwa wastani wa miaka 52.49, Wanaume wanategemewa kuishi wastani wa miaka 50.99 na wanawake ni wastani wa miaka 54.03. Hii ni kwa mujibu wa CIA the-world-factbook.

  Sasa kwa mtu ambaye ni mlevi na mvutaji wa sigara, wastani wake wa kuishi upungua sana ukilinganisha na wastani wa jumla. Ukifariki chini ya wastani huo, ina maanisha kuwa umekufa ukiwa chini ya wastani ulio tarajiwa kuishi. Ukipita umri wa miaka 55+ basi upo juu ya kiwango cha kuishi.

  Idadi ya ndoa zinazo sambaratika kwa sababu ya ulevi ni nyingi sana kulinganisha na wasio walevi...!

  Kwenye ulevi kuna mambo mengi sana yenye kuchangia kuharibika kwa ndoa, mlevi hana haya, hana heshima, hana ustaarabu, na kufanya matendo ya kipuuzi mara nyingi. tunashuhudia kila leo kwa walevi Kutoa maneano machafu kama matusi, walevi wengi ni wagomvi, kuharibu ndoa kwa kukosa kutimiza haki za mke na watoto.

  Lingine kubwa ni kuharibika kwa afya na siha ya mnywaji ulevi...!

  Vifo vinavyotokana na saratani ya mapafu na kansa ya ini ni kubwa sana duniani.

  Walevi na wavutaji sigara wengi wapo hatarini kupata maradhi ya moyo na mapafu (heart attacks, strokes, chronic obstructive pulmonary disease (COPD), emphysema, and cancer (particularly lung cancer, cancers of the larynx and mouth, and pancreatic cancer), pia wapo hatarini kupata kitu kinachiitwa peripheral vascular disease na hypertension. Na matatizo ya Ubongo.

  Wataalam UK wa maradhi mbali mbali wanatufahamisha kuwa ulevi peke yake unasababisha vifo vya watu visivyopungua 33,000 kila mwaka... Hii ni nchi iliyoendelea, na wastani wake wa kuishi ni mkubwa kulinganisha na Tanzania, je vifo kwa Tanzania vifo vinavyo sababishwa na uvutaji na unvyaji wa ulevi ni wa kiwango gani?

  Tunasoma kwenye mafundisho ya dini na imani zetu:

  Wala msijitie kwa mikono yenu katika maangamizo.
  Q 2: 125

  Enyi mlio amini! Bila ya shaka ulevi, na kamari, na kuabudu masanamu, na kupiga ramli, ni uchafu katika kazi ya Shet'ani. Basi jiepusheni navyo, ili mpate kufanikiwa.
  Hakika Shet'ani anataka kutia kati yenu uadui na chuki kwa ulevi na kamari, na akuzuieni kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kusali. Basi je, mmeacha?

  Q5:90-91

  Ole wao waamkao asubuhi na mapema, wapate kufuata kileo; wakishinda sana hata usiku wa manane mpaka mvinyo imewaka kama moto ndani yao!
  Isaiah 5:11

  Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi,
  ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,
  husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.

  Galatians 5:19–21
   
 20. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #20
  Dec 29, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Unaweza kuthibitisha hayo niliyoyakoza?
   
Loading...