Kipi ni hatari zaidi

mbona mnatutisha jamani? Tuacheni wenyewe tuendelee kuburudika si hata mabango yao yanaeleza athari za uvutaji? Sasa si mtuache tufe wenyewe mapema? Alaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaah!
Mkuu soma post namba 1. Hakuna kutishana, ila ni kuelezana ukweli.
 
Sawa mkuu nimekuelewa...! Vipo vya mapema nina maanisha Life expectancy, ambao ni wastani wa kuishi wa mwanadamu, kulingana na overall quality of life... Baadhi ya vitu vinavyochangia ili kupata wastani wa kuishi kulingana na nchi hadi nchi, kama nilivyo eleza hapo juu ni ubora wa maisha wa mtu mmoja mmoja na kwa ujumla... hapa kuna maradhi na mazingira anayo ishi mtu....!

Mtanzania wa kawaida anategemea kuishi kwa wastani wa miaka 52.49, Wanaume wanategemewa kuishi wastani wa miaka 50.99 na wanawake ni wastani wa miaka 54.03. Hii ni kwa mujibu wa CIA the-world-factbook.



Sasa kwa mtu ambaye ni mlevi na mvutaji wa sigara, wastani wake wa kuishi upungua sana ukilinganisha na wastani wa jumla. Ukifariki chini ya wastani huo, ina maanisha kuwa umekufa ukiwa chini ya wastani ulio tarajiwa kuishi. Ukipita umri wa miaka 55+ basi upo juu ya kiwango cha kuishi.

Idadi ya ndoa zinazo sambaratika kwa sababu ya ulevi ni nyingi sana kulinganisha na wasio walevi...!

Kwenye ulevi kuna mambo mengi sana yenye kuchangia kuharibika kwa ndoa, mlevi hana haya, hana heshima, hana ustaarabu, na kufanya matendo ya kipuuzi mara nyingi. tunashuhudia kila leo kwa walevi Kutoa maneano machafu kama matusi, walevi wengi ni wagomvi, kuharibu ndoa kwa kukosa kutimiza haki za mke na watoto.

Lingine kubwa ni kuharibika kwa afya na siha ya mnywaji ulevi...!

Vifo vinavyotokana na saratani ya mapafu na kansa ya ini ni kubwa sana duniani.

Walevi na wavutaji sigara wengi wapo hatarini kupata maradhi ya moyo na mapafu (heart attacks, strokes, chronic obstructive pulmonary disease (COPD), emphysema, and cancer (particularly lung cancer, cancers of the larynx and mouth, and pancreatic cancer), pia wapo hatarini kupata kitu kinachiitwa peripheral vascular disease na hypertension. Na matatizo ya Ubongo.

Wataalam UK wa maradhi mbali mbali wanatufahamisha kuwa ulevi peke yake unasababisha vifo vya watu visivyopungua 33,000 kila mwaka... Hii ni nchi iliyoendelea, na wastani wake wa kuishi ni mkubwa kulinganisha na Tanzania, je vifo kwa Tanzania vifo vinavyo sababishwa na uvutaji na unvyaji wa ulevi ni wa kiwango gani?

Tunasoma kwenye mafundisho ya dini na imani zetu:

Wala msijitie kwa mikono yenu katika maangamizo.
Q 2: 125

Enyi mlio amini! Bila ya shaka ulevi, na kamari, na kuabudu masanamu, na kupiga ramli, ni uchafu katika kazi ya Shet'ani. Basi jiepusheni navyo, ili mpate kufanikiwa.
Hakika Shet'ani anataka kutia kati yenu uadui na chuki kwa ulevi na kamari, na akuzuieni kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kusali. Basi je, mmeacha?

Q5:90-91

Ole wao waamkao asubuhi na mapema, wapate kufuata kileo; wakishinda sana hata usiku wa manane mpaka mvinyo imewaka kama moto ndani yao!
Isaiah 5:11

Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi,
ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,
husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.

Galatians 5:19–21

kaka umegusa nyanja zote kielimu na kiimani kweli kaka upo deep.
Nimekusoma vyema sana........
 
Back
Top Bottom