Kipi kitatokea endapo Tanzania itawekewa vikwazo vya kiuchumi?

Wewe unao ushahidi???? Je ni mwanasiasa gani kashitakiwa bila kufuata sheria? Je ni nani yupo kizuizini bila sheria? Unajua nyie wapinzani ni wajinga na wapumbavu sana. Mnavunja sheria halafu mnataka msamehewe kisa nyie wanasiasa wakati huo huo mgekuwa ninyi ndiyo wenye serikali mgehakikisha mnajidai kutumia hizo sheria kulinda amani. Kwa ufupi wapinzani mmeishiwa nguvu mmeanza kutafuta ufadhili
Hummer the Idiots
 
Baadhi ya huduma za kijamii na miradi mbalimbali itasuasua

Mzunguko wa fedha utapungua na baadhi ya biashara zitadorora na pengine kufa kabisa

Nadhani ifike pahala TUJITEGEMEE WENYEWE NCHI KAMA NCHI NA SIO KUTEGEMEA WAHISANI WENYE MASHARTI MAGUMU
Hata mwanao huwezi mwambia ajitemee ghafla tena bila kujua anaanzaje hilo zoezi. Kujitegemea si kukurupuka tu panata kujipanga kisawasawa. Acheni masikhara tumshauri mkuu arekebishe misimamo yasitufike mabaya
 
Sasa mkuu huoni kwamba kukubali sera za LGBT ni kuiharibia sifa nchi yetu?
 
Yani kwa mfano nini kitasababisha tuwekewe hivyo vikwazo?
Wakuu naomba tujadili hili, maana kama indicator tumeshawashiwa...

Je ni athari gani tutapata kama nchi na kwa mtu mmoja mmoja!

Kutokana na hali tete ya uchumi tuliyonayo je tukianguka kabisa itakuwa rahisi kuinuka??

NB: Mods msiunganishe huu uzi, pengine tutapata hapa namna ya kujiandaa na yajayo na kufunga mkanda!!
 
Mziki wa vikwazo vya uchumi kamuulize iran na russia. Inshort kwa akili fupi za viongozi wetu tukiwekewa ni ndani ya wiki nchi haipo...
 
Acha uwoga wewe bora tufe na njaa kuliko hao wazungu watuamlishe tufirane wenyewe kwa wenyewe
 
Na kingine wakiweka vikwazo vya kuuza na kununua bado itakuwa vilevile

Wakituwekea vikwazo via kiuchumi maana yake itakuwa vigumu kwetu kuuza bidhaa zetu kama vile korosho nchi za nje na pia hata tukiwa na pes za kigeni itakuwa vigumu kununua kutoka nchi za nje!! Tutakuwa kama ROBINSON CRUSOE kisiwani peke yake!! Nadhani Jiwe hajui implications kwa nchi hawa jamaa wakitutenga!!!
 
Penye ukweli hapahitaji ma love. Mbow yupo ndani kwa sababu alikiuka sharti la dhamana, na kosa hilo lipo kisheria na sheria zetu ziko wazi na zinajulikana.
Na kosa la msingi yeye na wenzake walifyatua risasi iliyomuua Akwilina, kiukweli makosa yao yapo kisheria
 
Wakituwekea vikwazo via kiuchumi maana yake itakuwa vigumu kwetu kuuza bidhaa zetu kama vile korosho nchi za nje na pia hata tukiwa na pes za kigeni itakuwa vigumu kununua kutoka nchi za nje!! Tutakuwa kama ROBINSON CRUSOE kisiwani peke yake!! Nadhani Jiwe hajui implications kwa nchi hawa jamaa wakitutenga!!!
hatari sana mkuu
 
wafadhili wa nje inawezekana

Inawezekana kama tutakuwa na mipango inayotumia akili na sio kwenda kununua ndege cash halafu hatujui hata hizo ndege zitatumika kwenye njia gani!!! Kuchukua mikopo ambayo riba yake ni kubwa na kutakiwa kuanza kulipa kabla hata mradi uliowekeza haujaanza kuzalisha ni upunguani wa hali ya juu!!
 
Sasa mkuu huoni kwamba kukubali sera za LGBT ni kuiharibia sifa nchi yetu?
Ukiondoa ushoga mengine wapo sahihi, haya siyo maisha,kutishana kila kuitwapo Leo. AMANI ya nafsi ni bora kuliko fedha. 1978/79, kujifunza. Nyerere alitangaza vita na Idd Amin,nikuambie tulishikamana kwa kiwango cha hali ya juu sana, wote tuliimba wimbo mmoja aliotuanzishia Mpendwa Rais wetu. Watu walitoa mahindi,mchele,Kuku,mbuzi,kondoo,na ng'ombe.Wenye magari walisafirisha vyote hivyo kwa hiari ya moyo tena tulifurahia kutoa na kujitoa. Saa3 usiku kila mtanzania alikaa Katibu na radio 277 kusikiliza kipindi cha majira Rais wetu atatuambia nini! Wana muziki walitunga nyimbo cha kutiana moyo,nguvu na kuhamasishana bila kulazimishwa na kiongozi yeyote. Nyerere hakuwa na lugha za kukera wananchi wake,hakuwa na mabavu. Alitumia muda mwingi kuelimisha uma. Tulikuwa Masikini lakini tulibaki na umoja upendo na mshikamano wa ajabu sana. @ Pascal mayalla kama ulishazaliwa,haya ndiyo ya kuwaelimisha vijana ambao hawakuwepo wakati huo,waache kushabikia hali hii ya mgawanyiko. Viongozi wa sasa wakipita humu wawe na la kujifunza. Wajeshi,Polisi waliheshima kwa kazi zao,hawakutisha kama hivi leo.walifanyakazi kwa weledi lakini walitanguliza upendo. Tuna mengi ya kusema muda hatoshi. Wale wahenga waliomo humu watakubaliana nami. TULIPO SIPO NA TUNAKOENDA SIKO
 
Back
Top Bottom