Kipi kitatokea endapo Tanzania itawekewa vikwazo vya kiuchumi?

Lavit

JF-Expert Member
May 16, 2011
12,959
26,020
Wakuu naomba tujadili hili, maana kama indicator tumeshawashiwa...

Je ni athari gani tutapata kama nchi na kwa mtu mmoja mmoja!

Kutokana na hali tete ya uchumi tuliyonayo je tukianguka kabisa itakuwa rahisi kuinuka??

NB: Mods msiunganishe huu uzi, pengine tutapata hapa namna ya kujiandaa na yajayo na kufunga mkanda!!
 
Bidhaa muhimu zitakuwa adimu. Hii itapelekea kupanda bei pia itabidi kupanga foleni ili kupata baadhi ya mahitaji. Mche wa sabuni utakuwa laki moja, wafanyakaz wa umma mtasubirishwa mishahara kwa miezi kadhaa, na mtaambiwa hutaki kazi acha. Yaani ni kama ambavyo kinatokea Zimbabwe sasa hv. Mugabe hakuwahi safiri kuelekea Ulaya tokea akosane nao.safar zake ilikuwa Asia
 
Zaidi watu wa hali ya chini ndy waaathirika wakubwa ,sababu kipato chao hadi sasa ni mbaya sana haielezeki , watu wamekuwa kama vichaaa mtu unamsikia akiongea peke yake , vijijini ndy usiseme
 
Baadhi ya huduma za kijamii na miradi mbalimbali itasuasua

Mzunguko wa fedha utapungua na baadhi ya biashara zitadorora na pengine kufa kabisa

Nadhani ifike pahala TUJITEGEMEE WENYEWE NCHI KAMA NCHI NA SIO KUTEGEMEA WAHISANI WENYE MASHARTI MAGUMU
 
Wakuu naomba tujadili hili, maana kama indicator tumeshawashiwa...

Je ni athari gani tutapata kama nchi na kwa mtu mmoja mmoja!

Kutokana na hali tete ya uchumi tuliyonayo je tukianguka kabisa itakuwa rahisi kuinuka??

NB: Mods msiunganishe huu uzi, pengine tutapata hapa namna ya kujiandaa na yajayo na kufunga mkanda!!
Tafadhalini sana msituondolee ARV'S , taarifa mpya zinaonyesha kwamba 89% ya viongozi wanaishi kwa nguvu ya hiyo kitu .
 
Baadhi ya huduma za kijamii na miradi mbalimbali itasuasua

Mzunguko wa fedha utapungua na baadhi ya biashara zitadorora na pengine kufa kabisa

Nadhani ifike pahala TUJITEGEMEE WENYEWE NCHI KAMA NCHI NA SIO KUTEGEMEA WAHISANI WENYE MASHARTI MAGUMU
Mkuu kuna utofauti kati ya kunyimwa misaada na vikwazo vya kiuchumi (economic sanctions)...
Sawa tunaweza kujitegemea.. ila hatuwezi kujitosheleza kwa kila kitu... tunahitaji kuuza nje na kununua pia!!
 
Yeah uko sahihi pia... lakini kumbuka misaada hiyo ndio inayotumika kufadhili miradi mbalimbali ya kimaendeleo katika sekta mbalimbali mfano huduma za kijamii..shule..maji..hospitali.. barabara na miundombinu mingine

Na kingine wakiweka vikwazo vya kuuza na kununua bado itakuwa vilevile
 
Baadhi ya huduma za kijamii na miradi mbalimbali itasuasua

Mzunguko wa fedha utapungua na baadhi ya biashara zitadorora na pengine kufa kabisa

Nadhani ifike pahala TUJITEGEMEE WENYEWE NCHI KAMA NCHI NA SIO KUTEGEMEA WAHISANI WENYE MASHARTI MAGUMU
Lini sasa tutaanza kujitegemea mkuuu
 
Aliwekewa vikwazo Nyerere na nchi ilienda, hatuwezi kufuata Amri za mabeberu Kisa vikwazo, we must have our own denstiny this is our land hata kwao hatuwaingilii iweje watuingilie, wanataka kutuvuruga kwakua wanaona tuna Songa mbele bila ya misaada yao ya masharti
 
Baadhi ya huduma za kijamii na miradi mbalimbali itasuasua

Mzunguko wa fedha utapungua na baadhi ya biashara zitadorora na pengine kufa kabisa

Nadhani ifike pahala TUJITEGEMEE WENYEWE NCHI KAMA NCHI NA SIO KUTEGEMEA WAHISANI WENYE MASHARTI MAGUMU
Kujitegemea hakuji kwa kukurupuka,ni lazima mtu ujipange.
Tusiwe kama viongozi wetu kutoa majibu mepesi kwa maswali magumu,vijana wanapolilia ajira,hujibiwa kirahisi tu,nendeni vijijini mkalime...majibu ya kipuuzi kabisa
 
Aliwekewa vikwazo Nyerere na nchi ilienda, hatuwezi kufuata Amri za mabeberu Kisa vikwazo, we must have our own denstiny this is our land hata kwao hatuwaingilii iweje watuingilie, wanataka kutuvuruga kwakua wanaona tuna Songa mbele bila ya misaada yao ya masharti
Mkuu lakini mbona mambo unayosema wanatuingilia ni mambo ya msingi... kwanini haki ya msingi za kiraia zibinywe? Kwanini wapinzani wageuzwe kuwa wahaini?
Hizi sheria za mitandao na takwimu zinalolenga wakosoaji wa serikali peke yake kwako unaona sawa?

Hata wao wasipotuingilia unafikiri tupo kwenye mstari sahihi kuelekea kile kinachoitwa maendeleo?
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom