Vikwazo vya kiuchumi, kisiasa na sayansi na teknolojia [Marekani, umoja wa nchi za Ulaya, Urusi na China]

DENG XIAOPING

JF-Expert Member
Mar 6, 2022
2,398
2,593
Vikwazo vya kiuchumi, kisiasa na Kisayansi na teknolojia [Marekani,Umoja wa nchi za ulaya,Urusi na China]. Awali ya yote ningependa kumshukuru MUNGU kwa huu uzima wa afya alionipatia. ningependa tulejea kichwa cha mada hapo juuu chenye kunena“VIKWAZO VYA KIUCHUMI, KISIASA NA VYA KISAYANSI NA KITEKNOLOJIA [MAREKANI {U.S.A}, UMOJA WA NCHI ZA ULAYA, URUSI NA CHINA]”.

1.Ningependa tujiulize nini maana halisi ya hili neno vikwako(wingi)au Kikwazo(umoja)?

-Kwa tafasiri sahahi ya lugha ya kiswahili Kikwazo au vikwazo ni inamaana ya neno kizuizi au vizuizi

-Kwa maana rahisi Vikwazo vya Kiuchumi(biashara),Kisiasa,Na sayansi na teknolojia kwa nchi ni vizuizi vya kiuchumi, Kisiasa Na sayansi na teknolojia juu ya nchi husika iliyo wekewa vizuiz(vikwazo)hivyo

2.Asili ya Vikwazo dhidi ya Nchi Duniani mbalimbali ilianza lini? na sababu ilikuwa ni nini?

-Asili ya Vikwazo vya nchi mbalimbali Duniani ilianza Karne ya Kumi na tisa[19th Century]

- Na sababu ilikuwa ni kuiepusha Dunia dhidi ya vita mbalimbali ambayo njia kuu ya kuzima vita kwa wakati ule ilikuwa vita inazimwa kwa vita .kwa hiyo njia mbadala iliyoletwa ilikuwa ni kuzima au kuepusha vita ilikuwa ni kupitia vikwazo mbalimbali iwe vya Kiuchumi au Kisiasa au Kisayansi na teknolojia

3 Je historia inatuambia ni nchi ngapi Kubwa au maarufu Duniani zilizowahi kuwekewa vikwazo mbalimbali iwe vya Kiuchumi au vya Kisiasa au vya Kisayansi na teknolojia?

-Mpaka sasa dunia imeshuhudia nchi mbalimbali Duniani kuwekewa vikwazo vikubwa kwa vidogo vya kiuchumi,Kisiasa na vya Kisayansi na teknolojia. Mfano wa nchi maarufu na kubwa ni Japan(toka 1945 kijeshi ), Ujerumani(1919Kijeshi ),Iran(toka1979Kijeshi,Kiuchumi, Kisayansi na teknolojia ), Zimbabwe( toka 2002 kiuchumi ),Korea ya kaskazini (toka miaka ya 1950s Kiuchumi , kijeshi ,Kisayansi na teknolojia), Urusi( Kwa miaka ya karibuni toka2014 Kiuchumi,Kisayansi na teknolojia)China(toka 2020kisiasa( Viongozi)),U.S.A(toka 2020kisiasa(viongozi)).

4.Kwa miezi ya karibuni tumeshuhudia mataifa mbalimbali Duniani yakiwekeana vikwazo Kama njia ya kukomesha vita. nasi nchi nyingine bali ni nchi za umoja wa ulaya na marekani dhidi ya taifa la urusi ilikuweza kuidhibiti operation ya kijeshi ya urusi katika ardhi ya ukraine.Maswali je?
i, Vikwazo vimeweza kuwa njia mbadala za haraka kuidhibiti vita au operation ya kijeshi zisifanyike? Mfano operation ya kijeshi(Vita) Urusi na Ukraine.

ii,Vikwazo vimefaulu au vinaweza kufaulu kudhibiti operation ya kijeshi (Vita)au vimeshindwa kufanya hivo?

iii,Je ni ipi njia ya dhibiti Vita kwa haraka je nj kwa njia ya vikwazo,Vita kwa Vita au kwa njia ya mazungumzo ya Amani?

iv, Je ni taifa lipi linapata maumivu makubwa(madhara) ya vikwako.Mfano vikwazo waliowekeana Marekani ,Umoja wa ulaya dhidi ya Urusi au Vikwazo vya Urusi dhidi ya Umoja wa ulaya na Marekani?

V, Ni kwasababu zipi zinapelekea mataifa ambayo hayapo kwenye vikwazo kuathirika na vikwazo vya mataifa mengi? Mfano Vikwazo vya kiuchumi vya umoja wa ulaya na Marekani dhidi ya Urusi vimeiathiri pia Dunia ya tatu

Vi, Tuangalie uwiano wa kiuchumi,Kiushawishi na Kisayansi na teknolojia Kati marekani na umoja wa ulaya dhidi ya urusi:-
Kiuchumi
-Marekani ni taifa namba moja kiuchumi duniani ,taifa namba mbili kwenye kuuza bidhaa zake nje ya marekani duniani(export)nyuma ya china ,marekani ni taifa tajiri namba mbili duniani nyuma ya china,Bank ya marekani nj Bank namba mbili kubwa duniani nyuma ya benki ya China

- Miongoni mwa mataifa ya Ulaya yenye uchumi mkubwa duniani ni ujerumani ikishika namba nne(4), Uingereza tano(5),Ufaransa sita(6),Italynane(8)

-Taifa la urusi likishika namba Kumi na moja duniani(11).ukiwa taifa nambari moja kwa uuzwaji wa gas Ulaya , taifa linalouza mafuta duniani kwa kiwango kikubwa,taifa linaloongoza kwa uuzwaji wa makaa ya mawe ulaya
Sayansi na teknolojia

-Hapa mataifa ya Umoja wa ulaya na Marekani yametawala kwa kiwango kubwa dhidi ya taifa la urusi licha ya kuwa taifa urusi ni tegemeo kwa mataifa ya Umoja wa ulaya na merakani katika teknolojia ya anga za mbali

- Kwa hizi hoja chache inatuonesha nj kwa Jinsi gani mataifa ya Ulaya yalivyo tegemezi kwa urusi katika upande wa nishati kitu pekee kinachowapa nguvu urusi dhidi ya Vikwazo vya umoja wa ulaya na marekani .tofauti na urusi alivyotegemezi katika nyanja mbalimbali kwa umoja wa ulaya na Marekani kisayansi na teknolojia katika mifumo mbalimbali ya kiuchumi,kifendha n.k

5.Je itakuwa ni rahisi kwa mataifa ya Ulaya na merakani kumewekea china vikwazo vikubwa au vye mfanano na vile alivyowekewa urusi ikitokea china akataka kukiunganisha kisiwa Cha Taiwan na china bara kwa kutumia nguvu ya kijeshi?

6.Na je. vikwazo atavyowekewa china Vita kuwa na athari gani kwa china na faida kwa mataifa yaliyoweka vikwazo?

7.Pia je vikwazo atakavyoweka yeye china dhidi ya marekani na umoja wa ulaya vitakuwakuwa na athari gani kwa mataifa yatakayowekewa vikwazo na je china itapata faida kiasi gani?

8.Na je mataifa ya dunia ya tatu yatakumbwa na athari kiasi gani endapo vikwazo hivyo vikiwekwa na marekani na umoja wa ulaya dhidi ya china. Vile china ataweka dhidi ya marekani na umoja wa ulaya na mataifa rafiki?

9.Mfanano wa kiuchumi wa marekani,na mataifa mbalimbali ya Ulaya dhidi ya china
Kiuchumi
- Marekani ni taifa namba moja kichumi duniani ikifuatiwa na china
SOURCE-IMF.jpg


-China ni taifa namba moja tajiri duniani ikifuatiwa na marekani
graph-1.jpg


-China ikiwa ni taifa namba moja kwa kuuza bidhaa zake nje ya china(export) ikifuatiwa na marekani
Top-Countries-by-Exports-2.jpg


-Sarafu ya marekani(dollar) ikiwa na nguvu kwenye matumizi ya fedha duniani ikifuatiwa sarafu ya ulaya(euro) na ya tatu ikiwa sarafu ya china(Yuan) ya china
rmb-euro-dollar-yes-three-together-big-yes-35504231.jpg


-Uku benki ya China ikiwa ndio benki yenye nguvu duniani ikifuatiwa na benki ya marekani
1236.jpg


-Mfumo wa malipo kifedha bank wa umoja wa ulaya swift dhidi ya mfumo wa China wa malipo ya kifedha bank CIPs

- Mfumo wa kadi ya malipo ya kifedha wa Mataifa ya Ulaya na marekani marekani visa na master card dhidi ya mfumo namba mbili wa kadi ya malipo ya kifedha wa kichina union pay
Sayansi na teknolojia
-Katika sayansi na teknolojia mataifa ya Ulaya na marekani yamekuwa ya kiuchua vikali katika uvumbuzi mbalimbali wa teknolojia mfano.katika teknolojia ya sayansi kupitia urushwaji wa roketi na satellite angani na pia kupitia umiliki wa vituo vya anga ulaya na Marekani wakimiliki(International space station) Uki china akimiliki kituo Cha anga Cha pekee yake licha ya kuwa china alipigwa banned katika international space station iliyopelekea kutengeneza Cha kwake na ushindani katika tafiti mbali mbali za kwenye mwezi ,Mars na sayari zingine mbalimbali
Screenshot_20220502-233214.jpg


-Ushindani wa china na umoja wa ulaya na Marekani katika uvumbuzi wa teknolojia mpya mbalimbali mfano electric car technology ,AI , Internet generation etc
UstNFnoWyiCpBUXgQ_s6iyqgoNhIZe_IxENIiFF5eyw.jpg


- ushindani katika teknolojia ya miundombinu Kati ya china pamoja na marekani na umoja wa ulaya ambapo china anaongoza duniani kote

Nchi zinazoongoza kwa sayansi na teknolojia duniani
Eqw9Uzo6hjGfdbju40_RHscQchAmrgSTxJ-qQ4r5Ywk.jpg


Kiushawishi
-Taifa la marekani na pamoja na Baadhi ya maitafa ya ulaya mfano.uingereza,ufaransa yanaongoza kwa ushawishi katika mataifa mengi duniani ikifuatiwa na taifa la china na tatu ni Urusi

9.Kama ilivokuwa ni rahisi kwa mataifa ya Ulaya kuiwekea vikwazo urusi je itakuwa ni rahisi na kwa haraka mataifa ya Ulaya na marekani kuiwekea vikwazo china?

10.Je mgogoro wa China na Taiwan ukitokea ni njia ya mazungumzo ya amani ndio itayokuwa njia sahihi dhidi ya Vikwazo pamoja na vita?

:Asante kwa leo. Karibu mwenye majibu ya Baadhi ya maswali niliyouliza na mwenye maswali ya nyongeza pia anakaribishwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtu anaweza akajiuliza, why China why not Tanzania. Tunapungukiwa na nini hadi sisi tuwe washangiliaji wa China kwenye majukwaa.

Kwa hiyo huo utajiri wa nchi wanaou-ongelea ni GDP ya nchi ambayo inaweza kuwa kubwa sana huku wananchi wengi wakiwa ni machinga na wachoma mahindi 🌽 tu.

Nafikiri njia nzuri ya kupima utajiri wa nchi inapaswa iwe ni kwa kutumia Social Development Index (SDI) kama kipimo badala ya hizo GDPs.
 
Mtu anaweza akajiuliza, why China why not Tanzania. Tunapungukiwa na nini hadi sisi tuwe washangiliaji wa China kwenye majukwaa.

Kwa hiyo huo utajiri wa nchi wanaou-ongelea ni GDP ya nchi ambayo inaweza kuwa kubwa sana huku wananchi wengi wakiwa ni machinga na wachoma mahindi tu.

Nafikiri njia nzuri ya kupima utajiri wa nchi inapaswa iwe ni kwa kutumia Social Development Index (SDI) kama kipimo badala ya hizo GDPs.
Ndugu kwahiyo kifanyike kipi ili GDP iendane na maisha hali ya wananchi wote kwenye nchi husika?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom