Kipi kikomo cha kusalimia shikamoo?

Kipi kikomo cha kusalimia shikamoo?

Hiyo salaam niliiacha mda sana, nilipopita ujana tu.
 
Nianze kwa kujibu swali la msingi.Shikamoo haina umri wa kuacha,itabaki hivyo kwa mdogo kusema Shikamoo, mkubwa kusema Marahaba. Binafsi,nimekulia utamaduni huu, lugha tunayotumia ni Kiswahili katika familia,mpaka leo sioni siku nitaacha kumwambia mzazi wangu ama wakubwa zangu shikamoo.

Sasa turejee kwenye hoja nyingine,mfano, hiyo ya kusema eti shikamoo ni ukoloni, inaashiria ubwana na utwana. Suala la utamaduni halitazamwi hivi,yule wa utamaduni mwingine anaweza kuona mfanyacho siyo. Lakin nyinyi wahusika msione shida yoyote. Mitazamo hii ndiyo wanayo wazungu dhidi yetu, utasikia tohara kwa mwanamke ni mbaya lakini ushoga ni haki ya binadamu.

Ukitaka kujua hili la salamu ni suala tu la mtazamo wa watu fulani, tazama hii.Baadhi ya makabila kule mashariki kama Korea, ninasikia ni mtu mzima ndiyo humshika kichwa mtoto.Niliambiwa hapa kwetu wamasai pia wanafanya hivi,japo sijathibitisha. Mimi niliezoea kuinama ili kitoto kishike kichwa changu kama salamu nitaona wale wanakosea.

Hiki ni Kiswahili,kina msamiati na utamaduni wake.Baadhi yetu Kiswahili ni lugha pili,hivyo si msamiati wala utamaduni wa Kiswahili tunao.Ndiyo maana vitu hivyo tunaona tofauti.Ukisema shikamoo ni ukoloni,ukashauri salamu hizo za kidini(uislamu na ukristo) sasa umekimbia ukoloni hapo?

Aidha, ni suala la kawaida katika lugha na tamaduni zote kitu fulani kuonekana kimepitwa na wakati.Kamusi sahihi itakwambia kabisa neno hili ni la kale,hakitumiki au limebaki kutumika pale tu.Hivyo, huenda watu tunaona shikamoo imepitwa na wakati, hii ina mashiko zaidi kuliko kusema eti shikamoo ni ukoloni.
 
Kiswahili ni lugha zawa la kiarabu na kibantu,sawa
Ila nihoji upande wa shikamoo huko uarabuni wao huitumia hiyo salamu???
Na huitumia hivohivo tunavyoitumiaga sisi???
Kama Kuna wa kunijibu tuendeleze mjadala
 
Nini asili ya hii salamu? nini maana ya neno "Shikamoo?" tukipata hayo majibu nadhani ndio tutapata conclusion ya kuitumia hii salamu au tusiitumie,haijalishi huyu ni mkubwa au mdogo.
Asili ya Neno Shikamoo Ni Kiingereza(Shakemore) yaani tikisa zaidi na Neno Marahaba Ni Kiarabu(Marahaba) yaani Karibu.
Chimbuko, Kadhia hii ilianza kipindi Cha Mzungu kuingia Mara ya Kwanza hapa Tanganyika huko maeneo ya pwani ya bahari ya Hindi, akamkuta mwarabu, Sasa ikawa mwarabu hajui kimombo Wala Mzungu hajui Kiarabu, ndipo Wakapeana mkono na yule Mzungu akawa anasema " Shakemore" Shakemore" kwa furaha, na Mwarabu nae akawa anasema "Marhaba" Marhaba" ndipo Mswahili (Mzee wetu wa kibantu) alivyorudi kwake akaanzisha Sheria hiyo nyumbani kwake kwamba asubuhi kukicha watu wote mle ndani wamwambie Shikamoo na yeye akawa anajibu Marahaba. Kama ujuavyo kipindi hicho ukanda wa pwani ulikuwa na Maendeleo kuliko sehemu nyingi Tanganyika, ndio hii Mila ikaenea Sana na mpaka mikoa ya Bara Kama Mwanza, Shinyanga n.k. Hivyo imekuwa Kama sehemu ya Mila ya Kitanzania jinsi ya kumuanza Mkubwa kirahisi Ni kusema "Shikamoo". Aidha Haina mwisho Ni pale wewe unapokuwa ndio mkubwa kwa kuzaliwa kuliko wote hapo ulipo.
 
Shikamoo
Asili ya Neno Shikamoo Ni Kiingereza(Shakemore) yaani tikisa zaidi na Neno Marahaba Ni Kiarabu(Marahaba) yaani Karibu.
Chimbuko, Kadhia hii ilianza kipindi Cha Mzungu kuingia Mara ya Kwanza hapa Tanganyika huko maeneo ya pwani ya bahari ya Hindi, akamkuta mwarabu, Sasa ikawa mwarabu hajui kimombo Wala Mzungu hajui Kiarabu, ndipo Wakapeana mkono na yule Mzungu akawa anasema " Shakemore" Shakemore" kwa furaha, na Mwarabu nae akawa anasema "Marhaba" Marhaba" ndipo Mswahili (Mzee wetu wa kibantu) alivyorudi kwake akaanzisha Sheria hiyo nyumbani kwake kwamba asubuhi kukicha watu wote mle ndani wamwambie Shikamoo na yeye akawa anajibu Marahaba. Kama ujuavyo kipindi hicho ukanda wa pwani ulikuwa na Maendeleo kuliko sehemu nyingi Tanganyika, ndio hii Mila ikaenea Sana na mpaka mikoa ya Bara Kama Mwanza, Shinyanga n.k. Hivyo imekuwa Kama sehemu ya Mila ya Kitanzania jinsi ya kumuanza Mkubwa kirahisi Ni kusema "Shikamoo".
 
Asili ya Neno Shikamoo Ni Kiingereza(Shakemore) yaani tikisa zaidi na Neno Marahaba Ni Kiarabu(Marahaba) yaani Karibu.
Chimbuko, Kadhia hii ilianza kipindi Cha Mzungu kuingia Mara ya Kwanza hapa Tanganyika huko maeneo ya pwani ya bahari ya Hindi, akamkuta mwarabu, Sasa ikawa mwarabu hajui kimombo Wala Mzungu hajui Kiarabu, ndipo Wakapeana mkono na yule Mzungu akawa anasema " Shakemore" Shakemore" kwa furaha, na Mwarabu nae akawa anasema "Marhaba" Marhaba" ndipo Mswahili (Mzee wetu wa kibantu) alivyorudi kwake akaanzisha Sheria hiyo nyumbani kwake kwamba asubuhi kukicha watu wote mle ndani wamwambie Shikamoo na yeye akawa anajibu Marahaba. Kama ujuavyo kipindi hicho ukanda wa pwani ulikuwa na Maendeleo kuliko sehemu nyingi Tanganyika, ndio hii Mila ikaenea Sana na mpaka mikoa ya Bara Kama Mwanza, Shinyanga n.k. Hivyo imekuwa Kama sehemu ya Mila ya Kitanzania jinsi ya kumuanza Mkubwa kirahisi Ni kusema "Shikamoo". Aidha Haina mwisho Ni pale wewe unapokuwa ndio mkubwa kwa kuzaliwa kuliko wote hapo ulipo.
Kwani kwa sasa mikoa ya bara inaizidi mikoa ya Pwani kimaendeleo ?
 
Write your reply...hadi hapa nilipofikia nitasalimia wazazi tuu basi

mtu mzima mwengine yeyote hapana hata kumpisha kikongwe au mjamzito akae kwenye siti yangu kwenye dalala sifanyi huo upuuzi teh teh Nina miakili mingi Mimi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom