Kipi kifanyike kwenye kilimo?

Rebeca 83

JF-Expert Member
Jun 4, 2016
14,840
31,583
Hello JF,

Hii ni moja ya kati za threads zangu za mwisho mwisho..LOL

I am trying to cut my time spending browsing JamiiForums.

So far, i am doing great, sijapost chochote in four days..LOL.

Anyway,

Ningependa kujua nini kinachokosekana kwenye Kilimo chetu?

Ili kiwe chenye tija kwa manufaa ya Watanzania?

Tuna depend kwenye Kilimo, yet nahisi hili ni eneo moja ambalo halijawa exploited fully...

Again, tu brainstorm wapi pana tatizo..

Thanks all..
 
Inshu ya kumtafuta mchawi kwenye kilimo chetu me naona ngumu sana, hatuwezi kumpata mchawi wa moja kwa moja. Japo serikali tunaweza kuitupia lawama lakin hata sisi pia wananchi bado hatupo smart kwenye kilimo, wenzetu wakenya wanatupiga bao sana.

Tukipunguza mawenge na kuacha mhemuko wa kutaka utajiri wa shortcut pasipo kuwa na masterplan inayoeleweka, kilimo kitawanufanisha wachache sana.
 
Uko sahihi mkuu,sisi kama wananchi hatuna muamko, inabidi tubadilishe mindset zetu kwanza...kilimo kinaonekana ni cha wachache waliofeli maisha , i guess Kilimo kiwe introduced slowly kwenye curriculum za wanafunzi..by the time wanamaliza shule wanakua na msimamo postive kuhusu kilimo.

Question is; huko shuleni tutawafundisha nini kuhusu kilimo?? mkuu embu tiririrka..lol
 
Uko sahihi mkuu,sisi kama wananchi hatuna muamko, inabidi tubadilishe mindset zetu kwanza...kilimo kinaonekana ni cha wachache waliofeli maisha , i guess Kilimo kiwe introduced slowly kwenye curriculum za wanafunzi..by the time wanamaliza shule wanakua na msimamo postive kuhusu kilimo.....

Question is; huko shuleni tutawafundisha nini kuhusu kilimo?? mkuu embu tiririrka..lol
Ni simpo sana.. kama ni shuleni me naona yale masomo ya ufundi stadi yarudishwe na kutiliwa mkazo pamoja na elimu ya kujitegemea, yani sio tu kilimo pekee bali hata katika nyanja nyingine.

Watoto waelezwe ukweli ajira zao zipo mikononi mwao, so katika kila wanalofanya lazma wawe smart, ujuzi, pamoja na elimu ya kutosha ili kupata matokeo chanya. Hapo angalau sasa lawama ibaki kwa serikali peke yake
 
Ni simpo sana.. kama ni shuleni me naona yale masomo ya ufundi stadi yarudishwe na kutiliwa mkazo pamoja na elimu ya kujitegemea, yani sio tu kilimo pekee bali hata katika nyanja nyingine. Watoto waelezwe ukweli ajira zao zipo mikononi mwao, so katika kila wanalofanya lazma wawe smart, ujuzi, pamoja na elimu ya kutosha ili kupata matokeo chanya. Hapo angalau sasa lawama ibaki kwa serikali peke yake

Asante mkuu kwa ushauri mzuri, ila ningependa specific tubaki kwenye Kilimo, specific nini kifanyike..kama ni shule, kwenye kilimo tufundishe nini?....thanks.
 
Kilimo Tanzania, sekta iliyoajiri raia wengi sana na ina changamoto za kutosha.

1. Pembejeo bora na stahiki
2. Elimu bora ya kilimo bora
3. Uwekezaji kwenye mindset za raia kuhusu kilimo na kilimo biashara
4. Masoko stahiki ya bidhaa za kilimo
5. Uongezaji wa thamani wa bidhaa za kilimo katika kuleta mnyororo wa thamani wenye tija.
6. Siasa na utashi wa wanasiasa katika kuendeleza kilimo
7. Upatikanaji wa mbegu bora za mazao na mifugo
8 . Uwepo wa viwanda vya uchakataji mazao ya kilimo
9. Sera zenye akili timamu
10. Matumizi sahihi ya ardhi kwa kilimo
11. Mahusiano na wadau wa sekta
12.

Ngoja nisinzie kwanza nitaelezea baada ya nane nane
Karibu kwenye siku kuu yetu sie wakulima na wafugaji
 
Asante mkuu kwa ushauri mzuri, ila ningependa specific tubaki kwenye Kilimo, specific nini kifanyike..kama ni shule, kwenye kilimo tufundishe nini?....thanks.
Tanzania vision 2025 imeeleza kilimo, cha makaratasi lakini
 
Mnazunguka mbuyu tu lakini ishu ni masoko tu. Tafuteni masoko ya uhakika watu tunalima sana changamoto inakuwa kwenye masoko. Kukosekana kwa uhakika wa masoko kunafanya tunauza mazao kwa pesa kidogo kiasi cha kufanya faida kidogo sana au wakati mwingine kukosa faida kabisa. Wakati mwingine ninauwezo wa kulima hata ekari hamsini lakini kila ukiliwazia soko unajikuta unalima ekari tano au kumi
 
Hello JF,

Hii ni moja ya kati za threads zangu za mwisho mwisho..LOL

I am trying to cut my time spending browsing JamiiForums...

So far, i am doing great, sijapost chochote in four days..LOL.....

Anyway,

Ningependa kujua nini kinachokosekana kwenye Kilimo chetu???

Ili kiwe chenye tija kwa manufaa ya watanzania....????

Tuna depend kwenye Kilimo, yet nahisi hili ni eneo moja ambalo halijawa exploited fully...

Again, tu brainstorm wapi pana tatizo..

Thanks all..
Becky licha ya Kikwete kuwa dhaifu Ila alijitahidi sana kwenye Ile Sera ya kilimo kwanza tatizo sisi wamatumbi. Jamaa alichoka akaamua kupotezea.

Yani sisi hatuwezi hata tukiwezeshwa.
 
Kilimo Tanzania, sekta iliyoajiri raia wengi sana na ina changamoto za kutosha.

1. Pembejeo bora na stahiki
2. Elimu bora ya kilimo bora
3. Uwekezaji kwenye mindset za raia kuhusu kilimo na kilimo biashara
4. Masoko stahiki ya bidhaa za kilimo
5. Uongezaji wa thamani wa bidhaa za kilimo katika kuleta mnyororo wa thamani wenye tija.
6. Siasa na utashi wa wanasiasa katika kuendeleza kilimo
7. Upatikanaji wa mbegu bora za mazao na mifugo
8 . Uwepo wa viwanda vya uchakataji mazao ya kilimo
9. Sera zenye akili timamu
10. Matumizi sahihi ya ardhi kwa kilimo
11. Mahusiano na wadau wa sekta
12.

Ngoja nisinzie kwanza nitaelezea baada ya nane nane
Karibu kwenye siku kuu yetu sie wakulima na wafugaji

Asante mkuu kwa mchango wako, naomba nijikite number two, Elimu bora ya kilimo inahusu nini specific?

Nimeipenda number tatu nayo,tunahitaji kuwekeza kubadilisha mindset zetu...mimi nahisi kuwe na wider campaigns za mara kwa mara za kilimo,kuwashtua wananchi kuona fursa zinazopatikana kwenye kilimo.
 
Becky licha ya Kikwete kuwa dhaifu Ila alijitahidi sana kwenye Ile Sera ya kilimo kwanza tatizo sisi wamatumbi. Jamaa alichoka akaamua kupotezea.

Yani sisi hatuwezi hata tukiwezeshwa.

Ni kweli mkuu, Kikwete alijitahidi sana... i guess mfumo wa uongozi ubadilishwe kwenye transition, kila kiongozi mpya akija aendeleze miradi iliyoachwa na mwezake aliyepita. hivi hivi, kila Rais atakuja na sera zake zisipoisha katika muda yupo madarakani then zinakufa,sad.
 
Haya Sasa ndiyo mambo ya Kujadili! Sema Sahv watanzania asilimia kubwa akili, mawazo yao wako kwenye mambo ya udaku bongo fleva bongo movie..

Ngoja turudi kwenye uzi Sasa-
Kwanza lazima mtambue kuwa sekta ya kilimo Tanzania inachangia karibia asilimia 29 ktk uchumi wa tanzania
Kuna vikwazo vingi Ambavyo vinarudisha nyuma au kukwamisha sekta ya kilimo Tanzania, mfano uhaba wa pembejeo ambazo hazitoshelezi, mbegu nazo hazina ubora, mbolea napo kizungumkuti, madawa nayo kasheshe...., kingine Kuna changamoto ya masoko
KITU KINGINE NILICHO KIONA KAMA SERIKALI INATAKA NCHI IPIGE HATUA KUBWA KWENYE KILIMO, waje na sekta 1 au 2 Yaani sekta dume
Wahamasishe watu, wakulima kulima sana mazao 1 au 2 kwa kiasi Kikubwa Mf mahindi, mpunga na hayo mazao ndiyo yatiliwe mkwazo snaaa
Huku wengine wakilima mazao mngine kama kawaida
Hapo ndipo kutaonekana na kupata mafanikio

Ova
 
Mnazunguka mbuyu tu lakini ishu ni masoko tu. Tafuteni masoko ya uhakika watu tunalima sana changamoto inakuwa kwenye masoko. Kukosekana kwa uhakika wa masoko kunafanya tunauza mazao kwa pesa kidogo kiasi cha kufanya faida kidogo sana au wakati mwingine kukosa faida kabisa. Wakati mwingine ninauwezo wa kulima hata ekari hamsini lakini kila ukiliwazia soko unajikuta unalima ekari tano au kumi
Masoko utauza nini kama huzalishi?
 
Uko sahihi mkuu,sisi kama wananchi hatuna muamko, inabidi tubadilishe mindset zetu kwanza...kilimo kinaonekana ni cha wachache waliofeli maisha , i guess Kilimo kiwe introduced slowly kwenye curriculum za wanafunzi..by the time wanamaliza shule wanakua na msimamo postive kuhusu kilimo.....

Question is; huko shuleni tutawafundisha nini kuhusu kilimo?? mkuu embu tiririrka..lol
Watanzania wanapenda kitu kinacholipa.

Weka mazingira mazuri ya kilmo halafu uone kama watu hawatalima mpaka ukakimbia.

Mfano halisi ni ni mbaazi,korosho na mihogo.

Baada ya kuchanganya watu walililma sana.

Ila sasa tatizo kubwa ni kwamba CCM haipendi watu watoke kwenye umasikini.

CCM inapenda kumwona kila mtaznia ni fukara wa kutupa ndio maana inapambana kuhakikisha hilolinatokea. Ni kama mashetani vile.

Kuna mazao ambayo tayari yalikuwa yashaonesha mwelekeo wa kumkomboa mkulima ila CCM wametumia nguvu kubwa kuyaua mpaka wakulima wamekata tamaa na hawana matumaini tena.

1. Kahawa ( Wachagga wao wameacha kabisa kulima, Kagera wao wanaolima wanapangiwa bei. Wakitorosha kupeleka Uganda kwenye beui nzuri wanakamatwa ). Kahawa ni hot cake ila wakulima ni hohe hae wa kutupa.

2. Koroshao. ( Hili zao lilikuwa limeanza kuleata matumaini ya kumtoa mkulima kwenye umasikini ila CCM wamepeleka jeshi limepora wakulima korosho zao na hwana matumaini mpaka sasa zaidi yamistori ya siasa tu )

3. Mbaazi ( Hili ni multbillion zao, na wakulima walikuwa wanapata pesa kibao. Kaja Kibwengo ana bifff zake a Kina Manji ambao walikuwa wanunuzi zao limekufa. Yaani utafikiri hili zao halijawahikuwepo hapa nchini )

4. Tumbaku ( Yale yale )

5. Pamba ni yale yale.

Haya kwenye mazo ya chakula na kwenyewe ukilima sehemu ya kuuza utategemea Janasiasa limeamkaje siku hiyo.

Kilimo Tanzania hakina sehemu ya kupumzika.

Very risk kuanzia unapanda, mvua mavuno mpaka soko.
 
Asante mkuu, Mimi nadhani kuiachia serikali iingilie kilimo na kupanga bei za mazao ndio MISTAKE number MOJA, mimi sio mchumi but i guess tuna evidence za kutosha kuwa serikali ikiachiwa kila kitu inafanya blunders,

kwa mfano hili swala la Korosho hakuna aliyefaidika sio serikali wala wakulima,

nadhani kila mtu alime anavyoweza apange bei anayotaka..

. Market ndio ifanye ku determine bei ya zao,

na sio mtu kakaa zake ofisini anakuja kupanga bei.....

mpaka mimi nahisi ni kweli ma CCM ni mashetani,

huwezi uka ignore hussles za mtanzania mwenzako hivi...

.Asante naona umeainisha MAZAO makubwa MATATU ambayo yanaweza kutupa faida kwa ujumla wetu watu wa tanzania,

nayo ni Kahawa, Korosho na Mbaazi,

very good,

kama nilimpata vyema mkuu mrangi tutafute serikali kuhamasisha kulima mazao machache,

ila kuwavuta wakulima wengi kulima hayo mazao machache......

kila mtu mwenye uwezo wa kulima Korosho, au Mbaazi au Kahawa afanye hivyo...

uzuri wake ukisha IDENTIFY nini kinahitajika kwako na una uwezo ku PROVIDE...then maswala mengine yanakua SMOOTH...

SIO KWELI hayo mazao matatu uliyotaja DEMAND yake imewahi kuwa ndogo duniani...

Ni sisi tu hatujaweka mipango endelevu ya kuuza hayo mazao duniani...

Na hatuna mipango endelevu kwa sababu as you put it maCCM yanafaidika na umasikini wa watanzania...

Its high time tuwe na tume huru ya uchaguzi....

.
 
Hello JF,

Hii ni moja ya kati za threads zangu za mwisho mwisho..LOL

I am trying to cut my time spending browsing JamiiForums...

So far, i am doing great, sijapost chochote in four days..LOL.....

Anyway,

Ningependa kujua nini kinachokosekana kwenye Kilimo chetu???

Ili kiwe chenye tija kwa manufaa ya watanzania....????

Tuna depend kwenye Kilimo, yet nahisi hili ni eneo moja ambalo halijawa exploited fully...

Again, tu brainstorm wapi pana tatizo..

Thanks all..
Unreliable Market, Jana nilisikia katika taarifa ya habari ya saa 2 usiku ITV, kuwa wakulima wa kahawa Arusha na Masama juu huko wanalalamika sana kukosekana kwa soko la kahawa

Mwaka huu huu mwezi wa 6, wakulima wa nyanya walikuwa wanamwaga nyanya jalalani na huku wakiwa na stock kubwa ya nyanya tatizo lilikuwa pia ukosefu wa soko.

Changamoto nyingine ni ukosefu wa Viwanda na dawa za kuhifadhia (Food processing industries &Preservatives) kwa mfano matunda yatokayo Tanga kuna kipindi yanaozea shambani au sokoni wakati yangetengenezewa juices zingeweza kuwa exported na kuingiza kipato kikubwa

Ukosefu wa pembejeo ni tatizo pia lakini tatizo la SOKO LA UHAKIKA ni serious zaidi.
 
Taasisi za kifedha pia zimegoma kuwa rafiki wa mkulima, mkulima hakopesheki akikopesheka basi kwa masharti lukuki, sector za kifedha zimulike fursa zilizopo ktk kilimo ili kuwawezesha wakulima kufanya kufanya kilimo chenye tija.
 
Masoko utauza nini kama huzalishi?
Nafikiri hujawahi kulima ndio maana unasema hvyo. Mazao mengi sana hayana soko la uhakika japo hayazalishwi kwa wingi sana, Sasa yakizalishwa kwa wingi tena itakuwaje? Na ukumbuke hayazalishwi kwa wing sana coz pia wengi wenye mitaji wanakikwepa kilimo. Miaka mingi kilimo kinajiendesha chenyewe tu, kusiwepo na ruzuku watu wanalima ila mwisho masoko yanakuwa ishu. Angalia matunda na mbogamboga, mahindi, mpunga, mbaazi n.k
 
Back
Top Bottom