Kipi bora kati ya miembe ya kisasa na mitiki?

bachelor sugu

JF-Expert Member
Jan 30, 2018
2,689
3,642
Habari za usiku ndugu katika Jukwaa hili. Nimekuwa njia panda nikijaribu kufikiria kipi ni bora kukifanya kati ya hivyo viwili katika heading hapo.

Hebu tujaribu kupanuana mawazo katika hivi vitu viwili, ni kipi bora kukifanya kwanza kati ya kupanda miti ya miembe ya kisasa au kupanda miti ya mbao ya Mitiki?

Let say una ekari zako tano(5) then unataka kuwekeza ktk haya mazao mawili. Miembe ya kisasa wastani inachukua mwaka 1.5------>3 mpaka kuanza kuvuna hivyo inaanza kukingizia kipato ndani ya muda mfupi.

Mitiki kama miti ya mbao inachukua muda mrefu kuanzia miaka20 na kuendelea mpaka kuivuna japo ukiikatia hati miliki una uwezo wa kukopa kiasi kikubwa cha pesa toka benki iwapo shamba lako umelitunza vema.

Sasa naomba tuchangiane mawazo katika hili kipi bora kukipanda ili kuhakikisha unapata ustawi mzuri na kizazi chako(watoto)wanabaki na urithi wa maana?.Tafadhali maskhara tuweke pembeni kwanza.

Karibuni kwa mawazo.
 
Inategemea na dhumuni lako la huo uwekezaji kama ni kutaka kupata faida mda mfupi ama mda mrefu. Upandaji wa miti unahitaji utunzaji miaka mitatu ya mwanzo na uvumilivu kusubiri uvunaji kuanzia miaka 7 na kuendelea (mitiki). Ila matunda kama maembe ya kupandikiza miaka miwili tu unaanza kuvuna ila inabidi uwe na soko la uhakika maana mara nyingi yanaiva kwa pamoja na ni rahisi kuoza.
 
Mkaritusi ni mti wa mbao wenye faida ya haraka kulikn mtiki kwani ndani ya miaka 2.5 unaweza kuanza kuvuna. Watafute wakala wa misitu ujifunze kuusu hii miti. Tafuta tifori kwenye website.
 
Mkaritusi ni mti wa mbao wenye faida ya haraka kulikn mtiki kwani ndani ya miaka 2.5 unaweza kuanza kuvuna... Watafute wakala wa misitu ujifunze kuusu hii miti. Tafuta tifori kwenye website
Ok ntacheck hao tifori nione
 
Mie ningekuwa ni wewe ningeshauri maembe tu kwa kweli.utaendelea kuyavuna kwa miaka na miaka,



Labda kwa vile sifahamu vizuri kuhusu mitiki,
Hapa tungekuwa na mchanganuo halisi wa miembe na mitiki interms of their their total returns tungejua which is the best.
 
Nakumbuka miaka iliyopita niliwahi kusoma article moja ya mh,Waziri wa maliasili na utalii wa enzi hizo ndugu Ezekiel Maige akiwahamasisha waTz kujiingiza ktk kilimo cha mitiki akifafanua kuwa
Cubic metre ya mbao za mtiki ni USD 800 Mumbai-India na USD 1200 Madrid-Spain so wastani wa mapato kwa ekari moja ni karibu sh.Bil 3 je kuna ukweli hapa?
 
Mkuu mikaratusi hii hii miaka 2.5 ?
Mkuu, faida ya karitusi utaanza kuipata ndani ya miaka hiyo. Kwa maana ya fito na milunda na majani yake ni dawa nzuri sana... Mitiki itabidi usubiri sana... TIFORI watakusaidia kuelewa zaidi ukiwatembelea kwenye web yao...
 
Mkuu mikaratusi hii hii miaka 2.5 ?
Mkuu, faida ya karitusi utaanza kuipata ndani ya miaka hiyo. Kwa maana ya fito na milunda na majani yake ni dawa nzuri sana... Mitiki itabidi usubiri sana... TIFORI watakusaidia kuelewa zaidi ukiwatembelea kwenye web yao...
 
Ok ntacheck hao tifori nione
Wanaitwa TAFORI
Ni watafiti wa misitu
Ipo mikaratusi iliyofanyiwa cloning, inakua haraka sana.
Yote kwa yote kilimo cha miti usikikurupukie bila ya kujua kama location ya mahala utakapoipanda ina favour ukuaji hiyo aina ya miti husika.
Bila ya hivyo hutolifikia lengo lako
 
Back
Top Bottom