Kipenga chapulizwa, vijana wa Chadema Ruksa kusogea majimboni kuajiandaa na uchaguzi 2025

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
876
4,101
Vijana wengi wa chadema wenye maono na fikra za kugombea Ubunge, udiwani na Urais walikuwa njia panda kujisogeza majimboni kwao kuanza rasmi harakati za kuwatoa wabunge waliopo.

Nimeona Moto uliowashwa Mwanza jimboni au nyumbani Kwa Pambalu, Ile NI walk-up call Kwa vijana kwenda kwenye majimbo kuanza kufanya siasa kuelekea 2025.

Nimemsikiliza Mhe Mbowe, siyo Tu mwanasiasa Bali NI kiongozi. Amezungumza na Taifa Kwa lugha ambayo MTU mwenye kiburi na mwenye kujiweka yeye na chama chake mbele asingeweza kuzungumza. Ameonyesha wazi hakwenda kwenye kikao na Mhe. Rais Kwa kujipendekeza Bali aliitwa kama MTU mwenye nguvu ya kisiasa na ambaye hayumbishwi.

Natambua hakuna kiongozi wa CCM anayeweza kukemea uovu adharani Kwa wafuasi wake kama alivyofanya Mbowe. Hii haimaanishi kwamba chadema wasikemeane Bali inaonyesha NI wapi tuna watu sahihi na wapi kuna chawa.

Mnapokwenda huko majukwaani kuzungumza na wananchi, jitahidini Sana kuyaishi aliyowaasa Mwenyekiti. Niwatakie hamsha hamsha njema kuanzia vyuoni Hadi kwenye matawi
 
Back
Top Bottom