Je unao uwezo wa kufanya maamuzi sahihi katika muda muafaka?
Jamaa pichani ni baba wa familia hapo yuko kwenye harakati za kufanya uokoaji.. Anapaswa kuchagua mmoja wa kumuokoa kwa wakati huo
Yupo baba mzazi
Yupo mke wake wa ndoa
Yupo mwanae
Amuokoe nani sasa?
Jamaa anaamua kumuokoa baba yake mzazi ambaye ni mzee na anayekaribia kabisa kuzama na kumuacha mke wake na mwanae ambao ni wepesi zaidi wa kuokoa wakiangamia... Je huu ni uamuzi sahihi?! Vipaumbele ndio hutoa majibu yote! Sahihi na yasiyo sahihi
Kwenye picha kuna watu wane
1. Mtendaji/ mtoa maamuzi ... Mwamuzi wa kipaumbele
2. Baba mzazi ni kiwakilishi cha wakati uliopita (past)
3. Mke ni kiwakilishi cha wakati wa sasa( present)
4. Mtoto ni kiwakilishi cha wakati ujao (future)
Jamaa anaamua kuishi wakati uliopita kwa kumuokoa baba mzazi na kuacha mke na mtoto wakiangamia (present & future).. Lakini kwa picha ilivyo naye ataangamia
Kwa mantiki ya kimaisha jamaa anaishi jana, ambayo ina msaada kidogo sana kwake! Anaidharau leo ambayo ndio tunda la kesho... Kesho yake chaji yake ni leo lakini kwa kughafilika kaigeuza jana ndio leo na kesho yake! Kutoboa ni ngumu!
Je kesho yako unaitengeneza jana ama leo?
Vipaumbele!
View attachment 2501337