Kipaumbele chako katika maisha ni kipi?

Kipaumbele chako katika maisha ni kipi?

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,456
Reaction score
872,090
Je unao uwezo wa kufanya maamuzi sahihi katika muda muafaka?

Jamaa pichani ni baba wa familia hapo yuko kwenye harakati za kufanya uokoaji.. Anapaswa kuchagua mmoja wa kumuokoa kwa wakati huo
Yupo baba mzazi
Yupo mke wake wa ndoa
Yupo mwanae
Amuokoe nani sasa?

Jamaa anaamua kumuokoa baba yake mzazi ambaye ni mzee na anayekaribia kabisa kuzama na kumuacha mke wake na mwanae ambao ni wepesi zaidi wa kuokoa wakiangamia... Je huu ni uamuzi sahihi?! Vipaumbele ndio hutoa majibu yote! Sahihi na yasiyo sahihi

Kwenye picha kuna watu wane
1. Mtendaji/ mtoa maamuzi ... Mwamuzi wa kipaumbele
2. Baba mzazi ni kiwakilishi cha wakati uliopita (past)
3. Mke ni kiwakilishi cha wakati wa sasa( present)
4. Mtoto ni kiwakilishi cha wakati ujao (future)

Jamaa anaamua kuishi wakati uliopita kwa kumuokoa baba mzazi na kuacha mke na mtoto wakiangamia (present & future).. Lakini kwa picha ilivyo naye ataangamia
Kwa mantiki ya kimaisha jamaa anaishi jana, ambayo ina msaada kidogo sana kwake! Anaidharau leo ambayo ndio tunda la kesho... Kesho yake chaji yake ni leo lakini kwa kughafilika kaigeuza jana ndio leo na kesho yake! Kutoboa ni ngumu!

Je kesho yako unaitengeneza jana ama leo?
Vipaumbele!
Screenshots_2023-01-31-15-07-02.jpg
 
Hata sielewi
Umenichanganya sana
Kuna watu wanashindwa kusonga mbele kwakuwa fikra zao zote ni kuhusu yaliyopita, waliyoyafanya jana na juzi.. Hawana jipya la leo wala kesho
Ndio hao wanaoishia kusema
Usimuone anaringa tulimpokea mjini sisi
Huyo yuko hivi sasa hivi lakini darasani alikuwa mweupe kabisa..nknk
 
Past, present na future havipo separate bali ni muendelezo Kila kimoja kinakijenga kingine! Past imebeba majibu mengi ya future, past ndio chanzo Cha future na present ni kiunganishi tu! Inategemea na muktadha. Maisha ni balance kati ya kale, Sasa na yajayo! Kwa muktadha huu nitaiokoa future kwa maana present ni Mimi na ndani yangu nimeibeba past!
 
Its alright. But don't cling to the past!
 
Umeongea kitu kizuri sana brother

Lakini mara nyingine si kwamba watu wote hawapendi kusahau ya nyuma na kuianza kesho ila athari za past yao huwawinda popote

Kingine hata leo itakuwa jana pale kesho itakapofika kwa hiyo ni ngumu kusema kama kila siku huja na lake pasipo athari ya uliyoyafanya..baada ya kupanda ni kuvuna mkuu🙏🏽
 
Je unao uwezo wa kufanya maamuzi sahihi katika muda muafaka?

Jamaa pichani ni baba wa familia hapo yuko kwenye harakati za kufanya uokoaji.. Anapaswa kuchagua mmoja wa kumuokoa kwa wakati huo
Yupo baba mzazi
Yupo mke wake wa ndoa
Yupo mwanae
Amuokoe nani sasa?

Jamaa anaamua kumuokoa baba yake mzazi ambaye ni mzee na anayekaribia kabisa kuzama na kumuacha mke wake na mwanae ambao ni wepesi zaidi wa kuokoa wakiangamia... Je huu ni uamuzi sahihi?! Vipaumbele ndio hutoa majibu yote! Sahihi na yasiyo sahihi

Kwenye picha kuna watu wane
1. Mtendaji/ mtoa maamuzi ... Mwamuzi wa kipaumbele
2. Baba mzazi ni kiwakilishi cha wakati uliopita (past)
3. Mke ni kiwakilishi cha wakati wa sasa( present)
4. Mtoto ni kiwakilishi cha wakati ujao (future)

Jamaa anaamua kuishi wakati uliopita kwa kumuokoa baba mzazi na kuacha mke na mtoto wakiangamia (present & future).. Lakini kwa picha ilivyo naye ataangamia
Kwa mantiki ya kimaisha jamaa anaishi jana, ambayo ina msaada kidogo sana kwake! Anaidharau leo ambayo ndio tunda la kesho... Kesho yake chaji yake ni leo lakini kwa kughafilika kaigeuza jana ndio leo na kesho yake! Kutoboa ni ngumu!

Je kesho yako unaitengeneza jana ama leo?
Vipaumbele!View attachment 2501337
Fikirishi sana hio, The past is Gold
 
Back
Top Bottom