Kipaumbele cha serikali yetu ni kipi?

Kipaumbele cha serikali yetu ni kipi?

Kipaumbele cha hivi karibuni kabisa ni ziara ya Kahama kuwashukuru wananchi,sijui kama ina tija.
 
Mwezi wa 8 keshokutwa waziri wa viwanda na biashara alitoa ahadi ya kuishangaza dunia atakapozindua mikakati ya wizara jinsi watakavyofufua viwanda; wiki ijayo ndio August tusubiri.
 
Hakuna walijualo ni kuropoka kuiga kila kitu uongo na kuvizia cha kusema unaambiwa sasa wana kula mpaka akiba hawana hata cha kufanya zaidi ya kukwama mkwamo wa mwaka serikali isyona Baraka ya Mungu huwa hivyo hivyo
 
Nimecopy hii katika chanzo kimoja cha habari wakati akitaja mambo 25 atakayo tekeleza katika utawala wake


Dar es Salaam. Mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli amefungua pazia la kampeni za chama hicho kwenye Viwanja vya Jangwani katika tukio lililohudhuriwa na maelfu ya wananchi, huku akieleza mambo 25 atakayoyafanya iwapo Watanzania watamchagua kuwa Rais wa Awamu ya Tano.

Huku akitumia maneno: “Mimi kazi tu”, “Tanzania ya Magufuli ni ya viwanda”, Dk Magufuli aliyetumia dakika 53 kueleza sera zake, kuanzia saa 11.40 hadi 12.33 jioni alisema Watanzania wanataka kitabu kipya cha mabadiliko na yeye na mgombea mwenza, Samia Suluhu ndiyo wanaoweza kuyaletea.

Mgombea huyo wa urais wa CCM aliahidi kuanzisha mahakama maalumu ya kusikiliza kesi za rushwa na ufisadi, kumaliza tatizo la wanafunzi wa elimu ya juu kukosa mikopo, kuhakikisha mama lishe hawabughudhiwi, kusimamia haki za wasanii, kulinda Muungano na usalama wa nchi.

Aliahidi kutoingilia utendaji kazi wa Bunge na Mahakama, kuheshimu mawazo ya vyama vingine vya siasa, kuimarisha vyombo vya ulinzi na usalama, wafanyabiashara wadogo na wakubwa wote kulipa kodi, kuendeleza kilimo, mifugo, uchimbaji wa madini, majisafi na elimu bora.

Nyingine ni kusimamia nishati ya gesi, ujenzi wa barabara, reli, kuboresha sekta ya utalii, kuimarisha uwekezaji, kuwasaidia walemavu na kusimamia uhuru wa habari.

Mkutano huo ulioanza rasmi saa 9.30 alasiri ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na CCM, wakiongozwa na Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete na marais wastaafu, Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa. Wengine ni Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba na Salim Ahmed Salim.
Ahadi alizotoa

Mgombea huyo alitoa ahadi mbalimbali ikiwamo ajira akisema: “Ninataka Watanzania wapate ajira, kazi ya Serikali itakuwa kukusanya kodi tu. Viwanda vinaweza kutengeneza ajira kwa asilimia 40 hasa kwa vijana wanaohitimu vyuo mbalimbali nchini.”

Kuhusu ubinafsishaji, alisisitiza: “Kuna viwanda vilibinafsishwa sasa wahusika wasipoviendeleza wajiandae kuvirudisha haraka.”

Mbali na kurejesha viwanda vilivyobinafsishwa, alisema akipewa ridhaa hiyo atahakikisha chini ya uongozi wake, anajenga viwanda vingi vipya, akiainisha vile mahsusi kwa shughuli za kilimo, mifugo, kusindika nyama na madini.

Alitaja kipaumbele kingine kuwa ni kilimo na kwamba atahakikisha sekta hiyo ambayo ndiyo mhimili wa uchumi inaendelezwa.

“Tutaleta vitendea kazi, pembejeo na vifaa vingi vya kisasa na vya kutosha kwa wakulima… kama nilivyosema hapo awali, tutajenga viwanda kwa ajili ya wakulima pia.

Mbunge huyo wa zamani wa Chato alisema pia kipaumbele kingine katika Serikali yake ni kuhakikisha kuwa wananchi wa mjini wanapata majisafi na salama kwa asilimia 95 na wananchi wa vijijini wanapata maji kwa asilimia 85.

Kuhusu afya alisema: “Tutahakikisha tunakuwa na vituo vya afya, zahanati na hospitali katika maeneo mbalimbali kwa sababu tunaamini maendeleo ya kweli hayawezi kupatikana kama wananchi hawana afya bora.”

Kipaumbele kingine ni mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu akisema watakuwa wanapata mikopo kwa wakati bila kuchelewa na kwamba watajikita pia katika kujenga hosteli kwa wanafunzi wa vyuo.

“Mishahara ya walimu na wafanyakazi wote tutaishughulikia. Hata madereva haki zao za msingi lazima ziangaliwe,” alisema huku akishangiliwa na wafuasi wa chama hicho.

Mgombea huyo alisema anafahamu kero ya msongamano wa magari katika Jiji la Dar es Salaam na kwamba maendeleo ya kweli yatapatikana kama changamoto hiyo itafanyiwa kazi.

“Tutaunganisha mikoa yote kwa barabara zenye viwango vya lami na pia tutajenga barabara za juu saba jijini hapa,” alisema Magufuli.

Alisema akipewa ridhaa hiyo itashughulikia suala la reli kwa kujenga reli ya kisasa kwa viwango vya Standard Gauge” na kuboresha bandari na usafiri wa anga.

Kuhusu maliasili, alisema ni kipaumbele katika Serikali yake endapo akipewa ridhaa ya kuongoza nchi huku akieleza kukerwa na ujangili... “Ninapata shida sana ninapoona meno ya tembo yanauzwa Ulaya halafu unaambiwa yanatoka Tanzania… sasa unajiuliza yanapitaje?”

Alisema ili kushughulikia suala hilo atahakikish
Vipaumbele hivyo vilivyotolewa wakati wa kampeni ni sahihi kabisa. Lakini hili la kwenda Dodoma Kwa haraka haraka sidhan kama lilitajwa.

Nadhan akiwa kama mkuu wa nchi awaite wasaidiz wake kuona namna bora ya jinsi ya kuhakikisha Serikali inahamia mjini Dodoma kwa utaratibu sahihi.
 
Vipaumbele hivyo vilivyotolewa wakati wa kampeni ni sahihi kabisa. Lakini hili la kwenda Dodoma Kwa haraka haraka sidhan kama lilitajwa.

Nadhan akiwa kama mkuu wa nchi awaite wasaidiz wake kuona namna bora ya jinsi ya kuhakikisha Serikali inahamia mjini Dodoma kwa utaratibu sahihi.
Nilikuwa namkumbusha mleta thread juu ya swali la vipaumbele vya serikali ni vipi ...
Kuwaita watu wake wa karibu wakati tayari matamko ya kuhama within weeks yashaanza kutolewa na wasaidizi wake ..
 
Tangu mwezi wa 11 mwaka Jana, Serikali ilituambia kuwa kipaumbele chake cha kwanza ni viwanda. Leo ni mwaka unaelekea kuisha, sioni hata dalili ya hicho kiwanda.sasa hivi wamekuja tena na mpya. Mnaniambia ni kuhamia Dodoma. As I know fedha za kuhamia Dodoma ni nyingi kuliko ambazo zinahitajika kufufua viwanda vyetu.

Hali za maisha za watu mitaani ni mbaya sana. Mzunguko wa pesa ni mdogo haijawahi kutokea tangu Mwinyi. Ni dhahiri kuwa wananchi hawana furaha kabisa. Kila mtu analalamika. Tajiri analalamika. Masikini ndiyo kabisa anahisi bora asingezaliwa.

Nataka kujua seriously. Nini hasa kipaumbele chenu?. Kesho hatujui mtatuambia kituko gani tena kipya. Mimi nafikiri mngetekeleza kwanza la viwanda halafu hayo mengine yaje taratibu. Hatuna haraka ya kuhama kiasi hiki, Serikali kuweni na huruma na mnaowangoza. Rekebisheni kwanza hali zao za uchumi. Hali zao ni mbaya mno huko mitaani.


KIPAUMBELE NI KUENDELEZA UVAMIZI ZANZIBAR KWA KUWEKA VIBARAKA KWA COST YOYOTE

KUKANDAMIZA DEMOKRASIA NA KUUWA UPINZANI KWA KUTUMIA JESHI NA POLISI KAMA ILIVYO SASA
 
Jambo la muhimu ni kuendelea kumuomba Mungu Taifa liende katika njia sahihi.
Rais anayo nia njema kwa Nchi na watu wake ila nadhani approaches zinazitumika katika kufanikisha malengo ndiyo tatizo.
 
Safi Sana kwa ufafanuzi na nitajitahidi kuwa mzalendo, mbona kwenye vipaumbele ambavyo umetaja mbona hakuna swala la kuhamia Dodoma?, sasa hayo malengo mengine kweli yanaweza kukamilika kwa wakati maana naona Kama serikali sasa imelukia jambo lingine ambalo halikuwepo kwa jinsi ufafanuzi wako ulivyoutoa
swala la kuhamia dodoma kwani umeanza kulisikia lini ewe mtanzania ?????
 
Kuwakomboa watanzania kutoka ktk umasikini.
 
Back
Top Bottom