Kipaumbele cha serikali yetu ni kipi?

Kipaumbele cha serikali yetu ni kipi?

Sasa hivi wamekuja na nilazima ueshim nembo za taifa wimbo ukipigwa simama na bendera ikishushwa na ww upo Karibu ni wajbu wako kusimama
 
Nimecopy hii katika chanzo kimoja cha habari wakati akitaja mambo 25 atakayo tekeleza katika utawala wake

Dar es Salaam. Mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli amefungua pazia la kampeni za chama hicho kwenye Viwanja vya Jangwani katika tukio lililohudhuriwa na maelfu ya wananchi, huku akieleza mambo 25 atakayoyafanya iwapo Watanzania watamchagua kuwa Rais wa Awamu ya Tano.

Huku akitumia maneno: “Mimi kazi tu”, “Tanzania ya Magufuli ni ya viwanda”, Dk Magufuli aliyetumia dakika 53 kueleza sera zake, kuanzia saa 11.40 hadi 12.33 jioni alisema Watanzania wanataka kitabu kipya cha mabadiliko na yeye na mgombea mwenza, Samia Suluhu ndiyo wanaoweza kuyaletea.

Mgombea huyo wa urais wa CCM aliahidi kuanzisha mahakama maalumu ya kusikiliza kesi za rushwa na ufisadi, kumaliza tatizo la wanafunzi wa elimu ya juu kukosa mikopo, kuhakikisha mama lishe hawabughudhiwi, kusimamia haki za wasanii, kulinda Muungano na usalama wa nchi.

Aliahidi kutoingilia utendaji kazi wa Bunge na Mahakama, kuheshimu mawazo ya vyama vingine vya siasa, kuimarisha vyombo vya ulinzi na usalama, wafanyabiashara wadogo na wakubwa wote kulipa kodi, kuendeleza kilimo, mifugo, uchimbaji wa madini, majisafi na elimu bora.

Nyingine ni kusimamia nishati ya gesi, ujenzi wa barabara, reli, kuboresha sekta ya utalii, kuimarisha uwekezaji, kuwasaidia walemavu na kusimamia uhuru wa habari.

Mkutano huo ulioanza rasmi saa 9.30 alasiri ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na CCM, wakiongozwa na Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete na marais wastaafu, Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa. Wengine ni Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba na Salim Ahmed Salim.
Ahadi alizotoa

Mgombea huyo alitoa ahadi mbalimbali ikiwamo ajira akisema: “Ninataka Watanzania wapate ajira, kazi ya Serikali itakuwa kukusanya kodi tu. Viwanda vinaweza kutengeneza ajira kwa asilimia 40 hasa kwa vijana wanaohitimu vyuo mbalimbali nchini.”

Kuhusu ubinafsishaji, alisisitiza: “Kuna viwanda vilibinafsishwa sasa wahusika wasipoviendeleza wajiandae kuvirudisha haraka.”

Mbali na kurejesha viwanda vilivyobinafsishwa, alisema akipewa ridhaa hiyo atahakikisha chini ya uongozi wake, anajenga viwanda vingi vipya, akiainisha vile mahsusi kwa shughuli za kilimo, mifugo, kusindika nyama na madini.

Alitaja kipaumbele kingine kuwa ni kilimo na kwamba atahakikisha sekta hiyo ambayo ndiyo mhimili wa uchumi inaendelezwa.

“Tutaleta vitendea kazi, pembejeo na vifaa vingi vya kisasa na vya kutosha kwa wakulima… kama nilivyosema hapo awali, tutajenga viwanda kwa ajili ya wakulima pia.

Mbunge huyo wa zamani wa Chato alisema pia kipaumbele kingine katika Serikali yake ni kuhakikisha kuwa wananchi wa mjini wanapata majisafi na salama kwa asilimia 95 na wananchi wa vijijini wanapata maji kwa asilimia 85.

Kuhusu afya alisema: “Tutahakikisha tunakuwa na vituo vya afya, zahanati na hospitali katika maeneo mbalimbali kwa sababu tunaamini maendeleo ya kweli hayawezi kupatikana kama wananchi hawana afya bora.”

Kipaumbele kingine ni mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu akisema watakuwa wanapata mikopo kwa wakati bila kuchelewa na kwamba watajikita pia katika kujenga hosteli kwa wanafunzi wa vyuo.

“Mishahara ya walimu na wafanyakazi wote tutaishughulikia. Hata madereva haki zao za msingi lazima ziangaliwe,” alisema huku akishangiliwa na wafuasi wa chama hicho.

Mgombea huyo alisema anafahamu kero ya msongamano wa magari katika Jiji la Dar es Salaam na kwamba maendeleo ya kweli yatapatikana kama changamoto hiyo itafanyiwa kazi.

“Tutaunganisha mikoa yote kwa barabara zenye viwango vya lami na pia tutajenga barabara za juu saba jijini hapa,” alisema Magufuli.

Alisema akipewa ridhaa hiyo itashughulikia suala la reli kwa kujenga reli ya kisasa kwa viwango vya Standard Gauge” na kuboresha bandari na usafiri wa anga.

Kuhusu maliasili, alisema ni kipaumbele katika Serikali yake endapo akipewa ridhaa ya kuongoza nchi huku akieleza kukerwa na ujangili... “Ninapata shida sana ninapoona meno ya tembo yanauzwa Ulaya halafu unaambiwa yanatoka Tanzania… sasa unajiuliza yanapitaje?”

Alisema ili kushughulikia suala hilo atahakikish
 
Kwa bahati mbaya sana watanzania hawana uzalendo na nchi yao huo ndo ukweli...asilimia kubwa sana wapo kimaslahi kwahiyo hata ambao wana nia ya dhati ya kuitumikia nchi yao hawaaminiki lakini katika kila kutafuta mafanikio lazima upitie shida...hamna kitu kizuri kinachopatikana kirahisi...
Tujitahidi kusoma malengo ya taifa letu...tuache kuwa na roho za kulipizana visasi mbaya sana hiyo...watu inapaswa tujue ktk mpango wa serikali 2016/2017-2020/2021 ni kufufua na kujenga viwanda na mpango wa serikali wa 2021/2022-2025/2026 ni kuboresha na masoko ya bidhaa na hasa kupata masoko ya nje...watu kila siku mnakalia kuuliza dira ya serikali etc badala ya kuisoma tu hyo dira ya serikali na kisha kufanya kazi kwa bidii ili kushirikiana na serikali iliyopo kufanikisha malengo...kuna miwatu inasubiri rais akosee ili 2020 wapate pa kuanzia ni mbaya sana...fikiria na muda pia hautakusubiri wewe mpka mwaka 2020 na huwezi jua hao unaowategemea na kuwaamini watakua wapi...kila mmoja ana malengo na siku zote malengo hayabadiliki ila njia za kufikia malengo hubadilika... Tuache siasa katika kujenga nchi... Tuwe wazalendo na nchi yetu...
 
Xlxmgm

Hehehehe imeingia hiyo watoto wa mjini tunasema IMOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
 
Hakuna kipaumbele kwenye serikali za CCM. Ni kukurupuka tuu. Kinachokuja mbele wanaanza nacho...

Hii inatokana na kukosekana kwa DIRA YA TAIFA!! Hapa kila anayeingia anaingia na ya kwake. hakuna mwendelezo!!! Kila awamu mambo yanaanza upya!!

Fikiri tuu Kitambulisho cha Taifa kiko wapi? Watu wangapi wanavyo? Na wala husikii tena kiongozi ye yote anaongelea. Wimbo wa Kilimo kwanza umeimbwa hadi umekwisha bila kuwa na mchezaji!!
Ni shiidaa
 
Tanzania tu, nchi ambayo wanasiasa wanaweza kutugeuza wapendavyo, enzi zile wanasiasa walitulaghai, kwa kikombe cha babu wa loliondo ili tusikumbuke EPA, leo tunaletewa agenda ya kuamia dodoma ili iue ile ya sera ya viwanda!

ongera sana! kila la heri! magufuli nyie ichezesheni nchi shegere ila kukipanzuka mtatafuta pa kukimlia hamtapapata!

ili lilikuwa ukurasa wa ngapi wa ahadi au ilani za ccm.!
 
Kuhamia Dodoma ni gharama kubwa sana !
Hili jambo sio kipaumbele
 
hahaa mkuu kama serikali ipo chini ya ccm usitarajie lolote tangu tumezaliwa mpaha tutakufa ni kamba.....................hata kuhamia dom nayo inaweza ikawa chai
 
Sasa imekuwa kila Siku bora ya jana. Badala ya kupiga hatua kwenda mbele sisi tunapiga kurudi nyuma. Watu wamekata tamaa mapema sana. Awe ccm awe ukawa awe asiye na chama, wote ni taabani. Dhufli hali
 
Viwanda ni kipaumbele but utekelezaji wake ni muda mrefu na kuhamia Dodoma siyo kipaumbele bali ni jambo la Lazima.Niambie Wizara gani haina ofisi Dodoma so siyo swala la KUHAMIA bali ni swala la KWENDA DODOMA fullstop
 
Kwa bahati mbaya sana watanzania hawana uzalendo na nchi yao huo ndo ukweli...asilimia kubwa sana wapo kimaslahi kwahiyo hata ambao wana nia ya dhati ya kuitumikia nchi yao hawaaminiki lakini katika kila kutafuta mafanikio lazima upitie shida...hamna kitu kizuri kinachopatikana kirahisi...
Tujitahidi kusoma malengo ya taifa letu...tuache kuwa na roho za kulipizana visasi mbaya sana hiyo...watu inapaswa tujue ktk mpango wa serikali 2016/2017-2020/2021 ni kufufua na kujenga viwanda na mpango wa serikali wa 2021/2022-2025/2026 ni kuboresha na masoko ya bidhaa na hasa kupata masoko ya nje...watu kila siku mnakalia kuuliza dira ya serikali etc badala ya kuisoma tu hyo dira ya serikali na kisha kufanya kazi kwa bidii ili kushirikiana na serikali iliyopo kufanikisha malengo...kuna miwatu inasubiri rais akosee ili 2020 wapate pa kuanzia ni mbaya sana...fikiria na muda pia hautakusubiri wewe mpka mwaka 2020 na huwezi jua hao unaowategemea na kuwaamini watakua wapi...kila mmoja ana malengo na siku zote malengo hayabadiliki ila njia za kufikia malengo hubadilika... Tuache siasa katika kujenga nchi... Tuwe wazalendo na nchi yetu...
Safi Sana kwa ufafanuzi na nitajitahidi kuwa mzalendo, mbona kwenye vipaumbele ambavyo umetaja mbona hakuna swala la kuhamia Dodoma?, sasa hayo malengo mengine kweli yanaweza kukamilika kwa wakati maana naona Kama serikali sasa imelukia jambo lingine ambalo halikuwepo kwa jinsi ufafanuzi wako ulivyoutoa
 
Serikali ya mwendokasi na iliyojaa mihemko..haiwezi kamwe kua na kipaumbele kinachoeleweka.
 
kwa kweli kutokana na hali ya kiuchumi ya nchi ilivyo kwa sasa haikutakiwa kuharakisha kuhamia Dodoma.ifahamike kuwa kuna gharama kubwa ambazo zitatumika kuhamisha watumishi na ofisi.sijaelewa hizo wizara zilizopanga kuhamia mwaka huu wa fedha wamepata wapi hayo mafungu maana kwenye bajeti hatukusikia kama kuna pesa za kuhamia Dodoma.huu mwendokasi unaosababisha ajali hatuutaki.
 
Kipaumbele cha serikali yetu ni kipi? Ni kuhakikisha kuwa CCM inatawala milele kwa gharama zozote zile!
 
Serikali nguvu ya soda. Mbwembwe nyingi hakuna utekelezaji.
Wamewekeza kuwanyamazisha wapinzani ili wasikosolewe. Bajeti ilikuwa utumbo na hao wabunge vila.za waliipitisha kwa mbwembwe.
Sasa hivi serikali haina fedha, ndo maana tunasikia misaada na mikopo kila siku. Mara South Korea, China, USA.
Hao mawaziri ni kama cheeleaders. Kushangilia kila anachosema badala ya kumpa ushauri pale anapokosea.
Sasa hivi tupo kwenye wimbo wa kuhamia dodoma, kabla haujaisha vizuri utaanzishwa wimbo mpya.
Wanataka tufuate sheria lakini wao ni wa kwanza kuzivunja.
Hakuna tofauti na wale wapuuzi walionzisha operation UKUTA.
Baada ya maazimio kibao kuferi ,Mara sangara,m4c ,ukawa, ,kususia bunge, na mengine mengi ya hovyo .
 
Sasa imekuwa kila Siku bora ya jana. Badala ya kupiga hatua kwenda mbele sisi tunapiga kurudi nyuma. Watu wamekata tamaa mapema sana. Awe ccm awe ukawa awe asiye na chama, wote ni taabani. Dhufli hali
Sasa kama kila siku unafanyiwa operation ya kushikishwa UKUTA ,lazima uone afadhali ya Jana.
 
Back
Top Bottom