Kipaumbele cha serikali yetu ni kipi?

Kipaumbele cha serikali yetu ni kipi?

Tangu mwezi wa 11 mwaka Jana, Serikali ilituambia kuwa kipaumbele chake cha kwanza ni viwanda. Leo ni mwaka unaelekea kuisha, sioni hata dalili ya hicho kiwanda.sasa hivi wamekuja tena na mpya. Mnaniambia ni kuhamia Dodoma. As I know fedha za kuhamia Dodoma ni nyingi kuliko ambazo zinahitajika kufufua viwanda vyetu.

Hali za maisha za watu mitaani ni mbaya sana. Mzunguko wa pesa ni mdogo haijawahi kutokea tangu Mwinyi. Ni dhahiri kuwa wananchi hawana furaha kabisa. Kila mtu analalamika. Tajiri analalamika. Masikini ndiyo kabisa anahisi bora asingezaliwa.

Nataka kujua seriously. Nini hasa kipaumbele chenu?. Kesho hatujui mtatuambia kituko gani tena kipya. Mimi nafikiri mngetekeleza kwanza la viwanda halafu hayo mengine yaje taratibu. Hatuna haraka ya kuhama kiasi hiki, Serikali kuweni na huruma na mnaowangoza. Rekebisheni kwanza hali zao za uchumi. Hali zao ni mbaya mno huko mitaani.

Mtafute mtu huko Sudan ya Kusini au Burundi au Somalia au Syria au Yemen, kisha kawaulize swali hilohilo: hivi kipaumbele cha serikali yenu ni kipi (kama utafanikiwa kuwapata hao watu wa kuwauliza). Moja ya vipaumbele vya serikali unayoilaumu ni kuhakikisha usalama wako. Si umesikia kilichotokea Kenya jana?

Na kabla ya kuihoji serikali kuhusu vipaumbele vyake, hebu tuambie wewe kama mwananchi vipaumbele vyako ni vipi? Uzoefu unaonyesha kuwa watu ambao wapo bize na masuala yao huwa hawana muda na 'masuala ya wngine.' Laiti ungekuwa mbele katika vipaumbele vyako, kwa mfano upo bize na self employment iwe biashara au kilimo au shughuli yoyote ile halali ya kukuingizia kipato, sidhani kama ungekuja na swali hilo. Hay tuambiwe, wewe kipaumbele chako ni kipi hasa?

Hali ya uchumi ni mbaya huko mtaani kwa sababu kulikuwa na watu ambao zamani tuliwaita kupe, waliovuna wasichopanda, walioendesha magari ya thamani japo hawakuwa na kazi maalum. Wengi wa manaolalamika kuwa hali ni ngumu mtaani ni wale mliokuwa mkifisadi nchi yetu. Sasa mianya imebwana, mnakuja kuiuliza serekali kuhusu mwelekeo.Mwelekeo wa serikali hii ni kwamba ASIYEFANYA KAZI NA ASILE. KILA MTU ATAKULA KWA JASHO LAKE. So get working.

I hope nimesaidia kukujibu swali lako
 
"We defined our priorities, based on the needs and interests of Rwandans, and we stuck by them. At each point, we asked ourselves: Will this unite Rwandans,or divide us further? Will it contribute to making Rwanda a dignified and prosperous nation for all? The choices we faced, were absolutely fundamental. For example, on national identity, are we Rwandans first and foremost, or something else? On service delivery and accountability, do officials serve the public, or will we tolerate it being the other way around?And on the quest for prosperity, is every citizen responsible for our well-being, or does the state or foreign donors owe us living? These choices involved extensive dialogue and consensus-building among citizens. But once agreed upon, we were able to set about building the institutions and systems necessary for implementation, and tracking progress toward our goals."

- President Kagame speaks alongside President Nyusi and shares Rwanda's story during an address to academics and members of the business community in Maputo,Mozambique.

For more pictures: https://www.flickr.com/photos/paulkagame/albums/72157674233670782

For videos:

 
Vibaraka wa mbowe mnajitahidi sana mitandaoni. Endeleeni hivyo hivyo mtapata zawadi kwa dada zenu kuolewa na mbooweee
Naomba nkulize swali we gamba....
Hivi mtanzania wa kawaida na wa hali ya chini anaishi kwa kutumis $ ngapi kwa siku?

OVA
 
Back
Top Bottom