Kipanya, Mkuu wa Mkoa ameruhusu ngono?

Kipanya, Mkuu wa Mkoa ameruhusu ngono?

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
104,319
Reaction score
183,600
Masoud (KP media) anaendesha mradi wa 'Inawezekana' kule sikonge Tabora. Washiriki wa mradi wamemlalamikia RC wa Tabora kuruhusu vitendo vya ngono kwa madai kuwa wao ni watu wazima, ilhali katiba ya mradi inakataza ngono kambini.

Pia wanailaumu Halmashauri kwa kutaka kupora nguvu zao hasa zile nyumba 100 so wametishia kuuza kila kitu. Najua Kipanya unapitaga humu ufafanuzi p'se!

Chanzo: Clouds Tv (Kipindi, Inawezekana).
 
Kwa ambaye hajaangalia kipindi ni vigumu kuelewa unachokudia kusema

Unaweza kuiboresha taarifa yako tafadhali
 
Mtoa mada tafadhari rudi utoe ufafanuzi.
 
JohnThebabtist mkuu hivi wale vijana wanakaa kambini tu hawaruhusiwi kwenda kwao?
 
Last edited by a moderator:
Sio wote wanaangalia hicho kipindi,ukileta taarifa humu ilete kama unamwandikia mtu ambaye hajui hko kipindi,jazia nyama tuelewe.
 
Madai mazito haya.ngoja kipanya atalitolea maelezo.
 
mmmh mwaka jana septemba mkuu wa kaya alifika kwenye hicho kijiji cha maisha plus. Kama vile aliruhusu wanaotaka kuoana waoane. hiyo ni mujibu wa kumbukumbu. Lakini hao sio watawa. Mkazi wa sikonge
 
Sijaelewa chochote hapa na namwomba mungu nisielewe chochote hapa!!
 
Mie nachangia kwakuwa naangalia Hiki Kipindi Cha INAWEZEKANA jioni.

Sasa Mie pia nakumbuka Ujumbe wa Wabunge kadhaa waliotembelea pale pia waliuliza hili suala.
Na Pale Mradi wa Nyumba wa kijiji cha mfano ni mradi mkubwa na nyumba kali sana za kisasa wamejenga washiriki.Na pia mashamba ya Tumbaku na Kilimo cha Mahindi.

Washiriki Baadhi wametolewa kwa Kufanya Ngono,na wakati sheria iliwazuia,lakini ifahamike kwamba wale wote ni watu wazima,na yale ni maisha halisia,sasa kupendana ni lazima kunatokea.
Kuna mshiriki mmoja nahisi kama amerejeshwa katika wangonoka,ambapo Kidogo niliona Babu anapambana kwenye hoja juu ya hili.

Wazo lile la Kipanya ni zuri,ila kama kuna inside dili kwenye zile nyumba,hapo ajue vijana watamganda shingoni,maana nyumba kali sana kama za NHC
 
Back
Top Bottom