vampire_hunter007
JF-Expert Member
- Jul 25, 2015
- 1,034
- 2,615
Huyu jamaa nimekuwa nikimfuatilia muda mrefu.. Aisee huyu jamaa ni kichwa sana.. Yaani unaweza ukachukua threads kibao za JF na comments za watu, lakini yeye akaweza kuyapresent kwa mchoro mmoja tu..
Matatizo mengi sana ya kijamii amekuwa akiyawakilisha katika michoro yake.. Na kuna muda inahitaji akili ya ziada kuweza kuelewa michoro yake.. Michoro yake mingi imejaa Sarcasm na inakosoa kila penye kosa bila kujali ni upande wa serikali wala upinzani..
Kuna muda anaweza akatoa mchoro wake ukauchukulia poa mpaka baada ya muda ndo unaelewa alichokimaanisha.. Mfano ile ishu ya Sefue kutumbuliwa..
Nikawaza kuwa huyu jamaa anapaswa kupewa degree ya heshima na vyuo vyetu hapa Tz..
Hebu mwenye kumjua vizuri historia yake kielimu aitupie hapa ili tumfahamu kwa undani... Jamaa ni kichwa sana..
================
Matatizo mengi sana ya kijamii amekuwa akiyawakilisha katika michoro yake.. Na kuna muda inahitaji akili ya ziada kuweza kuelewa michoro yake.. Michoro yake mingi imejaa Sarcasm na inakosoa kila penye kosa bila kujali ni upande wa serikali wala upinzani..
Kuna muda anaweza akatoa mchoro wake ukauchukulia poa mpaka baada ya muda ndo unaelewa alichokimaanisha.. Mfano ile ishu ya Sefue kutumbuliwa..
Nikawaza kuwa huyu jamaa anapaswa kupewa degree ya heshima na vyuo vyetu hapa Tz..
Hebu mwenye kumjua vizuri historia yake kielimu aitupie hapa ili tumfahamu kwa undani... Jamaa ni kichwa sana..
================
Interview Kipanya na Bongo Celebrity July, 2007
KWA KINA NA MASOUD KIPANYA(KP)
Ukiiona katuni yake gazetini, huhitaji kutambulishwa au kusaka sana jina la mchoraji hata pale anapokuwa hajaweka sahihi yake. Taswira yenyewe ya katuni itakueleza. Ni katuni ambayo imekuwa sehemu ya maisha ya watanzania kwa miaka mingi sasa. Wengi wetu tunamfahamu kama Masoud Kipanya. Lakini je hilo ni jina lake halisi? Alianza lini shughuli za uchoraji?
BongoCelebrity leo ina furaha kuwaleteeni mahojiano ya kina na Masoud Kipanya, maarufu pia kama KP, mchora katuni maarufu, mtangazaji wa CLOUDS FM na pia mbunifu mahiri wa mitindo (fashion designer). Katika mahojiano haya, pamoja na kuweka bayana maswali mawili yaliyoulizwa hapo juu, KP anaongelea zaidi maisha yake kama mchora katuni zikiwemo kasheshe alizowahi kukumbana nazo, mtizamo wake kuhusu jamii au nchi zinazoendelea kama yetu ya Tanzania, anatoa ushauri kwa wanaotaka kuwa wachoraji kama yeye na zaidi ya yote anao ujumbe maalumu kwa Watanzania kuhusu viwalo vya KP vitakavyokuwa sokoni hivi karibuni.Yafuatayo ni mahojiano yenyewe;
BC: Awali ya yote, hebu tueleze Kipanya ni jina lako halisi au ni jina la katuni wako? Na kama ni jina lako halisi kwanini uliamua kulitumia kwa ajili ya katuni wako maarufu kama KIPANYA?
KP: Jina langu halisi ni Ali Masoud, jina la Kipanya ni matokeo ya katuni ya Kipanya niliyoibuni karibu miaka 13 iliyopita.
BC: Kwa ufupi unaweza kutuambia ulianza lini na kivipi kuchora katuni au vikaragosi kama ambavyo wengine wanaziita?
KP: Mapenzi ya kuchora yalianza nilipokuwa darasa la pili, na nilianza kwa kuiga tu katuni za ndani na za nje kama ilivyo kawaida kwa yoyote anayeanza kufanya kitu, ila professionally nilianza rasmi mwaka 1988, huo ndio mwaka ambao katuni yangu ya kwanza ilitoka katika gazeti la Heko.
BC: Je unatoka katika familia ya wasanii au wachoraji? Unao ndugu zako ambao nao ni wachoraji?
KP: Hapana, bahati mbaya katika familia yetu hakukuwa na mchoraji kabla yangu, isipokuwa baada ya mimi kuna mdogo wangu ambaye tayari ameshaanza kuja juu katika fani ya katuni, ila baba na mama yangu ni watu ambao ingawa si wachoraji, lakini mfumo wa maisha yao inatosha kabisa kusema nao pia ni wasanii.
BC: Hivi sasa wewe unastahili kabisa kuitwa “professional cartoonist”. Unadhani lini hasa ulifikia kiwango hicho?
KP: Nadhani pale nilipoanza kuaminika na katuni zangu kuingia magazetini, naweza kusema mwanzoni mwa miaka ya tisini.
BC:Nini raha hasa ya kuwa mchora katuni?
KP:Raha ya kuwa mchora katuni, ama kuwa mchoraji kwa ujumla ni kwamba unaweza kufanya kile ambacho mpiga mpicha hawezi kufanya, yani unaweza kufanya mbingu ikawa ardhi na ardhi ikawa mbingu, unaweza kumfanya Bush ama Kikwete waonekane wana miguu kama spoku za baiskeli nk.
BC:Ni vikwazo gani unavyokumbana navyo kama mchora katuni? Na je huwa unavivuka namna gani?
KP:Kikwazo kikubwa kwangu ni censorship. Kwa wasioelewa, censorship ni ile hali ambayo unachora katuni halafu kabla haijachapishwa inapitiwa na kama itaonekana ina madhara kwa mtu ama jamii Fulani, basi itarekebishwa ama isichapishwe kabisa. Hayo yamenitokea mara nyingi tu katika maisha yangu nikiwa katika magazeti mbalimbali. Mara nyingi censorship hutokea pale inapoonekana unachora katuni zinazosumbua mioyo ya walengwa hususan wanasiasa wasiopenda kukosolewa.
BC: Katika maisha yako kama mchora katuni ni lazima umeshakumbana na mengi. Je kuna tukio lolote ambalo hutokaa ulisahau kamwe? Ilikuwaje?
KP: Matukio yako mengi, kwa uchache tu, nakumbuka siku niliyomchora mtu mnene akiwa amemshika kamba iliyomfunga mbwa ambaye ameandikwa ‘polisi’, maana ya katuni hii ukiangalia kwa haraka haraka ni kwamba jeshi la polisi haliko kwa manufaa ya umma bali kwa manufaa ya watu wachache hasa viongozi wa chama tawala.Hiki kilikuwa ni kile kipindi ambacho wapinzani walikuwa wakibughudhiwa na polisi kila walipotaka kufanya mikutano yao ya hadhara. La pili ni wakati ule mbunge mmoja aliyejulikana kwa jina la Tuntemeke Sanga alipokuwa anaumwa, nilichora katuni inayomuonyesha mheshimiwa Sanga akiwa amelazwa huku akiwa ametundikiwa damu, halafu pembeni yuko serikali akiwa amegeukia upande mwingine huku akivuta sigara kana kwamba hajali, bahati mbaya siku iliyofuata Mzee Sanga akafariki, naikumbuka siku hiyo vizuri, aliyekuwa katibu wa bunge wa wakati huo, Mzee Mlawa, alivamia ofisi za gazeti la majira, bahati nzuri, wakati anaingia mimi nikawa natoka, na pengine kutokana na umbo langu, hakuweza kudhani kwamba pengine huyu ndio masoud kipanya. Kilichoendelea kati yake na mhariri wangu kwa kweli sikukifahamu.
BC: Unaye mchora katuni yeyote ambaye alichangia uamuzi wako wa kuwa mchora katuni?
KP: Kwa kweli kama msanii, naweza kusema wasanii wengi niliokuwa nikitazama kazi zao wakati ule walini-inspire niweze kupiga hatua.
BC: Maendeleo ya tekinolojia duniani yanabadilisha kila kitu kadri siku zinavyokwenda. Tofauti na hapo zamani ambapo wachoraji mlitumia zaidi kalamu na karatasi siku hizi mnatumia kompyuta nk.Wewe unatumia vifaa gani katika kufanikisha kazi zako?
KP: Pamoja na kukua kwa teknolojia, bado kuchora kwa kutumia mkono, kalamu na karatasi ndio mtindo unaoendelea kutumika, kompyuta inatumika tu katika kuboresha kazi ya msanii.
BC: Mara nyingi wachora katuni wanakuwa na hadhira (audience) ya aina mbili, wanaochukia na wanaocheka wanapoiona na kuisoma katuni. Unaupenda zaidi upande upi?
KP: Kwangu pande zote ni muhimu na ninazipenda. Kwanini? Wote wananifanya niamini kuwa kazi inafanyika, ukichukia maana yake kazi inafanyika, ukifurahi pia maana yake kazi inafanyika.
BC: Nini maoni yako kuhusu tuhuma kwamba wachora katuni wengi, hususani wanaochora katuni za kisiasa (wewe unachora pia japo sio kila mara) huwa wanaegemea zaidi upande wa mabaya (negatives) zaidi ya mazuri(positives)?
KP: Bahati mbaya sana tunaishi katika mazingira ambayo mustakabali wa maisha yetu unategemea sana maamuzi ya wanasiasa tofauti na nchi kama Japan ambayo mwanasiasa ni mtunzi na msimamizi wa sera tu na mfanyabiashara na mkulima ndio wanaoweza kubashiri mustakabali wa nchi kutokana na trend ya kilimo na biashara kwa ujumla. Kwa nchi kama Tanzania, bahati mbaya, wengi wa hawa wanaopewa dhamana ya kuamua hatma ya maisha yetu wanachokifanya kwa kweli ni madudu tu, na ndio maana wakati wote tunalazimika kuwa negative kwao si kwa chuki bali kuwekana sawa ili na sisi tuweze kuishi kama wanavyoishi wenzetu katika maeneo mengine ya dunia. Sitaki kupoteza muda na nafasi ya safu hii kuanza kuorodhesha dhambi za baadhi ya watendaji wetu, kila mtanzania anafahamu.
BC: Mara kadhaa katuni zimesababisha sokomoko za aina yake kutokana na wengine kuhisi wamekashifiwa kutokana na mchoro wa katuni. Unawezaje kuhakikisha kwamba katuni zako hazisababishi sokomoko au mitafaruku ndani ya jamii?
KP: Sio siri, katika kuchora katuni, umakini wa hali ya juu unatakiwa. Na ili uweze kuwa makini basi ni lazima uwe na talent ya hali ya juu hasa katika upande wa uwezo wa kumchora mtu bila ya kumuandika jina lake mgongoni, na pia lazima uwe na analytical thinking ili uweze kuchambua kitu kwa uwezo bila ya kuonekana umemshambulia mtu. Haya ndiyo yanayoweza kukuokoa katika masokomoko na mitafaruku ya kashfa. Kwa miaka mingi nimekuwa nikiwachora viongozi vibaya lakini hakuna hata siku moja niliyompa mtu nafasi ya kunibana kisheria.
BC:Kwa vijana wadogo wanaotaka kuibuka siku moja na kuwa kama wewe au kufikia hapo ulipo unawapa ushauri gani na wanahitaji vifaa gani kuanza kuzijenga ndoto zao?
KP:Kujua kuchora pekee hakutoshi kukufanya uwe mchoraji katuni mzuri. Lazima uwe mjuzi katika masuala ya general knowledge, ujuzi wa maarifa huzaliwi nao, unatokana na tabia ya kupenda kusoma na kujua kinachoendelea duniani. Kiu ya kutaka kujua zaidi na kutojifanya mjuaji ndio silaha za kukufikisha katika umahiri katika kuchora katuni.
BC: Pamoja na kuwa mchora katuni maarufu, wewe pia ni mbunifu wa nguo na mitindo (fashion designer) na pia mtangazaji wa Clouds FM. Nini au nani alikushawishi kuingia katika fani hizo?
KP:Yawezekana dhiki na matatizo ndicho kichocheo cha kumfanya binadamu aweze ku-excel katika maisha, nami pia nataka kuamini kwamba matatizo ndio chanzo cha ubunifu katika kukabaliana na mitihani mbalimbali ya kimaisha, yawezekana ndo maana leo hii mimi ni mchoraji, mtangazaji na mbunifu wa mavazi, pamoja na utashi na upenzi katika fani hizo, bado kiu ya kuwa na financial independence ndio ndoto yangu.
BC: Kwa jinsi ulivyo na kazi lukuki ni wazi kwamba una ratiba ngumu ya kila siku. Unaweza kutuambia kwa kifupi ratiba yako katika siku ya kawaida? Yaani unaamka saa ngapi,unalala saa ngapi nk?
KP:Alarm inaniamsha saa 11 alfajiri, naoga, navaa na kuelekea studio. Naanza kipindi saa 12 mpaka 3 asubuhi, baada ya hapo napumzisha akili kwa kama nusu saa kwa kupitia magazeti mbalimbali then naanza kufikiria wazo la katuni, wakati mwingine kama sina wazo hunichukua mpaka nusu saa kudevelop wazo la katuni, by saa 4 asubuhi naanza kuchora editorial cartoon. Huwa natumia mpaka masaa mawili kutegemeana na aina ya katuni, baada ya hapo, saa sita mchana namkabidhi dereva (wa taxi, sio wangu jamani) apaleke katuni ofisi za gazeti la mwananchi kwa ajili ya kesho yake. Baada ya hapo nageukia upande wa illustrations, mara nyingi huwa nina kazi za taasisi mbalimbali za ku-Simplify text into cartoons kwa ajili popular versions za machapisho mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.
By saa 8 mchana huwa nimemaliza, kama kunakuwa na mikutano ofisini naingia, kwa kifupi by saa 10 jioni nakuwa nimemaliza ingawa wakati mwingine humaliza jioni zaidi, baada ya hapo narudi nyumbani kwa ajili ya kubadilisha nguo then naenda mazoezini. Nikitoka mazoezini huwa sitoki tena nyumbani.
BC: Kwa kumalizia, kuna lolote ambalo ungependa kuwaambia wasomaji na watembeleaji wa tovuti hii?
KP: Ningependa kuwaomba wasomaji na watembeleaji wa tovuti hii wakae tayari kwa nguo zangu ambazo nafanya launching ya nguo za KP kati ya July na August.
Nawategemea sana watanzania walioko nje ya nchi kunisapoti kwa kununua nguo zangu. Kwa kifupi ni kwamba natengenezea nguo hizi Uturuki, India na China. Kwa hiyo jeans, mashati ya kike na kiume, tops, tshirts, skirts na nk zitakuwa zinapatikana. Nakamilisha taratibu za international banking na wanaosafirisha vifurushi ili utapofika muda walio nje waweze kuzipata kwa urahisi, utaratibu wa oda nitawajulisha kupitia tovuti hii.
BC: Asante sana Masoud Kipanya, tunakutakia kila la kheri katika kazi zako.
KP: SHUKRANI.
![]()
Wengi humfahamu kwa jina la Masoud Kipanya, lakini hilo si jina lake halisi, tunaweza kusema hilo ni jina lake la sanaa kwani limetokana na na katuni za Kipanya ambazo huwa anachora.
Jina lake ni i Ali Masoud, jina la Kipanya ni matokeo ya katuni ya Kipanya aliyoibuni zaidi ya miaka 28 iliyopita. Alizaliwa tareha 23 Juni 1972 jijini Dar es Salaam.
Kipanya alianza kuchora katuni akiwa darasa la pili, na alianza kwa kuiga tu katuni za ndani na za nje kama ilivyo kawaida kwa yoyote anayeanza kufanya kitu, ila ‘professionally’ alianza rasmi mwaka 1988, huo ndio mwaka ambao katuni yake ya kwanza ilitoka katika gazeti la Heko.
Amewahi kufanya kazi kama mhariri wa katuni kwenye gazeti la Sanifu na mhariri mtendaji wa katuni gazeti la majira, pia katuni zake hutokea gazeti la Mwananchi.
Licha ya kujizolea umaarufu mkubwa katika uchoraji katuni, katika familia yake hakukuwa na mchoraji kabla yangu, isipokuwa baada ya yeye, mdogo wake naye ameshaanza kuja juu katika fani ya katuni. Licha ya kuwa wazazi wake si wachoraji, lakini mfumo wa maisha yao unatosha kabisa kusema nao pia ni wasanii.
Akizungumzia kazi yake ya uchoraji katuni, Kipanya alisema kuwa, changamoto kubwa anayokumbana nayo ni censorship. Kwa wasioelewa, censorship ni ile kitendo ambacho unachora katuni halafu kabla haijachapishwa inapitiwa na kama itaonekana ina madhara kwa mtu ama jamii Fulani, basi itarekebishwa ama isichapishwe kabisa.
Amesema hayo yamemtokea mara nyingi tu katika maisha yake akiwa katika magazeti mbalimbali. Mara nyingi censorship hutokea pale inapoonekana unachora katuni zinazosumbua mioyo ya walengwa hususani wanasiasa wasiopenda kukosolewa.
Alipoulizwa kama amewahi kupata misukosuko kutokana na katuni zake, Masoud alisema, “nakumbuka siku niliyomchora mtu mnene akiwa amemshika kamba iliyomfunga mbwa ambaye ameandikwa ‘polisi’, maana ya katuni hii ukiangalia kwa haraka haraka ni kwamba jeshi la polisi haliko kwa manufaa ya umma bali kwa manufaa ya watu wachache hasa viongozi wa chama tawala. Hiki kilikuwa ni kile kipindi ambacho wapinzani walikuwa wakibughudhiwa na polisi kila walipotaka kufanya mikutano yao ya hadhara.”
“La pili ni wakati ule mbunge mmoja aliyejulikana kwa jina la Tuntemeke Sanga alipokuwa anaumwa, nilichora katuni inayomuonyesha mheshimiwa Sanga akiwa amelazwa huku akiwa ametundikiwa damu, halafu pembeni yuko serikali akiwa amegeukia upande mwingine huku akivuta sigara kana kwamba hajali, bahati mbaya siku iliyofuata Mzee Sanga akafariki, naikumbuka siku hiyo vizuri, aliyekuwa katibu wa bunge wa wakati huo, Mzee Mlawa, alivamia ofisi za gazeti la majira, bahati nzuri, wakati anaingia mimi nikawa natoka, na pengine kutokana na umbo langu, hakuweza kudhani kwamba pengine huyu ndio masoud kipanya. Kilichoendelea kati yake na mhariri wangu kwa kweli sikukifahamu.”
“Alarm inaniamsha saa 11 alfajiri, naoga, navaa na kuelekea studio. Naanza kipindi saa 12 mpaka 3 asubuhi, baada ya hapo napumzisha akili kwa kama nusu saa kwa kupitia magazeti mbalimbali then naanza kufikiria wazo la katuni, wakati mwingine kama sina wazo hunichukua mpaka nusu saa kudevelop wazo la katuni, by saa 4 asubuhi naanza kuchora editorial cartoon. Huwa natumia mpaka masaa mawili kutegemeana na aina ya katuni, baada ya hapo, saa sita mchana namkabidhi dereva (wa taxi, sio wangu jamani) apaleke katuni ofisi za gazeti la mwananchi kwa ajili ya kesho yake. Baada ya hapo nageukia upande wa illustrations, mara nyingi huwa nina kazi za taasisi mbalimbali za ku-Simplify text into cartoons kwa ajili popular versions za machapisho mbalimbali ya ndani na nje ya nchi. By saa 8 mchana huwa nimemaliza, kama kunakuwa na mikutano ofisini naingia, kwa kifupi by saa 10 jioni nakuwa nimemaliza ingawa wakati mwingine humaliza jioni zaidi, baada ya hapo narudi nyumbani kwa ajili ya kubadilisha nguo then naenda mazoezini. Nikitoka mazoezini huwa sitoki tena nyumbani,” alisimulia Kipanya wakati akijibu kuhusu ratiba yake kwa siku.
Kipanya, ameshiriki maonyesho mbalimbali Tanzania na Afrika Kusini kama mtaalam wa matumizi ya rangi ‘Painter’ na amejishindia tuzo nyingi ikiwa pamoja na tuzo ya kwanza ya katuni Afrika Mashariki.
Mbali na kuchora katuni, Kipanya ni mtangazaji wa kipindi cha Power Breakfast cha Clouds FM, ni mwanamitindo lakini pia ndiye mbunifu wa vipindi vya runinga vya ‘Maisha Plus’ na ‘Inawezekana.’