Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana...

kwa hiyo serikali nao hawaziamini mahakama zetu!? si tulisikia wamefungua kesi sasa wanawateka wanini?
 
Hajatekwa kakamatwa kwa ajili ya kuhojiwa kwa vyovyote vile atakuwa ni kikwazo kwa serikali.
 
Huyo hajatekwa bali kakamatwa kwa mahojiano zaidi. Hata hivyo, reconciliation ndio aende pekee yake ? Naye alikosea kama kweli alienda pekee yake; maana hata watu wenye nia mbaya na Serikali wanaweza kuchukua hatua kama hiyo ili kuleta taharuki zaidi !!!!

Angekamatwa ingejulikana ni kwa sababu zipi na amepelekwa wapi, unasema amekamatwa kwa mahojiano zaidi,unajua amekamatwa na nani na anahojiwa kuhusiana na nini?
 
Huyo hajatekwa bali kakamatwa kwa mahojiano zaidi. Hata hivyo, reconciliation ndio aende pekee yake ? Naye alikosea kama kweli alienda pekee yake; maana hata watu wenye nia mbaya na Serikali wanaweza kuchukua hatua kama hiyo ili kuleta taharuki zaidi !!!!

inawezekana wameenda kujadiliana,sidhani kama atafanyiwa kitu kibaya mana utandawazi umeanika kila kitu,lazima waogope hilo
 
Hapo ndipo tunapokosea, kutumia mbavu katika kusuluhisha migogoro ya aina hii ni kuendeleza migogoro na jamii husika bila ulazima wowote, sitaki kuamini kuwa kwa kumteka/kumkamata Dkt. Ulimboka ndio migomo itakwisha huu ni ubabe ambao hauna nafsi katika nchi zenye demokrasia na utawala wa sheria. Ikitokea Dkt. huyo amedhurika katika kipindi hiki litokuwa doa kwa chama tawala na serikali yake.

Huu ndio ufisadi wa fikra. Pamoja na kuwa migomo hii ya madaktari inaendeshwa bila kuwa na mikakati madhubuti ya kuona kama inafanikiwa au la, bado pia serikali inashindwa kujipanga kuwashawishi kwa hicho wanachoamini na matokeo yake ni kuendeleza ubabe wa wenye dola ambao hawataki kufikiria na wasio na nguvu ya dola wanaodai haki yao ambao pia hawajui hatma ya hilo wanalolifanya.

Kukosekana kwa dhamira inayoeleweka zaidi ya kuamini tu kuwa watu wengi wakifa serikali itatusikiliza kwa sababu madaktari ni muhimu, bado ni tatizo katika migomo mingi ya tanzania na ndiyo maana hakuna mafanikio au yanakuwepo kidogo sana kwa kuwa kila upande unachotaka ni ubabe na siyo kuwa na dhamira madhubuti inayoeleweka na hata inayoainisha njia mbadala endapo iliyopo itashindwa katika kipindi fulani.
 
Wanabodi,

Tuache kuandika lawama tu hapa,tumelalamika sana inatosha inabidi twende hatua moja zaidi.Hili ni tatizo na lazima tudai taarifa rasmi aliko Dr Ulimboka.

Haiwezekani tuambiwe mtu muhimu kama Dr Ulimboka atekwe kihuni alafu tuishie kulalama bila kutafuta suluhisho hasa jukwaa hili likiwa limesheheni wanasiasa,watawala,wanausalama na sisi wananchi. Naomba comments hapa zisiwe za kulaumu tu bali kushinikiza kwa kila njia wapi alipo Dr huyu.

Kama kuna namna ya kudhibitisha hili itakuwa vyema ili nguvu ya umma ifanye kazi.
 
Angekamatwa ingejulikana ni kwa sababu zipi na amepelekwa wapi, unasema amekamatwa kwa mahojiano zaidi,unajua amekamatwa na nani na anahojiwa kuhusiana na nini?

Mkuu, ndio maana nimesema hata watu wenye nia mbaya na Serikali au Drs. wanaweza fanya jambo kama hilo au hata maadui zake wanaweza on hii ndiyo loophole ya kukoroga mambo zadi. Wewe hujui Propaganda ziko kila mahali ?
 
yaan serikali hapo ndo inapochemka!what do u think ikitangazwa kuwa amekamatwa au kitekwa,nchi haitatawalika jamani,mark my word!

hata akiuawa shuguli zitaenda tu Watanzania walishazoeleka kelele mdomoni vitendo zero! tukaeni kimya tufanye kazi watunyonye watufisadi hadi basi tutakuwa tunatumikia adhabu ya sisi kuwa wazembe na wajinga!adaktari wenyewe na usomi na weledi wao wamegawanyika wengine wamegoma wengine wanafanya kazi wengine hawaeleweki lakini wangeamua wakagoma kwa 100% serikali ilishawasikiliza siku nyingi!!
 
Kwanza kabisa ili angalau hii habari iwe credible tunaomba RB No. ya kutekwa kwa Dr. Ulimboka. Unadai tukio lime-ripotiwa polisi

Lakini pia sitashangaa sana kwa serikali kufanya mambo iliyofanya miaka zaidi 20 nyuma. Katika ule mgomo mkubwa ya UDSM wa mwaka 1989, serikali pia ilitumia mbinu hiyo hiyo ya kuwateka viongozi wa DARUSO marehemu Bazigiza na Matiko. Lakini wanafunzi tulisimama kidete hadi wakaachiwa!
 
Inabidi tupate uhakika kwanza na kuona ni mazingira gani huyu jamaa ametekwa/amekamatwa. Hapo yatapatikama mapendekezo mengi ya uhakika.
 
Back
Top Bottom