Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana...

nadhani hata naibu mwanasheria wa serikali anahusika kwa sababu jana alinukuliwa na VOA akisema madaktari wasiporudi kazini kwa kutii amri ya mahakama. Watasikia kesho nadhani hii ni mojawapo ya uthibitisho wa kauli yake. sasa watatujua sisi ni kinanani na sasa ndiyo wamechokoza moto hata na kwenye mahalmashauri madaktari watagoma, solidarity forever bravo madaktari

alizungumza kama mwanasheria sio kama mtekaji kwani hujui mtu akikaidi amri ya mahakama anafanywa nini?
 
Unajuwa ndani ya nchi kuna vyombo vingi vya usalama.vingine vinafanya kazi waziwazi na vinajulikana kwa watu.vingine vinafanya kazi kwa kificho na havitakiwi kujulikana na ofisi zao unaweza ukakuta ni mahandaki na vyote hivyo vinamiliki silaha kihalali na lengo lao ni moja.

Kwa hoja ya mleta taarifa kutekwa nineno zito sana halilingani na nguvu iliotumika kumchukuwa huyu dr.kutekwa lazima itumika nguvu kubwa.nguvu iliotumika hapa ni ya kawaida hivyo atakuwa amekamatwa na baadhi vyombo vya usalama ambavyo unaweza ukakuta hata vyenyewe havijuwani.

Kwa ajili ya kuhojiwa kuhusu mgomo wa madaktari unaoendelea.


Cha kushangaza ni kwamba, wanaenda kumuhoji nini wakati walishakaa meza moja wakayaongea hayo, Jumuiya ya madaktari ikatangaza huu Mgomo na zaidi Swala hili lipo Mahakamani sasa. Hapo ndiypo panapositua watu, ingekuwa huu mgomo umezuka ghafla hapo tungeelewa kuwa system ipo kazini. Ila kama hili ni kweli, basi serikali yetu sikivu ndiyo itakuwa imeharibu kabisa mchakato wa kutafuta suluhu.
 
ni kweli,madaktari wao wamesema aluta continue...mgomo unaendelea,wamesema watakutana na Dr..Uli... hukohuko walikompeleka....(source mimi mwenyewe ni daktari MNH)
 
Tusubiri kwanza kabla ya kuhukumu.

Lakini kama ni kweli hii itakuwa ni kutumia mabavu.


No secret under the sun
 
Nchi hii noana inanyemelea ukurasa mwingine, ukurasa mchafu wa dola kutisha maisha ya raia. Haya mambo ya kuteka watu ni ya kizamani na ni aibu kwa dola (state) kufanya uharamia wa aina hii dhidi ya raia wanaodai haki zao. Kama ni kweli basi serikali yetu itakuwa dhaifu sana. Dunia ya leo ni tofauti na mwaka 47, huwezi kufanya uharamia wa aina hii kwa siri.
 
I agree with Dr. Slaa, kweli serlikali imefikia mwisho wa kufikiri...
 
ni kweli,madaktari wao wamesema aluta continue...mgomo unaendelea,wamesema watakutana na Dr..Uli... hukohuko walikompeleka....(source mimi mwenyewe ni daktari MNH)
 
Kuna thread ipo yenye hii habari, ila nayo bado ni unconfirmed.

Ile ni thread kutoka kurugenzi ya habari ya chama kinachochochea mgomo ndio maana imekaa kichonganishi eti katekwa.
 
Kumteka mtu sio siri na sidhani serikali inaweza kumteka kipindi hiki kigumu tuwe makini na taarifa za aina hii
 
alizungumza kama mwanasheria sio kama mtekaji kwani hujui mtu akikaidi amri ya mahakama anafanywa nini?

Amri gani ya mahakama aliyokaidi?! ameshalifafanua hili...yeye ni kiongozi wa jumuiya ya maDaktari, si kiongozi wa MAT. MAT sio walioitisha mgomo, bali ni jumuiya ya maDaktari....Amri ya mahakama imeelekezwa kwa MAT, si jumuiya ya maDaktari anayoongoza Ulimboka. MAT wameshajibu hao hawajaitisha mgomo kwa hiyo amri haiwahusu...na jumuiya ya maDaktari imeshajibu kuwa haijapata amri yeyote ya mahakama iliyoelekezwa kwao....

Mbona mbumbumbu nyie wagumu kuunganisha dots tu wakati vyombo vya habari vinaandika haya kutwa-kuchwa!
 
yaani ukisikia upumbavu ndio huu sasa kwa kufanya hivi ndio wanafikiri wametatua matatizo ya madaktari siamini kuna watu wanafikiria kijinga namna hii, sasa mi si daktari lakini lolote litakalotokea kwa huyu mtu nitasupport maandamano ya kuing'oa hii serikali chafu, kufa tunaandikiwa its time to die a hero not an idiot. watu wanafikiria kwa kutumia nini jamani?halafu upumbavu mkubwa ni kuwa wanafikiri hawatajulikana it is very obvious who will be the no 1 suspect!
 
this government cannot think beyond vitisho.

kama kweli wamemkamata, madaktari wagome mara mbili ya mwanzo, kwanza kwa ajili ya maslahi yao, na pili kwa ajili ya daktari mwenzao.
 
Huu ujumbe nimeusoma sehemu, nikasema nije humu nione kama imeandikwa...wacha nijipe moyo kuwa aliyenitumia kautoa humu jamvini. Maswali ni mengi..kwanini saa 6 usiku?, kwanini aitwe peke yake....?
 
Back
Top Bottom