EllySkyWilly
JF-Expert Member
- Aug 28, 2020
- 2,204
- 2,083
- Thread starter
- #41
umeshindwa kuelewa sentensi ndogo kabisa.Mlete mada ameleta ujinga. Eti kuna amani ya Mungu na amani ya kisiasa.
Anayetakiwa kuwa na amani ni mwanadamu, na siyo Mungu. Na binadamu ili awe na amani, kunahitajika mambo mengi kwa pamoja, yaani mambo yanayogusa mwili na yale yanayogusa roho.
Aliyeleta mada hii ni mjinga anayedhani kuna wajinga kumzidi yeye ambao wanaweza kupokea hoja yake ya kijinga.
Ni matendo ya mwili ndiyo ambayo huifanya roho iwe na amani au ikose amani. Huyu mleta mada, kwa ajinga tu, hajui kuwa dhambi hutendeka katika mwili, lakini adhabu yake siku ya mwisho ni kwa roho, na siyo mwili.
Uovu wa mwili ndiyo huiangamiza roho. Anayetenda uovu kwa kuoitia shughuki za kisiasa, hana tofauti na anayetenda maovu katika maisha yao ya kawaida. Matendo ya kawaida maovu ya binadamu na yale kwa kupitia siasa, au humletea mwanadamu amani (yeye mwenyewe au wengine) au kumwondolea amani (yeye mwenyewe au wengine).
Kama tunataka kuleta amani ya roho ni lazima matendo yetu na shughuli zetu zote ziwe za haki kwa kadiri ya kweli ya Mungu. Biblia inatamka kuweni watu wa haki katika yote maana haki huleta amani.
Sent using Jamii Forums mobile app
Basi elewa hivi.
Unaweza kuwa na amani ya kisiasa alafu usiwe na amani ya Mungu. Amani ya Mungu inakuwa moyoni. Amani ya Kisiasa inaleta tu utulivu ndani ya nchi lakini sio mioyoni mwa watu,